Dr. Mkumbo aula UDSM

Katufu

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2012
Posts
523
Reaction score
309
Kwa mujibu wa press release iliyotolewa juzi tar 16/7/2012 na ofisi ya uhusiano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kamanda Dr. Kitila A. K. Mkumbo ni mmoja wa walioteuliwa kuwa wakuu wa vitivo katika vyuo vikuu vishiriki vya elimu vya Mkwawa na Dar es Salaam.

Huku Dr. Mkumbo akiwa ameteuliwa kuwa mkuu wa kitivo cha elimu katika chuo kikuu kishiriki cha elimu, Dar es Salaam yaani (Dean, Faculty of Education at the Dar es Salaam University College of Education).

Kwa kweli anastahili, Hongera sana Kamanda Mkumbo
 
Hongera Dr Mkumbo.Huwa unanifurahisha sana kwanye kile kipindi cha This week in perspectives!
 
hongera kamanda wanatambua umuhimu wako.
 
All the best mbunge mtarajiwa!
 
Isije ikawa HONGO ya kukunyamazisha ili 2015, usiende Iramba Magharibi kuchukua JIMBO LETU.

Nafikiri Nchemba masaburi yatamuwasha akisikia habari hii.

All in All congratulations Dr. Mkumbo and wishing you the best in your new position.
 
Kwa niaba ya Mwigulu Nchemba na Tendwa naomba kukupa pongezi za dhati kwa hilo..
 
Ni kweli Dr. Kitila anatoka jimbo la Chemba mwigulu?
 
Huyu alikuwa President wa Daruso mwaka 1998 na alifanya vizuri sana.

Akiwa A level Pugu pia alikuwa kiongozi.

Akiwa mwalimu UDSM amekuwa kiongozi wa UDASA ambao ni Umoja wa Wahadhiri wa UDSM (Vice Chairman).

Hizi zote ni nafasi za kuchaguliwa na watu.

Uongozi uko damuni mwake na pote alipowekwa kuwa kiongozi ali deliver.
 
Badilisha kichwa cha habari "aula" ndiyo nini, una maana haendi kufanya yaliyotarajiwa bali kujineemesha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…