Jumamosi moja, ya Mwaka 2010,May, CHADEMA iliandaa mkutano na makada wake wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu vya jijini Dar-Es Salaam
Katika mkutano huo ,Prof. Baregu,pamoja na mambo mengine alipata fursa kuelezea sakata lake la kunyimwa mkataba na serikali kufundisha UDSM na kuwa alikuwa akitaraji kupatatiwa jibu kutoka serikalini Jumatatu iliyokuwa ikifuata.
Prof.Baregu aliweka wazi ,kama wengine walivyokuwa wakielewa kuwa chanzo cha sakata hilo ilikuwa ni ushiriki wake kisiasa katika CHADEMA.(Ndugu zangu,kama tuzingatia ukweli kuwa Baregu ni Profesa wa Siasa tutaona ni sahihi kimantiki kwake ku -practice nadharia za taaluma yake aipendayo katika chama akipendacho !)
Baregu alimtahadharisha mapema Kitila Mkumbo,aliyekuwa ameketi meza kuu, kuwa yaliyokuwa yanamkuta yeye ilikuwa ni matokeo ya hila za kisiasa kutoka kwa watawala.Na kwamba yeye (Baregu) alikuwa yupo tayari kulipa gharama za uamuzi wake kushiriki siasa katika CHADEMA, hakuwa tayari kurudi nyuma na kwamba alikuwa tayari kwa jibu lolote!!Hii inagusa sana hisia.
Tunatambua, sote ,hata baada ya watawala kumnyima mkataba ,Baregu hakupata kutetereka .Na wala Kitila hakutishika kwa yaliyokuwa yamempata Mwanataaluma mwenzake.Wote wawili wanastahili pongezi.Historia itawakumbuka kwa kuishinda hofu.