Dr. Magufuri serikali imejenga kiwanda cha Dangote

hahahahaha yaaap ila coz watu wengi wanaoshabikia ccm wako nyuma kielimu wamnaamini kweli serikali imekijenga kiwanda cha Dar=ngote
 
duh? Kiki ya kuombea kura. Aliko dangote imekuwa serikali? Watz wasipokuwa makini watalia sana mana huu ni utapeli
 
Ana maana Serikali iliyo madarakani (CCM) wametoa kibali kwa Mwekezaji ambaye amejenga kiwanda hicho cha DANGOTE. Hapo kuna uongo?. Au mwekezaji alijileta tu mwenyewe na kuanza kujenga hicho kiwanda?

Una maana Magufuli hajui tofauti ya neno "kibali" na "imejenga"? Mbona huwa hakose kusemai "...Serikali imetoa kibali kwa wachina wajenge barabara"...?

Inaeleweka kuwa, kama haujazoea unapokutana na umati mkubwa wa watu usivyotarajia na wanakusubiri useme mustakhabari wa maisha yao, unaweza kujikuta umelopoka ujinga. Haya yanatokea kwa wapiga kampeni wote, ndimi zinateleza mara kwa mara. Tuielewe hali hiyo na mwisho wa siku, CHAGUA UKAWA!
 
Serekali ndio inayotoa kibali Ujenzi , mwekezaji haji akaamua anachotaka. Hapo hakusema uongo
 
dah hapa ndege imepiga rivaz angani....igwe dangote kageuka serikali ya tz?kweli ikulu kutamu
 
Serekali ndio inayotoa kibali Ujenzi , mwekezaji haji akaamua anachotaka. Hapo hakusema uongo

unashindwa kuelewa nini serikali imejenga inamaanisha ni cha serikali ila serikali imetoa kibali kwa mwekezaji akajenga hapo kuna maana mbili kuu tofauti
 
Ana maana Serikali iliyo madarakani (CCM) wametoa kibali kwa Mwekezaji ambaye amejenga kiwanda hicho cha DANGOTE. Hapo kuna uongo?. Au mwekezaji alijileta tu mwenyewe na kuanza kujenga hicho kiwanda?

Ni sawa na una nyumba ya kupangisha, unapata mpangaji na anamiliki gari. Wewe unaomba ujumbe wa mtaa kisha katika mambo ya kutafutia kura ni kusema " Nimeleta mpangaji wangu na mumeona anawasaidia kuwapa lifti mkienda hospitalini, naomba kura zenu"
 
Tatizo la mgombea wa ccm ni maneno mengi.
Ukimsikiliza utabaini ulaghai mwingi kama kikwete zamani huku Kutaja ccm ikiwa mwiko kwake.

Kuongea kwake sana kumeonekana ni usanii.
 
Mimi mwenyewe nilisikia, watu wakashangilia. Niliishia kusikitika tu.
 
Sasa mnabisha nini dangoke kajenga tanzania.na tanzania mali ya serikali na government ccm.
 
Hamjui kuwa Dangote kuletwa hapa na kuruhusiwa kuweka kiwanda hapa ni matunda ya juhudi za serikali katika kufungua mianya ya uwekezaji ambayo inatoa ajira kwa wazalendo?
Hicho ndicho alichokimaanisha Rais Maghufuli, tatizo mnajitoa ufahamu kama vile hamuelewi.
 
Ni sawa na una nyumba ya kupangisha, unapata mpangaji na anamiliki gari. Wewe unaomba ujumbe wa mtaa kisha katika mambo ya kutafutia kura ni kusema " Nimeleta mpangaji wangu na mumeona anawasaidia kuwapa lifti mkienda hospitalini, naomba kura zenu"

you nailed it,bro!asante
 
Kwahiyo wewe ni mtafasiri wa magufuli??? Kwa kile abachoongea??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…