Dr. Kaborou aiacha CHADEMA, Ajiunga CCM

kizazi cha kina Kaborou,Hiza na Kasaka ni kizazi chakavu hakina uwezo tena wa kuleta mabadiliko.Wamefikia ukomo wao wa kufikiri na kubuni.

Kizazi kipya kinapaswa kutafsiri mauzauza haya kama filimbi ya kuwaita waingia ulingoni.Maana sasa badala ya kujadili hoja tutakuwa tunajadili fulani katoka CHADEMA kaenda CCM,siasa zinachukua sura za watu badala ya hoja.Tunataka ushindani wa hoja ambazo hatimae zitaleta maendeleo badala ya kujadili watu!

Nimesikia jana kwenye vyombo vya Habari,anadai eti CCM ina sera nzuri,sasa hakuzisikia hizi sera wakati wa kampeni?

Makamba nae anachekelea galasa! Hakika wamejichokea! Tunataka siasa zitakazo sababisha mruko,siasa zitakazo chochea maendeleo sio hizi za kizamani!

Cha kuchekesha ni namna Habari ilivyoripotiwa kwenye gazeti la Mtanzania la Tarehe 20 septemba! Wanasema moja ya sababu ya kujitoa ni kwa kuwa Freeman ameonyesha upendeleo kwa wanasiasa vijana na wasomi! Hainingii akilini kuchukuziwa na jambo chanya kama hili! Chama chochote makini kinahitaji vijana wasomi!

Hu ni wakati wa kizazi kipya kuchukua nafasi yake!

the situation hasnt changed much...

just the blue corner members, it was kaburu, now zitto
 
Ni Hatari kuwa na fikra kwamba CCM itatawala milele! Na kama hali itaendelea kuwa kama ilivyo sasa na maendeleo yakiwa duni Tanzania italekea pabaya!

Watu watakata tamaa na vyama vya upinzani,baada ya hapo watakata tamaa na siasa! Matokeo yake watatafuta mfumo mbadala wa kuleta mabadiliko nchini,ole wake Tanzania.

Nashangalia kila ninaposikia vijana wanajiunga na vyama vya upinzani kwa maana ina maanisha bado watu wanaamini mabadiliko yatapatikana kupitia mfumo wa siasa.

Pamoja na uwizi wa CCM kwenye uchaguzi,bado CCM inacheza ligi ya peke yake! Ndio yenye rasilimali ambayo matokeo yake huvutia wataalaam,matajiri na wanafiki wengi!

Kwani mapambano ya kisiasa yako maeneo gani? Si ni Rasilimali,sera na watu.Kwa kuwa kuna tofauti kubwa katika eneo la rasilimali CCM inakuwa imekamata eneo moja la mapambano,kisha inakamata watu maeneo haya mawili yanafunika sera! Siasa za Tanzania hazina sura ya sera,watu hawapigi kura kulingana na sera na sehemu kubwa ya kampeni watu hawazungumzii sera! Kama tungekuwa tunachagua kwa sera CCM isingeshinda mwaka jana.

Kampeni za Kikwete hazikuwa na sera! Aliaahidi mambo kulingana na mahitaji ya eneo na sio kulingana na ilani ya uchaguzi.Mwenyewe alidai kuna ahadi za ilani na ahadi za papo kwa hapo! Haya ni masihara,kwa sababu ilani inapoandaliw,vyama huangalia rasilimali zilizopo na zitakazo patikana na kisha kuanisha vipaumbele! Ahadi za papo kwa hapo zina ulikini mkubwa! Kisha alithibitisha kuwa ilani yao ni kiini macho,alipokuwa anamponda Mbowe kwa Kuruka na chopper,walidai wanaenda kwa usafiri wa barabara ili watambue matatizo ya wananchi,sasa unawezaje kuwa na ilani kama hufahamu matatizo ya wananchi?

Tatizo la siasa za Tanazania sio kwa upinzani pekee! Tuna wanaisasa makini wachache mno,iwe ndani au nje ya CCM!

Ni lazima kuwe na wimbi kubwa la watu na rasilimali kuelekea upinzani na hatimae tuanze ushindani wa sera.Na huu ndio utakuwa mwanzo wa utungu!
once again... we are living the past

kila kitu ni vilevile, labda kidooogo kwamba ile ya kuema ccm wako kwenye their own league imeanza kufifia
 
Hii inamaana huko chama tawala hapakuwa na watu vichwa kama Kabouru! Ndo maana wakamghilibu ili akagombee Ubunge EAC! Hapa naona CCM wamejidhalilisha kwamba woote wabunge karibu 260 ni makaputi.....hadi wampate mpinzani awaokoe....!

.............................
:U Can't Change The Nature:

Ukitafakari sana maneno ya dr. Slaa utaona kwamba huyu walishamshtukia na yeye baada ya kuona ameshafahamika akaomba aruhusiwe kurejea sokoni kuendeleza biashara. Ndiyo akaambiwa basi rudi tutapeleka mwingine au waliobaki wanatosha. Na huyo ambaye pia wanaonekana kumshtukia ngoja kidogo tu anaye atarudi na kwa maana hiyo kwa wananchi itaonekana kana kwamba Chadema ndiyo inasambaratika. Ujinga ni kitu kibaya sana.
 
