Dr. Mwakyembe: Sitolipiza kisasi

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Dr.Mwakyembe-Sitolipiza kisasi ni moja ya vichwa vya habari nilivyovisikia leo ktk magazeti ya Tanzania

je kuna ukweli wowote juu ya habari ama ripoti ya Mwana JF aliyoitoa hapa,juu ya afya ya Dr MWAKYEMBE?

Mwakyembe: Namwachia Mungu

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameshindwa kueleza moja kwa moja kama amelishwa sumu, badala yake amemwachia Mungu juu ya wabaya wake waliotenda kitendo hicho.
Dk. Mwakyembe alisema hayo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya afya yake tangu arejee kutoka nchini India alikokwenda kwa matibabu.
Oktoba mwaka huu, Mwakyembe alikimbizwa nchini India kwa matibabu zaidi baada ya hali yake ya afya kuzidi kuzorota, huku tetesi kizitolewa kwamba amelishwa sumu na watu wasiojulikana.

Hata hivyo, jana Dk. Mwakyembe alisita kuweka wazi ukweli wa suala la kulishwa sumu na badala yake alisema yeye si mtu wa kisasi kwa waliomtendea hayo, hivyo akasema anashukuru amerudi salama akiwa na afya njema.

"Siwezi kueleza moja kwa moja kwamba nimelishwa sumu, ninachoweza kusema nilikuwa na hali mbaya sana wakati napelekwa India kwa matibabu na nimerudi salama nikiwa na afya njema, namwachia Mungu alipe kisasi, mimi si wa kulipa," alisema kwa kifupi.

Dk. Mwakyembe ambaye alivalia kofia nyeusi ya pama kichwa huku akiwa na gloves mikononi pamoja na T-shirt ya mikono mirefu, vilivyoweza kuficha ngozi yake isionekane kabisa, alisema anafahamu siri ya ugonjwa wake na kamwe hayuko tayari kuieleza.

Kwa mujibu wa maelezo yake, uchunguzi wa ugonjwa uliokuwa ukimsumbua hadi kupelekwa nchini India, tayari umetumwa Wizara ya Afya, hivyo ni jukumu la wizara kuweka taarifa hadharani.

na Datus Boniface,Tanzania daima
 
kama unawajua lipiza kisasi baadaye omba sala ya toba, Mungu atasamehe!
 
kishalegea huyu..ndo basi tena..mdomo umekuponza mzee wangu..wenzio hawapigani vita vya maneno wanafanya vitendo sasa yamekukuta
 
Hata kama angetaka kulipiza kisasi,wenzie ndio wamekwisha mtangulia wanamuhesabia siku tu kwani hiyo sumu waliomtengeneza nayo itamdhoofisha taratibu!!
 
alipize kisasi kwani anamjua aliyesababisha aumwe?jamaa ana bonge la nyumba(ghorofa),kumbe unaweza kujiita mpambanaji wa ufisadi hata kama ni tajiri kama mwakyembe?
 
alipize kisasi kwani anamjua aliyesababisha aumwe?jamaa ana bonge la nyumba(ghorofa),kumbe unaweza kujiita mpambanaji wa ufisadi hata kama ni tajiri kama mwakyembe?

Ufinyu wa mawazo yani ukiwa na nyumba kubwa basi wewe ni fisadi?!! akili za kijinga hizo..mwakyembe amejenga hiyo nyumba zamani kama hujui lofa uliza...hata kabla hajawa mbunge
 
POle kwa yalokukuta. Lakini mbona serikali inakuwa kimya hivyo na hawalitolei maelezo ? Kama wanakaa kimya basi kunaukweli ndani yake.
 
Kabla hajawa mbunge kajenga nyumba hiyo. Ndo maana ya kiongoz kuweza kujiongoza mwenyewe kabla hata wananch hawajakupa dhamana! Au Obama hana ghorofa?
 
kama unawajua lipiza kisasi baadaye omba sala ya toba, Mungu atasamehe!
Imeandikwa, Mungu hawezi kujaribiwa na uovu. kamwe usije ukamshauri mtu kutenda dhambi kwa makusudi sababu tu atatubu. " Mungu si mwanadamu" kumbuka hilo.
 
