Dr.hoseah na takukuru yake wanafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.hoseah na takukuru yake wanafiki

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee wa Usafi, Oct 24, 2010.

 1. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa niki fuatilia kwa makini utendaji kazi wa hii taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa muda sasa. Kwa muundo wake kwa sasa ni heri isiwepo kabisa kwani wanakula na kutuongezea gharama za kodi tu ili walipwe mishahara minono.

  Mara baada ya sakata ya Richmond kuwa hadharani unafiki wa Dr Hoseah ulijidhihirisha thahiri kwa kuipendelea serikali ya jeykey badala ya kuweka maslahi ya taifa mbele...

  kwenye kura za maoni ndani ya ccm watendaji kazi wake walikuwa na dhamira ya kweli kufanya kazi kumbe hawajui Dr Hoseah ni mwana mtandao mzuri tu yaliyotokea kwa wafanyakazi waliokamata watoa rushwa ni ya kusikitisha.... aliye mkamata mama Six ameteremshwa cheo na kuhamishwa, vile vile yule DBC wa sengerema aliyewazuia wa ccm kupokea rushwa kule bushosa ameteremshwa cheo na sasa yuko shinyanga anasugua benchi. RBC wa kilimanjaro naye hakunusurika na panga la mwanamtandao Hoseah, yupo akisoma magazeti arusha mjini. Hapa hakuna thamira ya kweli yakupambana na rushwa bali ni kuwaridhisha wafadhiri kuwa tuna kitu kama hicho. wagombea ubunge wote walio na kesi mahakamani jeykey kasema ni safi na anawahitaji je sisi tumwelewe je?
  Watu wanatoa kila siku tuhuma za mama Batilda kutoa rushwa lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yake......hivyo hii taasisi ni ya unafiki na inafanya kazi kwa directives kutoka kwa ccm
   
 2. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kampigie dr. slaa 31/10/2010
   
Loading...