Dr. Ndumbaro adai TFF haina mamlaka ya kumfungia

Dr. Ndumbaro adai TFF haina mamlaka ya kumfungia

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
Mwanasheria Damas Ndumbaro amesema TFF haina Mamlaka dhidi yake na kuainisha kuwa kama alikuwa na makosa kuvitetea vilabu
vya ligi kuu,TFF ingepeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya
mawakili au kwa mwanasheria mkuu wa serikali. Dkt. Ndumbaro amesema ataendelea kuvitetea vilabu vya Ligi Kuu nchini
na kuainisha kuwa kama alikuwa na makosa kuvitetea vilabu hivyo,TFF
ingepeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya mawakili au kwa
mwanasheria mkuu wa serikali. Kwa maana hiyo, Dkt Ndumbaro amesema ataendelea na shughuli zake
za soka kama kawaida.
 
ngoja tuone na hiyo sheria zenu naona wanasheria wa tff wamesomea kwenye mwembe na ndumbaru amesomea mbinguni
 
  1. Sitti bint Mtemvu!
  2. Diamond na uzushi wa Phd!
  3. TFF na Ndumbaro
  4. Simba na wahujumu wa klabu!
  5. Ukawa
  6. Na bado!
 
namtaka ndumbaru asituvurugia mpira hapa nchini kawavurugi akina wambura hukohuko kwenye simba yako kama hela zilichotwa kwa nini uzingumze leo baada ya kufungiwa peleka unafiki wako huko inasemekana uliwachochea wafanyakazi tazara wagome
 
Ndumbalo njaa itakuua, umevuruga simba sasa tff, au kwasababu kasim kanyimwa uuzaji wa jezi za taifa? Maana ndio mabwana unaowatumikia friends of simba
 
Hili jina la Ndumbalo sipendi kuliona tangu ile siku anamuidhininisha okwi kukipiga msimbaz kutoka Jangwani, kwan hawa watu wa ccm hawamuoni ili wamfanye kama Kibanda!!!!
 
hili group la simba lazima wamchukie malinzi sababu kasim kafutiwa wakala wa vifaa taifa stars mpaka sasa kadhibiti waamuzi kwa kutaka kucheza haki pamoja na vilabu japo leo mtibwa anaachia kwa simba hizo ndizo habari lakini ndumbaru ameusababishia simba hadi ilivyo leo
 
Huyo Ndumbaro naona yuko vizuri sana kwenye sheria, maake kipindi kilichopita aliwashinda nguvu TFF hadi akafanikiwa kumuengua hasimu wake Wambura, leo tena kawavimbia, acha tuone.
 
Another TFF movie. Nchi hii tunao wasanii wengi tu wa filamu.
 
Uwezo wa huyu bwana kisheria ni mdogo sana, hajui ana makosa ya kinidhamu na makosa ya kimaadili, ya kinidhamu ndiyo miaka saba, sasa bado ya kimaadili yanamngojea, pia haelewi maana ya Judicial Organs, hizi ni kamati huru hakuna wa kuziingilia, zinajitegemea hivyo alumbane na kamati siyo Rais wa TFF, pia ni dharau kwa wakili senior kwake kama Jerome Msemwa, anatafuta umaarufu.
 
Kuna vitu vingi vya kufanya mjini Ndumbaro shida moja kubwa huongea mno na kusahau wajibu....hujafungiwa kuwa wakili hiyo ni mamlaka nyingine ....kujihusisha na mpira Daktari elewa....muzeee this is an institution waliokuwa humo ktk kamati ni wanasheria wenzio.....jipange ...bro
 
Pia anapaswa kujua kwa kufungiwa kwake, wanafamilia wa mpira hawapaswi kumuhusisha katika kesi zao zinazohusu mpira, anaweza tumika kwenye masuala mengine ya uwakili lakini yasiyohusiana na mpira.Maana TFF haijamfungia uwakili wake.
 
Dhambi ya Wambura inawahukumu

Tunaapita tu
 
Awatakaa kwa amani mpaka waombe radhi kwa wambura
 
Ni kama movie vile ila nduguzanguni shuguli yenu nyumayake ni dhambi aliyofanyiwa wambura mkikaamkapata mud a mwomben radhi tu hat a kisirisiri mambo yatakuwa mswano
 
Tunapoelekea tutazalisha Tff Ukawa name Mungu apitishie mbali
 
Uwezo wa huyu bwana kisheria ni mdogo sana, hajui ana makosa ya kinidhamu na makosa ya kimaadili, ya kinidhamu ndiyo miaka saba, sasa bado ya kimaadili yanamngojea, pia haelewi maana ya Judicial Organs, hizi ni kamati huru hakuna wa kuziingilia, zinajitegemea hivyo alumbane na kamati siyo Rais wa TFF, pia ni dharau kwa wakili senior kwake kama Jerome Msemwa, anatafuta umaarufu.
Lakini ni Daktari (PhD Holder) na kama sikosei nilimsikia redioni akieleza jinsi alivyosoma. Au naye ni 'Dr' kama Maji Marefu na bosi wake, au ndio elimu ya Kitanzania!?

 
Kama TFF haina mamlaka rufaa kakata ya nini? Aseme wamekosea hilo litakuwa sawa.
TFF ya sasa hivi inaelekea kwa ile FAT ya Ndolanga. Ni ubabe na ufisadi uliojificha kwenye usiri. Nguvu iliyotumika kumtetea Malinzi wakati alipofanyiwa mizengwe kwenye uchaguzi ndio hiyo hiyo itatumika kumwondoa.
 
Back
Top Bottom