Ni vigumu sana kumdanganya Mtanzania wa leo tena alieelimika, Mwakyembe ni msanii tu hana lolote, huwezi kushindana na serikali unayoitumikia na ambayo umeahidi na umeapa kuilinda na kutunza siri zake.

Mpambanaji wa kweli hawezi kuwa ndani ya CCM, hapa tusidanganyane!!
 
"Siwezi kueleza moja kwa moja kwamba nimelishwa sumu, ninachoweza kusema nilikuwa na hali mbaya sana wakati napelekwa India kwa matibabu na nimerudi salama nikiwa na afya njema, namwachia Mungu alipe kisasi, mimi si wa kulipa," alisema kwa kifupi.

Hayo maneno aliyoyasema yanaonyesha kabisa kwamba hana uhakika kama ililishwa sumu. Sijafurahishwa na maneno yake aliyosema kwamba namwachia Mungu alipe kisasi, hapo kakosea Mungu halipizi visasi, hapo ni kama kusema Mungu anaweza kufanya uchafu wa kulipiza kisasi. Pale msalabani alisema Baba uwasamehe kwani hawajui wayatendayo, hakusema Baba nakuwachia uwashughulikie.
 
wanaolopa kisasi huwa wanasema?
Atulie nae awafanyie kazi hao wahuni taratibu kama ambavyo polonium inavyofanya kazi taratibu mwilini mwake.
 
Ni kweli ni vigumu kupambana na ufisadi ukiwa ndani ya CCM, lakini ni jambo zuri vilevile kwamba watusaidie kuiua CCM wakiwa ndani si unakumbuka wakina Raila Odinga Walivyoiua Kanu Wakati ule wakitokea ndani ya Kanu Yenyewe na alitoka kanu na Akina KALONZO MUSYOKA ,JOSEPH KAMOTO,SAITOTI.Mimi nafikili wanaweza kuendelea kuwa CCM,lakini watoke CCM 2015 Kwa kundi kubwa wakipinga mchakato wa uraisi kwani kama ilivyo ada mwenye fungu kubwa ndiyo atashinda.
 
POle kwa yalokukuta. Lakini mbona serikali inakuwa kimya hivyo na hawalitolei maelezo ? Kama wanakaa kimya basi kunaukweli ndani yake.

Hivi na ule waraka wake uleee. Ulioenda kwa IGP mwema haukuwa ukihitaji feedback?kama jibu ni ndio basi kulingana na statement zake ilipaswa abanwe kisawasawa. Ili anyooshe maelezo huwezi [kibinadamu]kumwacha adui yako nje ya mlango wako kisha uingie kulala bila kufunga mlango huku ukijua wazi kuwa adui yako huyo anasubiri ulale usingizi ili aku uwe
 
kama unawajua lipiza kisasi baadaye omba sala ya toba, Mungu atasamehe!

Atakuwa ametoa sababu nzuri kabisa ya kummaliza mchana kweupe usifikiri kila anayesema namwachia mungu anamjua mungu au ni kwa ridhaa yake kutolipiza Hebu jikumbushe hao unaodhani ni adui zake au uliosikia,then utazame nani wa kutishwa na HM
 
mnafiki wa kisiasa tu... mara ntasema yote, mara sitalipiza kisasi, mara namuachia mungu!! utalipiza kisasi kwani una uhakika kuna mtu amekufanyia??

guess work is killing our politico men
 
Ufinyu wa mawazo yani ukiwa na nyumba kubwa basi wewe ni fisadi?!! akili za kijinga hizo..mwakyembe amejenga hiyo nyumba zamani kama hujui lofa uliza...hata kabla hajawa mbunge

mkuu mbona mapovu yanakutoka?wapi nimeandika mwakyembe ni fisadi?soma uelewe sio kukurupuka chooni bila kutawaza..
 
kishalegea huyu..ndo basi tena..mdomo umekuponza mzee wangu..wenzio hawapigani vita vya maneno wanafanya vitendo sasa yamekukuta

kwani mkuu ulikuwa unataka afanyeje,maana kama ripoti ilikuwa ni lazima isomwe bungeni na kuanzia hapo ndipo maadui wakajitokeza sasa unadhani yeye angefanyaje? ameumizwa kwa kulitetea taifa letu,yatupasa tumpe nguvu na moyo
 
Back
Top Bottom