Yafuatayo yalishawahi kuandikwa. Wakati huo pia tujiulize ktk wote hawa wenye ushujaa wa kughushi vyeti, walitokea vyuo gani? maana vyuo vyote vilikuwa vya serikali (Mzumbe, UD, SUA MUHAS). Yanweza kuwa ni malezi ya waalimu wao.
JK ulishapewa ushahidi na Msolla juu ya Mathayo na wenzake sasa mbona kimya
http://www.jambonetwork.com/blog/?p=8198
March 20, 2008
Ndugu Rais najua hili si geni kwako ila ugeni ila ugeni ni kwamba hukujua kama tunajua kwamba Msolla amesha kupa Uhakika juu ya Elimu ya Mathayo mwanamtandao na wengine kwamba wana vyeti fake .Je unangoja nini hadi muda huuu kufanya kweli na tena umemrudisha Mathayo madarakani wakati Msolla alikupa taarifa siku nyingi .\
Sasa leo tunaweka hapa habari nzima na maisha ya Mathayo hadi kufikia hapo alipo .
Nimekutana na Mjasiamali huku Kijijini Iringa kasoma lakini kachoka sana anaanza kushangaa mambo ya Tanzania na jinsi mara ya mwisho amakutana kijijini kwao na aliyekuwa waziri wa Elimu ya Juu bwana Msolla na kumuuliza Mwalimu inakuwa jama wana vyeti feki nawe umekaa kimya ?Maongezi na mengineyo soma hapo chini huyu msomo mwenye degree yake yuko analima Nyanya na kufuga Mbwa kwa ajili ya kuuza huko Iringa kwa kitoweo anasema haya maana anamjua sana Mathayo Matayo David Msuya nimekuwa naye tokea high school Tosamaganga Iringa, akifanya CBG 1989-91, tukiishi bweni la Mwenge. Tulimaliza wote high school na Matayo alifaulu vizuri sana alipata daraja la kwanza point 7. Si kwamba alikuwa kifaru sana darasani, Matayo alisaidiwa na kaka yake aliyekuwa aakifundisha Mkwawa teachers college, nakumbuka usiku ule Matayo alipotea kwenye premises za Tosamaganga, na alikuwa alitokea mjini na kuingia kwenye mtihani Matayo aliiba mtihani na kufaulu sana masomo ya Chemistry na Biology kinyume na uwezo wake darasani.
Tulikwenda na Matayo JKT itende, Mbeya. Kwa kuwa mwenzetu alikuwa amefaulu sana kuliko sisi watoto wa masikini ambao hatukuweza kuiba ama kuchangia mtihani ule. Matayo alichanguliwa kwenda kusoma Makelele Uganda kwa kupitia mfuko wa mwalimu Nyerere, ambao ulikuwa unsomesha wanafunzi walifanya vizuri. Ajabu, Matayo alichukua zile pesa na hakwenda Uganda, akaamua kusoma Sokoine University degree ya tiba ya mifugo (Bachelor of Veterinary Medicine) mwaka 1993-1997. Matayo alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyekuwa na radio yenye double deck, (system) na TV set. Aliweza kununua hivyo kwa pesa aliyotakiwa kusomea Uganda. Kwa kuwa alikuwa na double scholarship ile ya Elimu ya juu ya Tanzania na ile ya Mwalimu Nyerere alikuwa na pesa sana aliweza kuchukua wasichana wazuri wote pale chuoni ikiwa ni pamoja na Mugros. Nakumbuka aliachana na Betty Manase kwasababu Matayo alifumaniwa akiwa na msichana mwingine wa kijijini, na Mathayo alipigwa kibuyu.
Siasa alizianza rasmi mwaka 1995 alitumia TV yake kwenda kuonyesha vijijini madhara ya vyama vingi, alitumia mapigano ya Rwanda na Burundi kama kutishia wananchi wasikubali upinzani na kipindi kile wananchi walikuwa wepesi kuelewa kumbuka TV hazikuwa nyingi Tanzania kipindi kile. Alijijengea umaarufu sana ndani ya chama mkoani Morogoro na kitaifa. Aligombea ujumbe wa NEC mkoa wa Morogoro kundi la vijana alishinda.
Matayo alimaliza SUA 1997 na kupata kazi ya kufundisha chuo kimoja Botswana. Kwa kuwa mjumbe wa NEC alikuwa karibu na akina Lowasa, JK na vingunge wengine aliweza kuwa anaonana na akina Makamba na akawa ni mwanamtandao. Matayo mwaka 1997 alifanya usanii wa hali ya juu alichangisha wanafunzi wa miaka ya mwisho Shs 10,000/= ilikupata form za kutafutiwa kazi Botswana alikusanya zaidi ya Tshs million 2,000,000 ambazo alitumia kununulia gari. Hahahahah…Pia Dr Matayo alirudi Tanzania na kudanganya wanafunzi wa SUA na kwa kutumia mabasi ya Aboud alipeka zaidi ya wanafunzi 200 Dodoma kupokea kadi za sisiem chini ya mwenyekiti wa CCM Mkapa. Wanafunzi walidanganya wangepatiwa ajira….hii ilimjenga sana Matayo na aliisha kuwa amekuwa maarufu kwenye ofisi za chama Dodoma, kama mjumbe wa NEC na mkutano mkuu..Pia alikuwa ameisha wadanganya akina Mkapa na wanamtandao wengine kuwa ana PhD.
Mwaka 2000 aligombea Ubunge Same Magharibi na kushinda na kuteuliwa kuwa waziri mdogo. Ninamvyomfahamu Matayo ameweza kuapanda chat sana kwa kutumia usanii, 1997-2001 inaonyesha ameweza kusoma MSc 2 na postgraduate diploma moja na kumalizia PhD (Agriculture). Jamani mimi hii ilinisumbua sana nilibahatika onana na Prof Msolla wakati huo alikuwa waziri wa elimu ya juu na sayansi ambaye alitufundisha wote na anamjua vizuri Matayo, nilimuuliza Mh Msolla vipi kuna wabunge wenye vyeti vya kuforge ama kununua, na mnukuu prof Msolla, "Biungeni na kwenye serikali kuna viongozi wengi wenye vyeti vya kugushi, naliisha mwita Dr Matayo kumuuliza PhD alifanya lini na wapi na pia aniletee PhD thesis yake, Matayo aliogopa sana na alikili mbele yangu, kuwa Prof mimi nimetumia hii title kisiasa zaidi, sina MSc wala PhD" mwisho wa kunukuu, Msolla alisema amepeleka kwa raisi wale wote wenye vyeti vya kugushi aliweza taja majina, Dr Nagu, Dr Nchimbi, Dr Kamalla, Dr Matayo na wengine wanavyeti vya kugushi vya sekondari, shahada za kwanza na Msc. Challenge aliyokuwa nayo Mh Msolla ni kusumbili utekelezaji wa raisi maana yeye anasema hawezi mlazimisha raisi kuchukua uamauzi. Raisi alimshukuru sana Msolla akaahidi kulifanyia kazi lakini yuko kimya ….kazi sijui zikoje kule wizara ya kilimo Msolla na Matayo..kazi ipo ninamfahamu sana Matayo yuko tayari kufanya lolote apate madaraka ya kisiasa, na ni fisadi wa muda mrefu. Alikuwa akipokea mishahara miwili ya uwaziri na ile kazi alokuwa akifanya Botswana huyo ndiye Mh Matayo David Msuya Matayo.