Dr. Kashilila ni kimbunga

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,496
Reaction score
17,635
Dr. Kashilila ni miongoni mwa watanzania wachache waliopata bahati ya kusoma hadi PhD. Taifa linabidi lijivunie kuwa nao watu wenye kiwango hiki cha elimu kwa sababu wao wanapaswa kuwa fimbo ya kuwaongozea wale wasioona ambao ni ndiyo wengi katika taifa la kimaskini kama letu. Watu wenye PhD ndio wanaopaswa kuongoza vita ya kuelekea full democracy, kupinga dhuluma, ujinga, uonevu, udini, na ukabila ndani ya jamii. Mtu mwenye kiwango hili cha elimu amefundishwa kusema na kutotenda mambo bila ya kuwa na takwimu sahihi (evidence). Mtu wa ngazi hii ana elimu ya what are variables (dependents and independents), mtu wa ngazi hii anajua namna dependent na independent variables zinavyohusiana. Anajua vema uhusiano kati ya dependent na independent variables unaweza kuwa ama causal-effect (causality) au association tu. Hivyo anajua kuwa ili uweze kusema kitu (variable) hiki (A) ndicho kinachosababisha (sufficient cause) jambo lile (B) litokee lazima kuwe na vigezo 9 ambavyo ni strength, consistency, specificity, temporality, biologic gradient, plausibility, coherence, experimental evidence na analogy (vigezo hivi vipo kwenye vitabu vyote vya applied epidemiology). Pia, Ili mtu aweze kusema kuwa kitu (A) kina uhusiano (association) na jambo (B) kutokea pia lazima uwe na hypothesis ambayo unaweza kuipima (significance testing) ili ujue kiwango halisi cha uhusiano kati ya vitu hivyo viwili kutokea pamoja kila wakati vinapokutana (p-value). Mtu mwenye PhD pia anajua kuwa ziko confounders na coincidence katika jambo kutokea ambavyo lazima mtafiti avi address kabla hajasema ama kuamua kutenda jambo.

Baada ya kuwakumbusha wasomi kile walichojifunza kwa kodi za wananchi, sasa ngoja nirudi kwenye hoja ya msingi. Ni hivi karibuni Katibu wa bunge Dr. T. Kashilila amesema kuwa utovu wa nidhamu wa baadhi ya wahemimiwa wabunge (wapinzani) unasababishwa na bunge kurushwa hewani live!! Hivyo wanatafuta umaarufu kwa wananchi. Hivyo dawa yake ni kusimamisha urushaji wa vipindi vya bunge live. Mimi siamini mtu mwenye sifa kama ya Kashilila anaweza kusema na kuamua hivyo, labda kweli amenukuliwa vibaya kama anavyosema yeye mwenyewe. Kashilila kama msomi alipaswa kufanya utafiti japo mdogo wa kina ili agundue vyanzo halisi vya kelele za wabunge bungeni ili agundue kama tatizo hasa ni luninga, kanuni za bunge, matumizi ya kanuni, utovu wa nidhamu wa waheshimiwa wabunge wa upinzani, ugeni wa wabunge bungeni, kukua kwa democrasia ama hali mbaya za maisha na huduma za jamii kwa watanzania?. Kusema moja kwa moja kama tatizo ni luninga sio sawa kitaaluma, na maamuzi ya namna hii hayawakilishi watu wenye taaluma kote duniani, maana hayana harufu ya usomi wowote ila ushabiki. Watanzania walishapata mazoea sasa ya kulifuatilia bunge lao, wanatenga muda wao japo sio kila siku kufuatilia bunge lao likijadili hatima yao. Wako watu wamenunua na kuweka luninga ofisini mwao na wengine viredio vidogo kwa kazi hiyo. Hata wagonjwa wanaposubiri zamu zao za kutibiwa huwa wanapenda kusubiri wakiangalia kipindi cha bunge. Jamani wasomi tumieni elimu zenu kusaidia mambo ya wananchi sio matumbo yenu yaende mbele
 
Dr (Magumashi) KASHILILA ni JANGA LA KITAIFA sio kimbunga! amedhalilisha elimu kwa ujumla na hasa shahada ya uzamivu ya Phd.
 
Au Udr wake ni ule heshima maana mimi nafanya PhD ila sipendi na sitaamini kuna njaa mbaya mithili hii ya huyu mbumbumbu kashilillah naamini hata mke wake anampenda kwasababu ni buzi lake la kudumu ila sio kwasababu ni mtu makini...Kuna haja ya huyu jamaa kupigwa msasa na walimu wa shule ya msingi iliopo jirani maana anafikiria kwa kutumia nyayo za miguu na sio masaburi....Eti nayeye huyu ni Dr. Manyang;au wanajiita madr.Shame on you kashillilah huna hadhi ya udr.labda kama ni Dr njaa
 
Hii sio hypothesis, bali ni fact: mtu akiishaamua kuitumikia CCM, akili, PhD, u-profesa, nk vyote vinafungiwa kwenye kabati. Kwa CCM ni vigumu kutofautisha akili na busara za, kwa mfano, Profesa Maghembe na Nd. Lusinde - kwa kutumia mfano mmoja. Kama unabisha, tutajie Profesa au Dr ye yote anayeitumikia CCM ambaye amejitokeza hadharani (eg katika mijadala ya Bunge) kutetea maslahi ya walalahoi kama vile kulaani ufisadi au uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola.
 
PhD holder halafu unakuwa Clerk (karani)?.........:rockon::rockon:

Unamuonea bure clerk wa bunge sio karani mkuu, ni mfumo wa kuiga kila kitu kwenye mabunge ya jumuia ya madola hivyo vyeo wamevitoa huko, huyu ndio sawa na katibu mkuu tu wa wizara
 
PhD ningeziona za maana kama wangegundua hata iphone!

iphone? Ha ha ha ha! Mkuu mbona unazungumzia "rocket science" kwa wasomi wetu. Watugundulie just "tooth picks" tuachane na ujinga wa kuziagiza kutoka China na mapori yote tuliyo nayo.
 

dr harrison mwakyembe ndie pekee ndani ya sisiem anayetumia taaluma yake kwa ajili ya masikini wa nchi hii,naomba umpe heshima yake mkuu japo yupo choo cha kike..
 
Dr (Magumashi) KASHILILA ni
JANGA LA KITAIFA sio kimbunga! amedhalilisha elimu kwa ujumla na hasa
shahada ya uzamivu ya Phd.

Unaweza kuta PhD yake ina fanania na kama zile degree za chupi...
 

Wewe umenena!... Hata Mwakyembe hajatusaidia kuwaweka mikononi watuhumiwa wa RICHMOND kwa kuficha ushahidi!... Waliotaka kumuua kwa kumuwekea sumu anawalinda.
 
Dr (Magumashi) KASHILILA ni JANGA LA KITAIFA sio kimbunga! amedhalilisha elimu kwa ujumla na hasa shahada ya uzamivu ya Phd.

Naona mtoa mada hajui maana ya KIMBUNGA
 
ni kashilila gani unaemweleza hapa! ni huyu wa ana makinda? au yule tafuta nyoka nyoka wa lutasyobya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…