Huyu mzee Ndiye Dr.LwaitamaHivi huyo Mzee ni nani?
kula kuku na vifaranga kwahiyari zao hiyo sio skendo bali ni umahili wa kushawishi.Hivi alisha kanusha ile kashfa ya kula kuku na vifaranga wake
State agent
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huyo Mzee ni nani?
Hajawatetea Chadema, hajakuambia ni mwanachama, altumia jukwaa la Chadema kuzungumza kwa sababu jukwaa la CCM haliruhusu hoja mbadala zaidi ya kuunga mkono na pongezi kwa mwenyekiti.Bora angejikita tu kuwa independent speaker kuliko kujitia kwenye siasa; matendo ya viongozi wa CDM yatamuumbua tu.
Pamoja na mashiko ya hoja aliwaona hao watu anaowatetea kuwa wanasimamia kuwa huru jinsi walivyokuwa wanagombania kumshika mkono huyo mtu anaemwita mtawala.
Nyie mna Dr shika kafanyia nini nchi?
kula kuku na vifaranga kwahiyari zao hiyo sio skendo bali ni umahili wa kushawishi.
The only logical explanation ujaiangalia video au umeangalia nusu. Vinginevyo humo ndani kaonyesha kadi yake ya CDM na katuambia tarehe aliyojiunga na sababu ambazo kama vile ni personal against Magu.Hajawatetea Chadema, hajakuambia ni mwanachama, altumia jukwaa la Chadema kuzungumza kwa sababu jukwaa la CCM haliruhusu hoja mbadala zaidi ya kuunga mkono na pongezi kwa mwenyekiti.
Hoja hii mwal. J K Nyerere aliwahi kusema enzi zake huu ya maendeleo ya watu na vitu viende sawia na uongozi bora.
December 11, 2019
Dar-Es-Salaam, Tanzania
Mada : Sera pacha ya Maendeleo ya Watu na Maendeleo ya Vitu
Dr. Azaveli Lwaitama akizungumza na wazee wa CHADEMA ameainisha jinsi sera pacha ya Demokrasia na Maendeleo inavyoshika kasi ushawishi miongoni mwa watu-huru.
Sera hii pacha ina kwenda sawasawa na maono ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( CHADEMA) ambayo tangu kuasisiwa kwake mwaka 1992 imesisitiza maendeleo ya vitu yaendane na maendeleo shirikishi ya watu kupitia demokrasia.
Ambapo wananchi mmoja mmoja na kama vikundi hukubaliana kupitia ushawishi wa kidemokrasia maendeleo pacha ya vitu na maendeleo ya watu yanapatikana sawia.
Source: DARMPYA TV
Sera hii ya maendeleo na demokrasia ni tofauti na mtizamo wa chama kongwe ambacho awamu hii ya 5 imeamua kutosa mwananchi yaani watu wasipate maendeleo na wala hawatakiwi kuhoji vipi mnatuacha na kushikilia maendeleo ya vitu.
Chama kongwe CCM sasa kinaamini katika kuminya demokrasia, mawazo huru na ushirikishwaji watu ktk maamuzi ya mustakabali wa maisha yao.
Hapa ndipo penye tofauti kubwa kuelekea 2020 ambapo CHADEMA ina ushawishi mkubwa wa watu huru kupitia demokrasia kujiamulia maendeleo ya vitu sambamba na maendeleo ya watu.
Huku CCM wao wameamua kuwapa kikundi kidogo kusingizia maendeleo ya vitu yataletwa kwa kuwanyima watu uhuru wao wa kidemokrasia huku wakiwanyima maendeleo ya watu kitu kinachopelekea umasikini na ugumu wa maisha kushika kasi nchini Tanzania.
Mzee namkubali sana huyu, leo amepigilia misumari ya moto ndani ya vichwa vya "WANA LUMUMBA", ana mtazamo chanya juu ya uongozi na utawala bora katika taifa letu haijawahi kutokea.
Huku kwetu "BIMA YA AFYA" ni bora kuliko "NDEGE" (In Roma's Voice).
Alipigwa marufulu kupanda ndege ya precission air huyo .Alishushwa kwenye ndege na polisi na kupigwa ban .Mtanzania wa kwanza toka Tanzania iwepo kushusha kwenye ndege na kupigwa ban kw ukorofi ndani ya ndegeHuyu mzee Ndiye Dr.Lwaitama
Kakwambia alikuwa TANU, pia ni mwanazuoni (retired senior lecturer (PhD), UDSM), sasa usichoelewa ni nini?