Dr. Isaac Ndodi, jirekebishe

Umeandika nini? Hiyo lugha haieleweki ni kiingereza au kilugha chenu. Next time andika lugha unayoimudu pia ujumbe wako utafika tu bila kukashifu
We mwenyewe umetoka mirembe juzi na dozi hujamaliza unafikiri utaelewa..?

**** Maruwengee *****
 

dk.ndodi namkubali sana kama anakubore badilisha station hujalazimishwa pia yeye ndiye anayelipia kipindi wewe kusikiliza tu
 
dk.ndodi namkubali sana kama anakubore badilisha station hujalazimishwa pia yeye ndiye anayelipia kipindi wewe kusikiliza tu

Hatuwezi kuona mtu mmoja anapotosha umma halafu wazalendo tunyamaze...tutapaza sauti tuu....
 
kuna tatizo gani kumhubiri Yesu kwa kila kiumbe? Uinjilisti ni kila mahali hata mawe yatahubiriwa. Kila kiumbe na kimtukuze Bwana, Ndodi hapa hana lawama kwani si lazima kufuata imani yake. But iko siku hata wewe utavutwa kwa Yesu, muda wako tu haujafika.
However, Ndodi huwa anachanganya uinjilist na mambo mengine ya kipuuzi kama masuala ya mechi........ anashabikia kama juha, utadhani ni wale wa upande wa pili.
Hapo anatakiwa kujirekebisha
 
Mkristo anachukia Yesu Kristo anapotangazwa kwa mataifa yote??? Mkristo wa wapi wewe?

Kushauriwa usinywe pombe haina maana anayetoa ushauri ni mjinga, ila anayeukataa ndio nina uhakika hana sababu ya msingi anayoweza kutoa kuthibitisha pombe au vileo vina faida au manufaa gani katika maisha yake. Mkristo wa KWELI anatambua kuwa mwili ni hekalu la roho mtakatifu, hivyo kuliharibu na kulitia unajisi kwa pombe sio hekima wala sio Ukristo.

Sioni kinachokuchukiza anapomtangaza Yesu Kristo, hata waandishi maarufu wanaheshimika duniani kama Dr. Ben Carson (MD) ameandika vitabu maarufu kama Gifted Hands, Think Big, Big Picture na anamtangaza Yesu Kristo ndani yake.

Kama kweli ni Mkristo wa kweli, usione aibu kumtangaza Yesu Kristo maana YEYE pia atakuonea aibu mbele ya Baba yake. Na pia kusikiliza kipindi sio lazima.

Samahani lakini.
 
Simple minded just like Dr Ndodi Non alcohol beer ni pombe? Nyinyi hamuwezi kunywa Baltika?
Achana nao hawajui walitendalo YESU aliwanywesha mvinyo waalikwa kwenye harusi ya Cana Wasabato ni matatizo kuliko Walokole
mbona Wakatoliki Padri anazuia mwenyew hichi kilagi bwana hata wanawake wanakitumia hasa Safari lager kwani kinaongeza mengi
 
Bei ya dawa zake mi ndiyo nachoka kabisa utasikia 1M nakuendelea.
 
Ni shauri mzuri kwa wanawake kwani nyie walevi ni ngumu sana kuwafikisha wake zenu kileleni mnawafanya wa outsource hiyo huduma. mnatupa kazi mara mbili sisi tusio kunywa pombe kuwaridhishia wake zenu.
 
Achana nao hawajui walitendalo
YESU aliwanywesha mvinyo waalikwa kwenye harusi ya Cana
Wasabato ni matatizo kuliko Walokole
mbona Wakatoliki Padri anazuia mwenyewe
hichi kilgi bwana hata wanawake wanakitumia kwani kinaongeza mengi

Heri mimi sijasema!
 
Wewe unafikiri kunywa bia ni sifa?vipi mwenye hiyo pumzi ya uhai akiichukua?
 
Hakuna jambo la kiimani kwenye tiba za ndodi unachanganya madesa.
Ni imani za kisabato anachanganya na science ya tiba.Nimeenda hadi ofisini kwake na wale wahudumu wake almos wote ni wasabato.Mimi mwenyewe huwa namsikiliza nikiona kwangu positive nachukua na nikioana negative naacha.

Lakini jambo ambalo kwangu negative kwa mwingine ni positive.Na biblia ndivyo ilivyo kila mtu anatafsiri kivyake na ndio maana kuna utitiri wa madhehebu.

Nb nimeenda hadi ofisini kwake na nadhani anachohubiri vingine havifuati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…