Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Tujisahihishe Tz

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
3,050
Reaction score
1,359
HUKUMU ya IGUNGA Leo..Kashinje Vs Kafumu,

....Kwakweli mpaka sasa hivi Mbunge wa CCM ameshindwa kumleta shahidi ambaye angetoa taswira njema kwa Ushindi wa Kafumu.

Kwani Bwana Magufuli, ambaye yeye ametajwa kwenye Kesi mara kadhaa; kwamba alikuwa akitoa Ahadi ambazo alikuwa akitoa mbele ya Jukwaa.. kwa hali hiyo Mgombea Wa Chadema anasema alikuwa anatoa Kama Nani? Waziri au mpiga Debe wa CCM?

Kwakweli Kesi imekaa patamu sana...kama Haki ikitendeka ...Basi Jimbo tutalajie kuwa Wazi katika Hukumu ya Leo..!!!

=======
UPDATES
=======
Mrithi wa Ubunge wa Igunga mh. Dalali Kafumu leo itajulikana ama kusuka au kunyoa. Mpingaji mkuu wa kesi hiyo ni aliyekuwa mgombea wa CDM na kawaailiaha hoja 15 za kupinga ushindi huo

Magari ya polisi, gari la maji washa, naona ndo yanawasili hapa mahakamani, ila bado hatujaingia ndani ya ukumbi wa mahakama, pia watu bado si wengi sana.
Leo ni leo. Ushindi wa Kashindye kupigwa tena mnada na Dalali? Watu wameshajaa Mahakamani tangu saa 12 asubuhi. Hukumu kuanza kusomwa saa 3 hii. Ni CHADEMA na CCM...

- Mahakama imemvua ubunge Dr. Kafumu!

Baada ya hukumu kutolewa Igunga wananchi wa Igunga wameripuka kwa furaha na nderemo na kuzunguka katika viunga vya mji huu huku wakiimba nyimbo za kuipongeza CDM na kumpongeza Magufuri kwa kusaidia ushindi huu.

attachment.php

attachment.php

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga amefunguka na kusema kuwa hakuwa na imani na jaji kwa kuwa aliegemea upande wa CHADEMA na matokeo yake ameipa CHADEMA ushindi.

Dk. Kafumu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa yeye siyo mbunge tena na ataendelea na kazi yake ya utafiti wa madini.

Source: EATV
 
Siku ya kusikiliza si ya kutoa uamuzi. hawezi kuvuliwa siku ya kusikilizwa kesi.
 
kesi ndo inaanza au imeshasikilizwa na leo ni hukum? dazu fafanua vizuri
 
Watamlinda tu,maana hakuchaguliwa na wananchi chama ndicho kilicho mchagua.
 
CDM tuandae millions kadhaa, kulipa fidia. Nyie hamuifaham ccm imeamua kama noma na iwe noma, baada ya kushutikia huu upepo haupiti.
 
tumeshaambiwa na pinda kuwa hao watumishi wa umma wanatekeleza sera za ccm, ikiwa ni kuhakikiisha pia kuwa ccm inaendelea kutawala! Tegemea danadana tu hapo
 
All da best CHADEMA, JAPO ANGEKUWEPO MTU MAKINI TABORA MAHAKAMANI AKITUPA UPDATES, KWANI CCM ILIFANYA RAFU NYINGI KT UCHAGUZI HUO. USHINDI KWA KASHINDYE NI USHIND KWA MAGEUZI
 
Hope upo ndani ya mahakama ukifuatilia kiundani hukumu hyo!Tunaomba utupe updates kwa umakini kabisa.
 
Hukumu haijavuja kweli kama upo eneo la tukio tujuze tafadhali ili kashindye ajiandae
 
Mkuu nipo hapa juu NSSF, ngoja niweke vizuri progressive report yangu, nakuja hapo fasta
 
Gambas, asante sana. Nadhani wengine wanatakiwa kujifunza kwa huyu bwana maana heading yake inaendana na anachoandika. KUna wenginewanaudhi sana, wanawekaheading kama hii halafu kwenyetext anaulizia nani ana habari zaidi. Mwaga mambo mzee Gambas
 
Last edited by a moderator:
umesema ukweli ccm ndiyo mshindi taka usitake liwalo na liwe
 
kama polisi n wengi mahakamani basi gamba limepewa ushindi na mahakama ya ccm
 
Back
Top Bottom