Dr. Magufuli bila kung'oa hii mizizi utapata shida!

Dr. Magufuli bila kung'oa hii mizizi utapata shida!

Mtoa Mada unamaanisha akina January Out,Mwigulu Out,Naniliu Out, Mwakyembe Out,... Dah,itakuwa Ngumu sidhani kama anayo Jeuri ya kuwapiga Chini akina January et la
Akifanikiwa kuwapiga Chini,Serikali yake itasimama muda si mrefu.
 
Kuna waliokuwepo ni clean mfano Aggrey Mwanri.

Huyu ni mchafu kama wachafu wengine. tofauti yake na wao ni kuwa, yeye alikuwa mzee wa kufunika kombe ili mwana haram apite. akikupa majibu utaamini ni kweli 100% lkn kumbe ni yaleyale.

amekuwa tamisemi kwa muda, lipi amefanya zaidi ya kujibu kwa hisia kali lkn hatua hakuna? mbaya zaidi ana wachaga wake ambao aliwapa ukurugenzi, wamejaa vibur, dharau na kebehi.
 
Kwa system ya chama cha mapinduzi magufuli hawezi kwenda na kasi yake lazima watamsitopisha ngoja tusubili tuone kama ataenda hivi hivi hadi mwisho itakuwa safi na kilio chetu watanzania kitakuwa kimesikika ila kama anabipu itakuwa mbaya tena mbaya na saa hizi ni tofauti na miaaka ya nyuma habari zinaenea haraka hadi huku vijijini zinatufikia bila shida.
 
Kwanza nikupongeze kwa mipango mizuri ya kazi, nakukubali kwa misimamo yako ila CCM siitaki hata kuisikia, Simamia ilani ya CCM maana ndiko ulikoombea nafasi.

Cha msingi ni kwamba unatakiwa kukata na kuing'oa mizizi yote aliyopanda mtangulizi wako, nje na hapo utapiga kelele huku nyuma wanakukuna kisogo na mwishowe utachoka! Hutaweza kufanya nao kazi maana sio type yako, wengine waliwekwa tu.

Nikushauri hata baraza lako la mawaziri weka sura ngeni zote, anza nao kazi upya kuinyoosha nchi, hawa waliopita watakuingiza mkenge, wengi wao walishaanza kujitengenezea mitandao kwa ajili ya kusaka madaraka hapo baadaye, hawa watu ni sumu acha kabisa usionje! Hawa wanaojiita ni watoto wa vigogo ni wanamitandao wakubwa na wanaiabudu mitandao hiyo achana nao nabisa.

Weka timu mpya, ifundishe kupiga kazi, wale wa zamani watajifanya wajuaji watakuharibia kazi maana wana Magodfather yao nyuma wanayaogopa hata kuyatoza kodi. Unao vijana wengi wapya wachapa kazi tafuta wenye uwezo songa nao mbele. Idara zote na taasisi zote za serikali weka sura mpya tupu paa mbele hapa ndipo utafanikiwa kwa haya madudu yote uliyoyaona serikalini yamefanywa na hawa wakongwe hawa.

Hili nalo neno.
 
Wakina marope wameshashindwa hata kuzibiti makampuni ya SIMU afu ndio waliokuwa wanampigania aingie ikulu unazani wataachwa haiwezekani
 
mwache awape japo nusu yao wakiboronga atakuwa keshapata sababuya kuwatimua. akiwatupa mojakwamoja watamsusumia na kazi itamshinda pekeyake
 
Mtoa Mada unamaanisha akina January Out,Mwigulu Out,Naniliu Out, Mwakyembe Out,... Dah,itakuwa Ngumu sidhani kama anayo Jeuri ya kuwapiga Chini akina January et la
Akifanikiwa kuwapiga Chini,Serikali yake itasimama muda si mrefu.
Inawezekana mkuu! Kuwapa hawa nafasi ni kujitaftia matatizo! Wameshaandaa mitandao ya wafuasi wengi.Hawa wote ni wa kupiga chini na kuweka safu mpya atakayoipa training, Hawa walishazoeshwa kupishana angani hawataweza watamuundia zengwe mzee wa watu.
 
mwache awape japo nusu yao wakiboronga atakuwa keshapata sababuya kuwatimua. akiwatupa mojakwamoja watamsusumia na kazi itamshinda pekeyake

Mkuu Tanzania kwa sasa ilipofikia si ya kufanyia majaribio tena, Yaani mtu unapewa unaibu waziri tu unaanza kuutamani ursis, hivi siku ukipewa uwaziri kamili si utampindua aliyeko madarakani? Mimi binafsi sina imani na safu iliyopita hata moja kwa ustawi wa taifa hili hata msemeje.
 
Back
Top Bottom