Dr. Kigwangallah ukifanya haya ntakupigia salute

makaptula

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
200
66
Kwanza kabisa kuhakikisha hospitali zote za serikali Tanzania bara na visiwani zinakuwa na vitanda vya kutosha kulaza wagonjwa.

Pili kuhakikisha madawa yanapatikana mahospitalini kwa wakati.

Tatu uishawishi serikali kuagiza ambulance na kila hospital iwe na ambulance moja au zaidi kulingana na ukubwa wake.

Nne kuakikisha vifaa vya vipimo kama Cit Scan, MRI, na machine za vipomo vingine muhimu zinapatikana na zinasambazwa kwenye hospital zote za serikali Tanzania.

Vile vile kuboresha Huduma mbalimbali za afya na kukomesha ile tabia ya wakuu Wa kaya kwenda kutibiwa nje ya nchi angali tuna madactari wwazuri ndani ya Tz.

Kwa kuanzia na hayo kwa mtazamo wangu utakuwa umewasaidia watanzania wengi wanaoteseka na Huduma mbovu za hospital za serikali.
 
Acha kukariri..! Vyote ulivyo visema vinategemeana na uchumi..! Sasa fanya kazi uchumi uinuke kwanza ndo hayo maajabu yaje! Otherwise utakuwa ndo walewale wanaofikiri mambo yanatokea kimiujiza ujiza. KAZI KWANZA....
 
mbona huyu naibu waziri mnamzungumza sana, kuliko waziri ,mtu mwenyewe hana uzoefu na mambo ya mahospitalini
 
Health care delivery ni system sio mtu... hayawezi kutokea hayo endapo kila mhusika hatatimiza wajibu wake... PS wa wizara ndio kinara wa shughuli za utendaji

Jaribu kupitia google mara chachechache ujue mfumo wa utendaji serikalini unafanyaje kazi... naibu waziri hawezi kuongeza bajeti ya manunuzi ya dawa bila kuwa na fungu lililopitishwa ndni ya bajeti
 
Dah!We jamaa mbona unamtwisha zigo zito Braza Kigwangwala bhana?! Unaacha kumwambia afanye ziara ya kushtukiza kwa Dr. Buberwa lakini we unamwambia ahakikishe hospitali zote zinakuwa na vitanda bwana na ambulance kwa kwenda mbele?! That's not fair at all; we jamaa una chuki na mbunge daktari wetu!!

Braza Kigwangala... kama utapita kwenye huu uzi achana na huyo jamaa!! Kinacho-trend Instagram hivi sasa ni Wema Sepetu kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi ambayo long time alidanganya kwamba aliinunua kwa 280M. Sasa mfanyie ziara ya kushitukiza manake huu uhamaji wa hovyo hovyo na usioratibiwa sometimes unaweza ukawa unasambaza magonjwa toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine!
 
Usisahau kuwaondoa AMOs na dental officers ambao wanakaimu u- DMO

Hahahahah... Acha kubana ridhiki za AMO, acha wajistaafie kistaarabu.. Nyie MD sio lazima muwe ma-DMO, huo Ni wadhifa tu ila wewe ujuzi wako utabaki kuwa juu zaidi ya AMO.
 
Acha kukariri..! Vyote ulivyo visema vinategemeana na uchumi..! Sasa fanya kazi uchumi uinuke kwanza ndo hayo maajabu yaje! Otherwise utakuwa ndo walewale wanaofikiri mambo yanatokea kimiujiza ujiza. KAZI KWANZA....

Maajabu gani sasa?wewe itakua ndio wale majibu..kuna nchi yenye uchumi kama huu then haina vitu ambavyo mtoa mada kavileta?wewe ndio umekariri ujinga.
 
Hahahahah... Acha kubana ridhiki za AMO, acha wajistaafie kistaarabu.. Nyie MD sio lazima muwe ma-DMO, huo Ni wadhifa tu ila wewe ujuzi wako utabaki kuwa juu zaidi ya AMO.

Hawana lolote, wanavurunda kazi tu kila kukicha, huku hawana mawazo mbadala ya kuendesha huduma za afya
 
Hawana lolote, wanavurunda kazi tu kila kukicha, huku hawana mawazo mbadala ya kuendesha huduma za afya
Tatizo moja la nyie ma MD Ni kujiona wa kipekee sanaa, ila kiukweli hao ma-AMO na CO Ndo wametuleta hapa tulipo (Tuwashukuru sana).

MD ambaye Ni less than 5years kazini Ni bado sana kujiweka level za AMO au CO ambaye kakaa kazini More than 15 years, hatuzungumzii elimu ya makaratasi, Bali ujuzi Wa Hosp kule.. Dx, na Mx..

Hao ma-AMO ndio wamekua wapasuaji pale mama zenu wanaposhindwa kujifungua kwa njia ya kawaida huko peripheral areas, nyie MD mkipelekwa huko mnakimbia, Mara hakuna maji, Mara umeme... Lakini AMO anafanya caesarian section kwa karabai na kuokoa maisha.

Rudi kasome mwaka m1 Wa management afu ndo udai u-DMO
 
Back
Top Bottom