Dr. Mponda na Nkya wanasubiri nini????

PrN-kazi

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
2,900
444
Waziri wa Afya(Dr, Mponda) na Naibu wake(Nkya) ebu kaa pembeni kwani nyie ndo mmeonekana kuwa kikwazo kwa maDaktari. kuendelea kung'ang'ania nafasi hizo ni adhabu kwa wananchi:

ni dhahili sasa vifo vya raia vitakavyotokea kutokana na mgomo wa Ma-Daktari nyie ndo wa kulaumiwa.
 
Rais Kikwete hapendi kuwawajibisha mawaziri wake, nimuombe awabadilishe wizara wote wawili ili aendelee kuwaona sura zao wakiwa mawaziri ila pale waondoke ili wananchi waendelee kupata huduma kwa kuwa uwezo wa kwenda India haupo.
 
wanajali?
wanajali???? kwani wao na maDaktari nani anajali zaidi, maDaktari madai yao yako genuine kabisa(vitendea kazi, mazingira bora ya kazi na maslahi): wakati akina Mponda wanapewa kila kitu Nyumba, Usafiri mzuri na maslahi wakati kinachofanyika hakipo zaidi ya kulinda CHAMA sasa hapo wanajali nini????????????
 
Matatizo ya Wizara ya Afya hayajaanza awamu ya Mponda kinachoonekana hapa ni kwamba Mponda amerithi matatizo lakini anaonekana ndiye mwanzilishi wake.


Prof David Mwakyusa ni prof katika fani ya tiba ni nani alijua angeweza kushindwa kuleta mabadiliko ya sekta ya Afya?

Tuna safari ndefu ya kutafuta chanzo cha kweli cha matatizo yanayoikumba wizara ya Afya na ndipo tutajinasua na migogoro hii.
 
Nadhani ni uleule utamaduni wetu wa kutopenda kuwajibika na kuona uwajibikaji kuwa ni defeat!!!
 
Back
Top Bottom