Dr.kitima aiponda serikali kuhusu bajeti 2013/2014

bajeti hii ni nzuri sana na imekuwa mwiba kwa machadema ndo maana mnaweweseka

Mwiba kwa wana CHADEMA au waTanganyika? Achana na AKILI ZA KUSHIKIWA! Mlizoea COPY and PASTE kutoka CHADEMA. Wameshagundua udhaifu wenu. Mwaka huu wamekula MINGO, hawajatoa budget yenye figure kiasi kwamba mtabaki na madudu yenu ya kuwatesa waTanganyika.

Mlizoea wakisha fikisha budget yao ofisi za bunge ndio mnaanza kukokotoa na kufanyia marekebisho budget zenu. Mwaka huu imekula kwenu.

Si umemsikia Chenge akiwaambieni kwamba "HATA HIZO PESA ZENYEWE HAZIPO NA WALA HAZIJULIKANI ZITAPATIKANA JE". Huo uzuri wa budget unatoka wapi?
 
mkuu, kwanza uelewe kuwa kwa sasa hatuna nchi inaitwa tanganyika. hiyo inaonyesha ni kwa kiwango gani umemezeshwa tu maneno. pole sana

Wewe wasema!

Sie tunajua Tanganyika ipo. Wewe baki na hiyo nchi unayo ijua!!!!
 
Kiongozi!

Kama mfumo ndio uko hivyo, waTanganyika tupo kwenye Jehanamu ya duniani. Hadi 2015 ifike tutakuwa tumesha unguzwa vya kutosha.

Maana kama waziri msomi wa kiasi hiki anaweza kusifia budget ambayo hata kabla hajaimaliza kuisoma, unaona jinsi inavyo mnyonga mTanganyika.

Lakini kwa ushabiki wa Kichama wa Wabunge wa CCM wanaipikia makofi kana kwamba neema imeshushwa Tanganyika.

Anyway, kwa vile budget hiyo imewaongezea zaidi maeneo ya kutumbua, ndio maana hawawajali waTanganyika.

Watawajali vip ndugu yangu wakati wao wameshiba? Kumbuka tu Mgimwa alivyokuwa akiwasilisha bajeti,alisema ushuru wa pikipiki na bajaji ni 0% huku akicheka cheka lakin wakati huo ameongeza kodi ya petroli ambapo bodaboda na bajaji nying zinatumia mafuta haya,we unadhan kuna unafuu hapo! Tupo kwenye jehenamu la balaa na utawasikia vijana wa Lumumba jins wanavyotoka povu kuishabikia,njaa mbaya sana ndugu na hii ndo Tanganyika!
 
kitima ni mnafiki na fedhuli mkubwa. yeye kazi yake ni kuangalia mabaya tu ya ccm bila ya kuyasemea yale mazuri. chadema wamemteka sana. anapita mule mule alimopita mbowe juzi. usomi wake na taaluma yake ameiweka pembeni na sasa amebaki ushabiki wa kisiasa tu.

Tatizo lenu ndo hilo mtu akiwaambia ukweli mnaanza kung'aka ooh mara anatumiwa,mnafiki,amefilisika kifikra.....badala kuufanyia kaz ushauri nyie mnautupa ndo maana nchi inaangamia,tena nyie vijana wa buku 7 ni majanga zaid kuliko hata wanaowalipa akina Nape!
 
toka lini makamu mkuu wa chuo cha kikatoliki akaisemea mazuri serikali ya ccm. kitima anatumika kama condom

Lizabon toa hoja ukatoliki umefuata nini hapa,acha kuweka akili yako kubwa mfukoni na kuruhusu hiyo ndogo kutumika Kitima ni mtu huru,katoliki ni taasisi so wat.
 
Huyu Dr Kitima balaa.Si muoga hata chembe anasema live iliyokweli hadi watangazaji wanajaa uoga!
 
Hongera sana Dr Kitima unatufungua na unatusaidia kujua mengi, kwani wasomi wengi wamekua wanafki na hujipendekeza kwa serikali ili wapate vyeo wakati inchi yetu inanyonywa na mafisadi. Tunatambua mchango wako endelea Mungu yupo nawe.
 
Serikali inapoongeza bei ya mafuta inaongeza mfumuko wa bei, inaongeza gharama za usafiri na usafirishaji, inaongeza bei za bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta yenyewe, inaongeza bei za vyakula, inapunguza bei za mazao mashambani, inaongeza ugumu wa maisha, inaongeza........................................................................................................................ iinaongeza ugumu wa maisha na kupunguza kasi ya maendeleo.
 
Lizabon, kama wewe umepitia maisha ambayo mtanzania wa kawaida na mwenye uchungu na nchi yake bora ungejinyamazia kuliko kupandisha watu hasira. Achana na mapenzi ya chama jikite kwenye mapenzi kwa nchi yako.....bajaeti unayoishadadia inakusaidia nini zaidi ya kuongeza matatizo kwa wananchi? Inamsaidia nini mkulima wa kijijini! Inamsaidia nini mfanyakazi wa Tanzania!? Natamani kukutukana najizuia kwa sababu sikulelewa hivyo! Unapoongeza bei ya mafuta unategemea nini! Asilimia iliyoshushwa kwenye PAYE ni ngapi mpaka ilete unafuu wa maisha...Stu**d! Kitima kaongea kama mtanzania na wala hajaongea kama CDM, mambo ya CDM na CCM wasubiri kina Mbowe na Kikwete au watumie wasemaji wao. Usijaribu kabisa kuhusisha Dr Kitima na huo ujinga wako. Dr kasema ukweli wewe unaleta mapenzi hapa jamvini! Usitetee upuuzi,bajeti hii ni janga na haina usaidizi wowote kwa mwananchi labda nyie mnaopata mianya ya ufisadi ndo mnaneemeka. Nchi gani inaendeshwa kwa kodi za wafanyakazi pekee! Tanzania ni mfanyakazi pekee ndo hakwepi kodi na ndie anaelipa kodi kamili,wafanyabiashara na wawekezaji ndo hata robo ya kodi watakiwazo kuzilipa hawalipi halafu unakuja hapa na mambo yako ya kipuuzi kushadadia upuuzi.Acha wenye akili wachambue ukae pembeni usituongezee hasira hapa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom