Dr. Magufuli ameona dimbwi badala ya bahari

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Rais ndiye mbeba maono (vision) ya taifa mkuu ya wapi taifa linatakiwa kuelekea kwa miaka kadhaa ijayo, kuwa na maono hakuzuki ghafla utakapokuwa rais bali maono unakua na kuishi nayo wakati yakisubiri muda mwafaka wa kutokea ufike. Bahati nzuri Dr. Magufuli huenda akawa rais wetu wa 5 kama Mungu akipenda. Swali ni je Dr. Magufuli anajuwa anachokwenda kukifanya kama akiwa rais?, je, anajuwa ukubwa wa kazi hiyo? je, alijiandaa kuifanya kazi hiyo siku moja? Je, alikuwa na maono gani kuhusu taifa hili? na Je, aliwahi kuwaza kama siku moja atahitaji kupigiwa kura na watanzania wote bila kujali vyama, eneo wanakoishi, dini zao wala utajiri wao?

Kazi, matendo, maneno na hulka (attitude) ya Dr. Magufuli kabla ya kuteuliwa kuwa rais ndiyo inayoweza kujibu maswali yote haya. Hebu tuangalie kazi, matendo, maneno na attitude ya Dr. John Pombe Magufuli kwa wananchi kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea urais.

1. Kuchimba dimbwi la kufugia samaki akiwa Waziri wa Uvuvi: Tanzania imezunguukwa na bahari, maziwa na mito mikubwa ambayo imejaa samaki wengi wa aina mbalimbali, pamoja na ukweli huu watanzania hawali samaki wa kutosha kutokana na ughali wake unaosababishwa na uvuvi wa kizamani. Kama Waziri mwenye dhamana ya uvuvi Dr. Magufuli alipaswa kuliongoza taifa katika kutafuta njia za kisasa za kuvua samaki wengi kutoka kwenye bahari, maziwa na mito ambayo imelizuunguka taifa ili watu wengi wale na wapate ajira na taifa lipate faida, badala ya yeye kufikiria kuchimba dimbwi la kufugia samaki la kwake tu na familia yake. Kama alivyofanya Basil Mramba kwenye ununuzi wa rada na ndege ya rais, Magufuli alipaswa kuwaongoza watanzania katika upatikanaji wa meli za kisasa za uvuvi wa maji yenye kina kirefu hata ikibidi kwa watanzania kula nyasi. Angefanya hivyo angeonyesha vision yake kuhusu bahari kwa watanzania. Watu wanafuga samaki kwenye madimbwi kwakuwa hakuna samaki wa kutosha wanaovuliwa nchini hasa baada ya TAFICO kufa sio vinginevyo. Mtu mwenye ndoto ya kuwa rais siku moja hawezi kuacha kuona bahari iliyoanzia Tanga hadi Mtwara, maziwa victoria, Tanganyika, nyasa, rukwa na kufikiria kuchimba dimbwi la kufuga samaki nyumbani kwake, bila shaka angewaza kulishauri taifa kununua boti/meli na nyavu za kisasa hata kama kwa kuvikopa na kuwapa vijana wakavue kwenye kina kirefu samaki aina ya Jodari.

2. Uuzaji wa nyumba za serikali: Magufuli alikuwa dalali mkuu wa kuzipiga mnada nyumba za watumishi wa umma kwa bei ya kutupa, huku akikifahamu kuwa nyumba hizo zilijengwa kutokana na jiografia za sehemu watumishi wanapofanya kazi za umma zilipo. Nyumba zile zilijengwa karibu na maeneo ya watumishi walipotakiwa kufanya kazi. Kama Waziri wa nyumba wakati ule alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kulishauri taifa kuhusu mpango wa kuuza nyumba za umma kwenye maeneo yaliyo karibu na kazini, maana zitahitajika hata kwa watumishi ambao hawajazaliwa. Hivyo hakuonyesha maono yake.

3. Wakazi wa Kigamboni kupiga mbizi: Hivi hakukuwa na lugha nyepesi na rahisi ingine ya kuwaelimisha wakazi wa Kigamboni waliokuwa wakipinga ongezeko la nauli ya kivuko badala ya kuwaambia wapige mbizi?. Hivi alijuwa kama iko siku angerudi Kigamboni kuomba kura? au alikuwa akifikiria kura za watu wa jimboni kwake Chato tu? inaonekana kuwa upeo wake ulikuwa Chato na uwaziri wa ujenzi tu sio urais, asingewajibu vile watu wa kigamboni kama angejua kuna siku angeowaomba pia kura zao.

4. Kejeli kwa vyama vya upinzani: Dr. Magufuli aliwaona watanzania walioko vyama vya upinzani kama watanzania walioko daraja la pili kwa kuwakejeli kila alipopata nafasi ya kufanya hivyo. Hakujua kuwa iko siku atakuwa rais wa wote.

5. Wizara ya Ujenzi: Dr. Magufuli alionekana kuipenda sana na kuonyesha uwezo mkubwa kwenye Wizara moja tu ya ujenzi, pamoja na kuwa yeye sio mhandisi. Sijui alikuwa akivutiwa na nini kwenye wizara ile. Hakujua kuwa kuwa iko siku atakuwa baba wa wizara zote nchini.

6. Ushirikiano na Wizara nyingine: Dr. Magufuli alionekana kufanya maamuzi ya peke yake bila kuhusisha Wizara nyinge kama vile nishati, uchukuzi, mambo ya nje, n.k. Hii ilionyeshwa pale alipotaka kulibomoa jengo la makao makuu ya tanesco Ubungo, alipoyazuia malori kupita barabarani na alipokamata meli ya wachina ya uvuvi ambayo hatima yake haijulikani hadi leo bila kuwashirikisha wadau wengine. Hakujua kuwa siku moja angehitaji mawazo ya watu wengine katika kufanikisha kazi zake kama kiongozi mkuu wa nchi.

7. Bomoa bomoa zake: Kwake yeye kilichoandikwa kimeandikwa, hana haja tena ya kufikiria utu, hasara na mateso watakayopata waathirika wa vitendo vyake. Yaani kwake yeye mtoto aliyechelewa kurudi nyumbani adhabu yake ni kufungiwa, kula na kulala hukohuko nje hadi asubuhi. Anambomolea mtu huku anacheka bila kujali maumivu ya wanaobomolewa nyumba zao huku akifahamu wazi kuwa serikali yake inahusika na ujenzi holela wa bila kuzingatia mipango miji.

Huyu ndiye mtu ambaye leo anaomba kazi ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi itakayompa uwezo wa kuwa Amiri jeshi mkuu, kuteua mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, majeshi, majaji, wakurugenzi, makatibu wakuu, wenyeviti wa board.

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom