Dr. Magufuli kumlipa Lowassa Monduli

Dr. Magufuli kumlipa Lowassa Monduli

Alipata samiya suluhu itakuwa magufuli? Amewaacja wamasai hata nguo hawana zakuvaa sasa watachezaje huo mziki?!nenda magufuli monduli
 
VUTA-NKUVUTE

Tunafahamu % 80 ya wakazi wa Monduli ni wamasai; hawa wanautambulisho wao unaofahamika kote duniani. Hao ndio tunatarajia kuwaona.

Aidha, hatutarajii kuona Diamond, Yamoto Band huko. Tukiwaona hao. Tutaelewa fika kuwa hadhira yenu ni ile ile mnayozunguka nayo kwenye malori.

Hiyo hadhira mtakayoipeleka Monduli nadhani itawagharimu mamilioni ya shilingi ukilinganisha na gharama zote mlizowahi kutoa mnapotengeneza hadhira za mikutano yenu ya kampeni.

Pia, tungeshauri muwe mnamjulisha Dr. Magufuli gharama mnazotumia kumtengenezea mafuriko ili naye aongee mambo yanayofanana na gharama hizo.

Halafu mwambieni Dr. Magufuli asirudie kutamka "Ahadi za Kikwete" hizo zinaleta maumivu kwa wananchi. Kule Kigoma kaahidi kuibadilisha Kigoma. Amesahau kwamba J.Kikwete alishaahidi kuifanya Kigoma kuwa Dubai. Ameahidi meli mpya ziwa Tanganyika, Kikwete aliahidi ivo hivyo. Wananchi wanahisi mmewageuza wajinga fulani hivi.
 
Last edited by a moderator:
Katika hali ya kuonesha ubabe wa kisiasa na kukubalika, mgombea wa CHADEMA/UKAWA alipata mapokezi ya kustaajabisha na mkutano mkubwa huko Chato. Chato ni jimbo na nyumbani kwa mgombea wa CCM,Dr. John P. Magufuli. Mapokezi ya Lowassa Chato, kutokana na wanyetishaji wangu, yamemuanika Lowassa kama anayekubalika popote na kumdhalilisha Dr. Magufuli.

Katika hali ya kulipa kisasi cha kisasa na kisiasa, Dr. Magufuli ameapa kwenda kuitikisa Monduli,jimboni na nyumbani kwa Edward Lowassa.Wanatimu wa Dr. Magufuli wameniambia kuwa lengo la kwenda na kuitikisa Monduli ni kuonesha umma wa Tanzania kuwa anakubalika popote, hata umasaini kwa Lowassa. Kisiasa, Dr. Magufuli anapaswa kujibu mapigo kama anavyotamani.

Go Dr. Magufuli and we see a real politics!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Asiende na kundi la wasanii na wala watu wasisombwe kwa malori.Aache watu waende kwa mapenzi yao kama anavyofanya Lowassa.Akifanya hivyo atavuna aibu ya kutosha.
 
Katika hali ya kuonesha ubabe wa kisiasa na kukubalika, mgombea wa CHADEMA/UKAWA alipata mapokezi ya kustaajabisha na mkutano mkubwa huko Chato. Chato ni jimbo na nyumbani kwa mgombea wa CCM,Dr. John P. Magufuli. Mapokezi ya Lowassa Chato, kutokana na wanyetishaji wangu, yamemuanika Lowassa kama anayekubalika popote na kumdhalilisha Dr. Magufuli.

Katika hali ya kulipa kisasi cha kisasa na kisiasa, Dr. Magufuli ameapa kwenda kuitikisa Monduli,jimboni na nyumbani kwa Edward Lowassa.Wanatimu wa Dr. Magufuli wameniambia kuwa lengo la kwenda na kuitikisa Monduli ni kuonesha umma wa Tanzania kuwa anakubalika popote, hata umasaini kwa Lowassa. Kisiasa, Dr. Magufuli anapaswa kujibu mapigo kama anavyotamani.

Go Dr. Magufuli and we see a real politics!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Magufuli amewashangaza wana-chato kwa kuchimba dimbwi la kufuga kambare huku ziwa kubwa likiwa liko karibu. Badala ya kuwapa vijana vifaa vya kisasa vya kuvulia samaki ziwani yeye akachimba dimbwi la kufugia samaki nyumbani kwake ale yeye na familia yake tu.
 
Back
Top Bottom