kuhusu zito no coments,ila huyo kaburu alifika kigoma akitokea marekani akiwa kachakaa,kajawa na mandevu kama karl max,akaingia kwa staili ya kuvaa saspenda na porojo nyingi,hakua na pesa hata za usafiri marehem mzee shaka akajitolea tax yake aina pugeot no7.na kumzunguza kwenye kampeni bure akina rama mtale walitoa malori yalioitwa see neva dry kuwa yanawabeba watu mji mzima kwenye kampeni zake bure, lakini cha ajabu alipopata ubunge ndio kwanza akamchukua dem wa fried wa bima aitwae aziza ambae inasemekana anangoma kwani fried alikua ana madem wawili kalekwa ambae alikufa positive kabisa then na huyo aziza ambae ndie mke wa kaburu hadi sasa. Sina imani sana na wagombea toka kigoma huyo kaburu aliefadhiliwa na kupewa jina na chadema alihama na kwenda ccm, je ndio huyo zito atashindwa?watu wengi wa kigoma wana asili ya unafiki,usaliti na kutokua na uzelendo wa kweli ndio maana hata maendeleo yanafika taratibu sana. Chadema ni chama makini naamini kina mizizi imara na hakitayumba kwa kutokuwepo kwa zito zuberi kabwe.nawasilisha.
 
Ebu kua kidogo
1. Kwanza ukampime huyo mtu ili ujue kuwa anangoma
2.Usigeneralise mambo kwani wao wa kigoma wakisema hwana imani na wachaga patakalika Tanzania
3. Haya ni maisha yao , uhuru wao, na wana uwezo wa kuamua lolote ilimradi tu wasikuathiri wewe
 
Mkubwa Waberoya,
Sidhani kama unamtendea haki huyo Dogo! Amejitahidi kutoa mawazo yake na uchambuzi wake kuhusu kuhama kwa Kabouru akilinganisha na kile unachokipigia upatu (Zitto Kujiondoa CHADEMA). Kama una cha kuchangia katika hoja hii ulitakiwa ukiseme na usiingize suala la uchaga na kwenda kupima wenye ngoma! Sitashangaa ndugu zako MS, Daressalam, Mtu wapwani nao wakirukia hili na kuingiza udini!

Naamini kuwa CHADEMA ni chama sasa kilichokomaa na ambacho hakitafanya makosa ktk suala la Mbunge wake Zitto, pia ninaamini Zitto kabwe pamoja na udogo wake kiumri hatafanya makosa ya kitoto kama aliyofanya Kaburu. (Yuko wapi sasa huyo Kaburu? si walimtumia kama kondom inavyotumika na kumtupa? nafikiri sasa huko aliko anatamani kurudi CHADEMA lakini hawezi kupokelewa) Wana CHADEMA wana imani na Zitto na bado wataendelea kuwa na imani naye maana bado ni Katibu mkuu msaidizi wa Chama.

OMBI: Zitto apunguze tamaa, aombe msamaha kwa wanachadema halafu tusonge mbele na kuwaacha CCM na NCCR MAGEUZI waendelee kukodolea mkono wa CHADEMA kuwa utaanguka hadi 2015 na wasiupate1
 
Hawa ndiyo wasomi wetu ambao tunawategemea kutuongoza kwa kuwa wana mwanga .Naamini Kaburu hakuwa na haja ya kufanya haya maana kama ni chakula anacho kwa umri wake .Kushindwa Kigoma ni sawa kama hakufanya la maana wakati akiwa Mbunge .Lakini Kaburu alionekana kwa muda sana kwamba angalienda CCM tangia akiwa Mbunge na nyendo zake watu walisha zipigia kelele mno .Chadema ipo na itaendelea kuwepo .Imetulia na wenye nia njema tu watabakia .Kaburu na kuyatafuta madaraka kwa nguvu alianza zamani sana .Nani hajui historia yake ? Chadema ipo bwana mwache akatafute kula na atapata huko na mgawanyiko ndani ya CCM utaanza maana kama mtu atahaa leo na kesho kuwa Mbunge kama ilivyokuwa kwa akina Mtemvu basi CCM wenye akili lazima kujinga .Kaburu muda sana alisha onekana kutaka kuhama Chama na ni haki yake kabisa kuhama na kuishia CCM.

Mwache aende bwana kwani wa nini? tunataka watu wenyemsimamo, waaminifu, jasiri na wasio walafi.:whoo:
 
Source plz.........................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
the situation hasnt changed much...

just the blue corner members, it was kaburu, now zitto

Mkuu wako na wengine ambao walipotea katika siasa za TZ pale walipoondoka upinzani na kurudi CCM, ni vema Zitto akajifunza hili.

Unapokuwa CCM ukaenda upinzani machoni pa watanzania wengi unaonekana ni shujaa na mwanamageuzi wa kweli, lakini ukitoka upinzani na kurudi na kurudi CCM stori ni kinyume chake, utaonekana njaa na kujipendekeza mfano wa Frank Magoba, Ngawaiya,Lamwai,Makongoro nyerere, Jidulamabambasi (RIP) etc.

Kwa hiyo ni vema wanasiasa wetu wa upinzani wakakumbuka hilo kuwa imani waliyopewa ni pale tu wanapokuwa upinzani, wakikubali kutumiwa wavuruge huku wakitegemea kurudi CCM bac wakae wakijua gadhabu ya wananchi itawasubiri
 
Unapokuwa CCM ukaenda upinzani machoni pa watanzania wengi unaonekana ni shujaa na mwanamageuzi wa kweli, lakini ukitoka upinzani na kurudi na kurudi CCM stori ni kinyume chake, utaonekana njaa na kujipendekeza mfano wa Frank Magoba, Ngawaiya,Lamwai,Makongoro nyerere, Jidulamabambasi (RIP) etc.
yes kuu, statemente hii ni ya kweli na bado itaishi. by the way huyu mzee yupo wapi siku hizi?
 
Back
Top Bottom