Dr. Ndumbaro adai TFF haina mamlaka ya kumfungia

Dr. Ndumbaro adai TFF haina mamlaka ya kumfungia

Kafungiwa na vyombo halali vya TFF vinavyojitegemea ambavyo Rais WaTFF hana mamlaka ya kuviingilia, na bahati njema katiba inasema viongozwe na wanasheria.Na aliyeongoza kikao alikuwa ni wakili maarufu Jerome Msemwa mmoja wa wadau wakubwa wa Simba.Haki imetendeka, na ikumbukwe Ndumbaro aliweka wakili kwenye kesi hii hili amtetee.Kuhusu ufisadi ni habari za kuokoteza watu waliochanganyikiwa, hivi kama kuna ufisadi si angetoa nyaraka.Hivi TBL waone ufisadi wasijitoe?tuache kudanganywa.kuna mambo ya msingi anataka kuficha, ila siku si nyingi nchi nzima itamtambua kuhusu anayofanya kwa kivuli cha soka.alikuwa wakala mnajua aliyoyafanya kuhusu Joseph Kaniki na Yusuf Soka, amewahi kujiita match agent je Tanzania imeshawahi kuwa na wakala wa mechi?
 
Lakini ni Daktari (PhD Holder) na kama sikosei nilimsikia redioni akieleza jinsi alivyosoma. Au naye ni 'Dr' kama Maji Marefu na bosi wake, au ndio elimu ya Kitanzania!?

Majimarefu alishauacha u Dr kitambo sana, hivi sasa ni Le Profeseri.
 
Huyu jamaa mwanasheria mzuri tu,tatizo anatumia usomi wake kuleta vurugu kwenye soka..refer to ishue of okwi,wambura nk
 
Wasiomjua wanaweza kudhani ni mwanasheria mzuri, uelewa wake ni mdogo, issue ya okwi hata angeenda mwenyewe angeshinda.mtu makini hawezi kukubali kutetea vilabu kama wakili dhidi ya TFF, wakati akijua kuwa ni mjumbe wa bodi ya ligi chombo kilichopo chini ya TFF.Lakini pia kama mwanafamilia wa Soka anajua vilabu vya ligi kuu ni wanachama wa moja kwa moja wa TFF, hivyo kuna jinsi ya vilabu kulalamika kwenye mfumo rasmi.Anajua taratibu za soka zilivyo, lakini yeye anaamua kuleta vurugu eti uchaguzi ufanyike ili agombee Urais wa TFF.
 
Lakini ni Daktari (PhD Holder) na kama sikosei nilimsikia redioni akieleza jinsi alivyosoma. Au naye ni 'Dr' kama Maji Marefu na bosi wake, au ndio elimu ya Kitanzania!?

Mwenye Thesis yake ai-upload tuisome na kuichambua tuone umahiri wake.
 
Mwanasheria Damas Ndumbaro amesema TFF haina Mamlaka dhidi yake na kuainisha kuwa kama alikuwa na makosa kuvitetea vilabu
vya ligi kuu,TFF ingepeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya
mawakili au kwa mwanasheria mkuu wa serikali. Dkt. Ndumbaro amesema ataendelea kuvitetea vilabu vya Ligi Kuu nchini
na kuainisha kuwa kama alikuwa na makosa kuvitetea vilabu hivyo,TFF
ingepeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya mawakili au kwa
mwanasheria mkuu wa serikali. Kwa maana hiyo, Dkt Ndumbaro amesema ataendelea na shughuli zake
za soka kama kawaida.

huyu bwana,ndumbaro ni laana yakina wambura na wenzake. inamtafuna na ndiyo inawatafuna hata klabu ya simba. wawa ombe msamaha wakina wambura.
 
Uwezo wa huyu bwana kisheria ni mdogo sana, hajui ana makosa ya kinidhamu na makosa ya kimaadili, ya kinidhamu ndiyo miaka saba, sasa bado ya kimaadili yanamngojea, pia haelewi maana ya Judicial Organs, hizi ni kamati huru hakuna wa kuziingilia, zinajitegemea hivyo alumbane na kamati siyo Rais wa TFF, pia ni dharau kwa wakili senior kwake kama Jerome Msemwa, anatafuta umaarufu.

sasa senior ikitokea amekosea aachwe tu.......
 
Kafungiwa na vyombo halali vya TFF vinavyojitegemea ambavyo Rais WaTFF hana mamlaka ya kuviingilia, na bahati njema katiba inasema viongozwe na wanasheria.Na aliyeongoza kikao alikuwa ni wakili maarufu Jerome Msemwa mmoja wa wadau wakubwa wa Simba.Haki imetendeka, na ikumbukwe Ndumbaro aliweka wakili kwenye kesi hii hili amtetee.Kuhusu ufisadi ni habari za kuokoteza watu waliochanganyikiwa, hivi kama kuna ufisadi si angetoa nyaraka.Hivi TBL waone ufisadi wasijitoe?tuache kudanganywa.kuna mambo ya msingi anataka kuficha, ila siku si nyingi nchi nzima itamtambua kuhusu anayofanya kwa kivuli cha soka.alikuwa wakala mnajua aliyoyafanya kuhusu Joseph Kaniki na Yusuf Soka, amewahi kujiita match agent je Tanzania imeshawahi kuwa na wakala wa mechi?

umelazimisha kupachika neno simbavili ipate uheyawani...
 
aveva nae kaingilia kati,huyu hapa hebu soma alichokisema.....

Uongozi wa Klabu ya Simba umelivaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kauli yao ya kuzitaka klabu kutojihusisha na wakili wa kujitegemea Damas Ndumbaro kupitia kampuni yake ya Maleta & Ndumbaro Advocate.

Rais wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa kwa upande wao bado wanaendelea kumsapoti Ndumbaro kwa asilimia 100 kwa sababu wao ndiyo waliomtuma na kudai kuwa watashirikiana naye kama kawaida katika masuala ya soka.

“Kamati iliyoshughulikia suala hilo ni huru na kwa upande wetu Simba tupo mstari wa mbele kuhusu suala hilo na tunamsapoti.

“Tutaendelea kumtumia Ndumbaro kama kawaida kwani tunatetea haki yetu na tunapinga vikali makato ya asilimia tano ya mapato.

“Hakuna waraka wowote tuliopewa klabu kuhusu jambo hilo,” alisema Aveva.

TFF ilitangaza kumfungia Ndumbaro kujihusisha na soka kwa miaka saba kutokana na kile kilichoelezwa kukiuka kanuni kadhaa za shirikisho hilo.
 
Attachments

  • aveva kanga.JPG
    aveva kanga.JPG
    93 KB · Views: 41
Hayo ni magazeti tu Aveva aandike barua asaini aone kamati ya nidhamu itavyomshughulikia, atulie na mambo yake ya Simba ambapo ni mwenyekiti jina, wanaoongoza wala hawakugombea.
 
ndumbaro kaza buti nenda cas ikadai haki yetu malinz ni jambaz
 
Tena mwanasheria Ndumbaro leo kwenye gazeti la mwanaspoti kamtukana Wakili maarufu Jerome Msemwa kwa kumuita kamati yake ni kichaka, jaman hivi hata mfumo wa kimahakama ukishindwa mahakama ya chini unaitukana, huyu hana maadili kabisa, jinsi anavyoongelea watu binafsi kwa masuala ya kitaasisi inaonyesha jinsi asivyo na weredi, hivi wanasheria mtuambie ni wapi mwanasheria anamtukana mwrnziye hadharani, hii ni kwa vichaa tu.
 
Back
Top Bottom