Dr.Magufuli Kusulubu Leo Watumishi Matapeli

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Waziri wa ujenzi, Dr John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuwaweka kitimoto baadhi ya watendaji wake walioidhinisha nyumba 59 zilipiwe fidia ili kupisha upanuzi wa barabara mbalimbali za katikati ya jiji la Dar es Salaam wakati nyumba hizo hazipo. Hatua hiyo inakuja baada ya Dr. Magufuli kubaini kuwepo kwa nyumba hewa zilizopendekezwa kuwa zinapaswa kulipiwa fidia. Waziri huyo amesema mhandisi yeyote atakaye kuwa amehusika na malipo hayo hewa atafukuzwa kazi na kufungwa kwakua atakua amevunja sheria. Hii imetulia.
 
Huyu ndie waziri pekee Tanzania anayetenda kazi ikaonekana, pamoja na mengine lakini ufuatiliaji wa Dr. Pombe inatia matumaini, bisha lakini usibishane na ukweli! wengine karaga bao tangu wateuliwe bado wanajifunza mazingira ya ofisi! hata majina ya watumishi wao bado hawayajui Mmoja anamuuliza katibu mkuu wake kila siku "hivi jina ni nani tena nikumbushe"!:A S 20:
 
Mzee Pombe fanya kweli waTZ walishalewa matatizo wasaidie walewe hiyo pombe yako waweze kuamka na kuchapa kazi bila blah blah.Big Up Mr. Yohana Alcohol Padlocks
 
Back
Top Bottom