Dr.Paul Swakala ni kada mkubwa wa CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Paul Swakala ni kada mkubwa wa CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Sep 18, 2012.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Wadau, taarifa nilizozipokea muda mfupi uliopita zimethibitisha kuwa Dr. Swakala, kiongozi wa kamati ya madaktari walioomba msamaha ni kada mkubwa wa CCM.
  Dr.Swakala, akiwa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo cha BUGANDO alifikia hatua kukigeuza Chuo kama Tawi la CCM kwa kuwashawishi wanafunzi wenzake kujiunga na CCM pamoja na kusambaza kadi. Pia daktari mwingine aliyetajwa, ambaye pia ni mmoja wa wale walioomba msamaha na mmoja kati ya wapishi wa move nzima Dr.Nuru Mwambola, aliwahi kutuhumiwa kuwahujumu wanafunzi wenzake wa udaktari akiwa Makamu wa Rais pale Kairuki mpaka kufikia kupigiwa kura ya kutokuwa imani nae.

  Dr.Nuru, ambaye amekuwa Mwanachama mtiifu kwa CCM alikuwa akitumika kushawishi wanafunzi wenzake kujiunga na CCM akiwa chuoni. Ni kwa kutumia nafasi hiyo, yeye Nuru, pamoja na Swakala walikwenda kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Wakili Makene tar 21.08.2012 na kumuomba awakutanishe na Stephen Wassira ili waweze kuonana na Rais.
  Wakili Makene aliwajibu kuwa Wassira yupo nje ya Dar ila ametoa maelekezo kuwa Rais yupo tayari kuwaona ila waombe msamaha kwanza kwa rais, serikali na wananchi. Baada ya agizo hilo ndipo wakaendelea na mchakato wa kukusanya majina ya interns, na kwa taarifa zilizopo ni kwamba ni inters 150 tu kati ya 319 ndio waliotuma majina yao.
  Baada ya kutekeleza agizo la kuomba msamaha hapo jana, baadhi ya wajumbe wa kamati ya Madaktari wa CCM walikwenda wizarani ili kupata mrejesho, na Naibu Waziri aliwajibu kuwa Mwizi akikiri ameiba kinachofuata ni hukumu.

  Habari hii ni kwa hisani ya Daktari ambaye hakupenda jina lake litajwe.

  Shukrani Ritz kwa angalizo lako!
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ndio Breaking News nadhani wewe ni mtu wa tano kuleta thread hii leo.
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Daktari wa ukweli, aliye fikia ngazi ya udaktari kwa uwezo wake mwenyewe bila kuchakachua ama kubebwa kwa namna yeyote ile, anajiamini na anatumia akili yake kuamua. Huyo Dk. Swala Kala amajidhalilisha si mtofautishi na Dk. Tallwater anayelamba viatu vya wafilisi nchi!
   
 4. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,747
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Swakala
   
 5. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mchumia tumbo huyo, he needs to learn from Dr. Kigwalagwala. CCM ina wenyewe
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kamati ya watu 7 ya wachumia tumbo.
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,821
  Trophy Points: 280
  Jamani msiumize vichwa kuhusu wasaliti hawa.Kwani kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo.
   
 8. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huyo ni "Sakala". Don't misuse the word Dr. Angekuwa Dr wa kweli asingefanya utumbo wa kuidhalilisha taaluma adimu namna ile.
   
 9. s

  sapal kihava Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  `` huyu swakala ametufungua macho yetu nafikiri ni muda muafaka sasa kwa selikali kufungua kesi juu yao ya mauaji ya wa Tanzania kwa uzembe wao madaktari . Hakuna mungu nihurumie hapa hawa jamaa wanataka sisi tuamini kwamba DR ulimboka nae alipigwa kwa uzembe wake mwenyewe hii inatokana na kauli yao kwamba ati ``TUNAOMBA MTUSAMEE TULIFANYA MGOMO BILA KUJUA ATHALI ZAKE NASASA TUNAJUTIA MAKOSA YETU MBELE YA WATANZANIA MTUSAMEHE`` Hapa hakuna msamaha selikali ikiwasamehe hawa basi nawafungwa walioko jela waliofanya makosa bila kukusudia waachiwe wote wawe huru.
   
 10. dogojanja 87

  dogojanja 87 JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 885
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyo swala kala na wenzie waloandika hayo majina yao kuomba msamaha washitakiwe haraka,namuunga mkono naibu waziri.kwanza wamekiri makosa,pili wamewasaliti wenzao na watanzania kiujumla kwasababu mgomo ulikuwa ni kwa ajili ya ukombozi wa afya za watanzania wote
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Hana ukada wowote bali ni mganga njaa tu
   
 12. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Asante kwa taarifa mkuu down the line tutawabaini wote
   
 13. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  Duh! sikujua kama na siasa imo humu ndani ya sayansi ya tiba! wasira, kikwete, katibu wa ccm wilaya, hawa walipitia chuo gani cha tiba mpaka wahusishwe na muafaka wa madaktari?! Ki ukweli mimi nilipoona maombi hayo ya msamaha nilipandwa na hasira kiasi nilikaribia kupasua tv! Kuomba msamaha kwa kitendo kilichokuwa kinafanyiaka kwa haki ni upunguani na kuonyesha kuwa wale wote waliowaunga mkono katika harakati zao hawana akili!

  Kama mapambano yalikuwa ni kudai waliyoainisha hakuna kuomba msamaha, bora kufa njaa kuliko kuweka ulimi puani!
   
 14. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu Dr. Swala Kala nimesoma naye A-level na kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu ni mtu ambaye kwa ujumla alikuwa mwoga sana, kwa maana nyingine hakuwa na msimamo. Ninavyofahamu mimi ni kwamba, kama akili zinafanya kazi sawa sawa unapokuwa unafanya jambo fulani ujue madhara yake ili uweke plan B. Inavyoonekana yeye aligoma bila ya kujua madhara yake na hivyo hakuwa na plan B, na pengine aliyokuwa nayo ndo hiyo ya kuomba msamaha. Kwa ujumla Dr. Swala Kala ni msabato feki kwani angekuwa halisia asingegoma tokea mwanzo kwa kuwa alijua kugoma kwake kutasababisha kupotea kwa uhai watu.
  My take:
  1. Walioomba msamaha wote wafunguliwe kesi ya kugoma.
  2. Watakuwa ni kikwazo kikubwa kwa baadae kwa kuwa ikitokea tena wadai mahitaji ya madaktari wao hawatakuwa pamoja na wenzao.
  3. Wataleta uhasama katika ofisi watakazokuwa wanafanya kazi kwani wenzao watawaona kama wasaliti.
   
 15. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mengi yatakuja kubainika kwenye hili sakata.
   
 16. D

  Determine JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati wa kumpokea Ulimboka pale Airport alisema kapata kazi chuo cha KAM na anamshahara mzuri tu. Sas sijui nini kimemsibu?
   
 17. m

  makelemo JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika kama suala la madaktari linahusiana na vyama vya siasa, na kama hao wamefanya kwa interest ya vyama vya siasa na si kwa matakwa yao, wamepotea.
   
 18. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  products za university za Accademy thats why. Nina imani angekuwa kapitia MUCHS haya msingeyaona.
   
Loading...