Dr. Mwakyembe: 90% ya watangazaji hawana taaluma

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,165
164,626
Waziri wa habari amesema asilimia 90 ya waandishi si wanataaluma.

======

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe amesema asilimia 90 ya watangazaji wa redio na televisheni nchini hawana sifa za kitaaluma katika tasnia ya habari.

Waziri Mwakyembe alitoa taarifa hiyo jana bungeni alipokuwa anawasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ya Sh bilioni 28.2. Kwa mujibu wa Waziri, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifanya ukaguzi wa kina katika huduma za utangazaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ikihusisha ukaguzi wa vifaa vya utangazaji, vyumba vya habari, maktaba, mikataba ya ajira pamoja na sifa za watangazaji katika vyombo vya habari.

‘’Vituo vyote vimeonesha kuwa na ubora wa huduma inayotolewa, hata hivyo asilimia 90 ya wafanyakazi wamebainika kutokuwa na sifa za kitaaluma za uandishi wa habari na utangazaji na kwamba hiyo ndiyo changamoto kubwa inayoikabili tasnia ya habari,’’ alisema Dk Mwakyembe.

Ukiacha changamoto hiyo, Waziri alisema taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake zimefanya vizuri katika majukumu yake kwa mwaka wa fedha uliopita, miongoni mwake ni pamoja na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wazalishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo na Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC).

Taasisi nyingine ni TCRA, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo na Baraza la Michezo la Taifa (BMT). Dk Mwakyembe alitoa pongezi kwa TSN kwa kuboresha majukumu yake ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha na kuongeza kwamba kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 magazeti hayo ya serikali yamevutia wasomaji wengi na pia kuongeza idadi ya watangazaji katika magazeti hayo kiasi cha kuongoza katika matangazo kwenye vyombo vya habari.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Juma Nkamia aliipongeza serikali kwa kutenga Sh bilioni 2.4 kwa ajili ya kununua mtambo mpya wa kisasa wa uchapishaji magazeti kwa ajili ya TSN.

“Kamati inapendekeza mtambo wa sasa wa kuchapisha magazeti wa Dar es Salaam uhamishiwe makao makuu ya serikali Dodoma ili kurahisisha usambazaji wa magazeti katika mikoa jirani ya Tabora, Mwanza, Iringa na mikoa mingine

Chanzo: Habari Leo
 
Unaposema kitu ni vema ukawa na takwimu. Waandishi wangapi wapo? Wangapi na kwa asilimia ngapi wanakidhi unayoita vigezo? Vilevile, wangapi na ni aslimia ngapi hawakidhi vigezo? Unashindwa hata na VEO hapa kwetu anatoa taarifa za vyoo kwa takwimu zinazoeleweka? Kuongea bila vibwagizo vya kusimamia hoja ni upuuzi mtupu au ni kuongea "vapour"!
 
Utawezaje kufanya kazi bila kupata taaluma yake?
Taaluma ya uandishi huhitaji darasa analolizungumzia kwani uandishi ni fani pana sana na huwezi kuipata huko ila kazini na kwenye taaluma mbadala.

Hizi ni hoja za kubana uhuru wa vyombo vya khabari kwa kuzuia wengi wenye uzoefu na vipaji kutupasha habari.

Kwa hizi soga za akina Mwakyembe Dr. Gupta wa CCN hana sifa na kwa sheria yetu hii isiyo na weledi leo hii Dr. Gupta hawezi kuajiriwa na kampuni yoyote ya habari kisa hana cheti cha habari.
Hivi tangia lini vyuo vya uandishi wa habari vikaanda wahabarishaji wa fani kama udaktari, uhandisi, sheria, n.k?
 
tutegemee uhakiki wa waandishi wa habari soon...
Lengo ni kuwafuta wale ambao wanawakosoa kwa madai potofu hawana sifa! Uzoefu walionao na taaluma mbadala za uandishi wa habari hawazitambui.

Ukiwa na B.A wewe hauna sifa ati mpaka uwe na B.A Mass communication au journalism!

Ndiko tulikofikia hadi sasa katika mikakati ya kuminya uhuru wa vyombo vya khabari
 
Duuu alijuaje au nao walipekeka vyeti kuhakikiwa
Mara nyingi simuamini huyu kiumbe anatoa habari za kukurupuka bila data nakumbuka hata issue ya vyeti vya ndoa hadi akapigwa stop na mkuu wa nchi
Kwa hiyo hata wa TBC na Uhuru ni majanga tupu?
 
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/22653-90-ya-watangazaji-si-wanataaluma

Mwakyembe-Bungeni_478_291.jpg
Screenshot_2017-05-06-16-25-28.jpg
 
Hata miezi miwili bado haijaa ofisini ameshaanza kutoa habari isiyo na utafiti.... Kwa hiyo anataka kuhakiki vyeti??
 
Back
Top Bottom