Dr Mwigullu: Bajeti ikishapitishwa na bunge ni Sheria, sitaweza kubadili chochote kwenye Tozo!

Waziri wa fedha Dr Mwigullu Nchemba amesema bajeti ikishapitishwa na bunge inakuwa ni sheria hivyo waziri hana nguvu ya kufuta wala kubadili chochote

Dr Mwigullu atakuwa hewani siku ya Jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 ITV akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo Chanjo ya Corona, bei ya petrol na Tozo katika miamala ya simu.

Source: ITV

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Kwa hiyo Wananchi wachukue / wafanye UAMUZI kama kwenye SAKATA LA BEI YA MKATE HUKO KWA WENZETU WAJANJA?
 
Tembeeni kifua mbereeeee ! Hii nchi ni tajiri sana.....

Maendereo hayana chamaaaa...

MATAGA : KWERIIII....

Kiufupi tu ni kuwa laiti Watanzania kwa akili zao wangekubali kufanya maamuzi October 28 basi tusingekua huku ! Hiyo ndio siku Tanzania ilizikwa rasmi akiwa hai! Itachukua muda sana kueleweka na pia itachukua muda nchi kurudi kwenye mstari
Huwezi kukabidhi nchi kwa wahuni, ukipatikana upinzani wa kueleweka watapewa nchi
 
Waziri wa fedha Dr Mwigullu Nchemba amesema bajeti ikishapitishwa na bunge inakuwa ni sheria hivyo waziri hana nguvu ya kufuta wala kubadili chochote

Dr Mwigullu atakuwa hewani siku ya Jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 ITV akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo Chanjo ya Corona, bei ya petrol na Tozo katika miamala ya simu.

Source: ITV

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Mwigulu asikwepe lawama , hivi aliyeandaa hayo mapedekezo ya hizo tozo ni nani kama sio yeye? Hapa amemchonganisha Rais na wananchi wake pakubwa sana!
Kionngozi unayepewa mamlaka makubwa kwenye wizara nnyeti kama ya fedha unapaswa kuwa mwepesi wa kung'amua athari za kiuchumi katika mipango unayoipanga!
 
Back
Top Bottom