Dr. Hamisi Kigwangalla na January Makamba, Kunani?

Le Grand Alexei

Senior Member
Nov 9, 2011
116
83
Nimekuwa nikifuatilia nyendo na harakati za wabunge wawili vijana wa CCM kwa muda sasa tangu waingie kwenye Ubunge. Nimekuja kugundua kuwa wote hawa wanafanya vizuri sana kama wabunge, kwa kusimamia maslahi ya Taifa na ya Chama chao, mpaka hivi siku za karibuni kufuatia msimamo wao kwenye posho walikaribia kufukuzwa uanachama wa CCM na kwa maana hiyo kuvuliwa Ubunge.

Kwa maoni yako hivi ni nani yuko juu zaidi ya mwenzake kwa misimamo? Hivi kuna fununu kwamba January Makamba yuko kwa ENL na Dr, Hamisi Kigwangalla yuko kwa Membe, je ni kweli?

Na pia ni kweli wanaandaliwa kuja kushika madaraka makubwa endapo makundi yao hayo yatashinda na kuingia Ikulu? Na pengine ndiyo maana wamekuwa wakishambuliana sana kwenye mitandao ya kijamii? January Makamba alikuwa Clouds FM kwenye Jahazi akielezea kuhusu Hoja yake ya nyumba, na Kigwangalla naye akasikika wiki hiyo hiyo Clouds FM kwenye Power Breakfast akiongelea Hoja yake Binafsi ya Kuhusu Ajira kwa Vijana.

Wadau mtujuze kuna lolote hapa kati ya hawa vijana chipukizi na machachari kutoka CCM???
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ah wapi, huwezi kumlinganisha Kigwangalla na huyo Marope Jr asiye na msimamo! HK amekuwa mstari wa mbele kabisa kutetea kwa dhati kabisa raslimali za nchi kwa nguvu zake zote. Amefanikiwa kuwatetea wachimbaji wadogo wadogo na mwezi uliopita Waziri Ngeleja kawarudishia leseni ya umiliki wananchi hao na mpaka leo nadhani Kigwangallah bado ana kesi mahakamani na alilala jela kwa ajili hii.

Kigwangalla siyo fisadi na anafaa kupewa nafasi yoyote ile ya uongozi siyo huyo Jr Makamba. Makamba ana nini huyo zaidi ya kuchangiwa pesa kupitia 'uhamasiahaji' wa dada yake Mwawar kwa wazungu, achilia mbali ukaribu wake na ENL na zile stori zake za kupewa dola 2ml na Barrick kutoka Canada
 
Makamba Jr anahaha sana kutafuta attention ya watu na kujipambanua kwamba naye ni mtu tofauti sana kwa kuwa eti alisoma USA. Hana msimamo wowote ule
 
Mie na magamba mbali mbali lakini hawa watu wawili kusema kweli nafuatilia sana kauli zao maana siku za karibuni nawaona kama wanatoa kauli ambazo nazikubali katika kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania lakini bado ni mapema mno kufikia hitimisho kama kweli ni watetezi wa Tanzania na Watanzania au ni nguvu ya soda tu ambayo haikawii kupotea.
 
Ah wapi, huwezi kumlinganisha Kigwangalla na huyo Marope Jr asiye na msimamo! HK amekuwa mstari wa mbele kabisa kutetea kwa dhati kabisa raslimali za nchi kwa nguvu zake zote. Amefanikiwa kuwatetea wachimbaji wadogo wadogo na mwezi uliopita Waziri Ngeleja kawarudishia leseni ya umiliki wananchi hao na mpaka leo nadhani Kigwangallah bado ana kesi mahakamani na alilala jela kwa ajili hii. Kigwangalla siyo fisadi na anafaa kupewa nafasi yoyote ile ya uongozi siyo huyo Jr Makamba. Makamba ana nini huyo zaidi ya kuchangiwa pesa kupitia 'uhamasiahaji' wa dada yake Mwawar kwa wazungu, achilia mbali ukaribu wake na ENL na zile stori zake za kupewa dola 2ml na Barrick kutoka Canada
Huwezi kumlinganisha January na Kigwangalla. January zaizi ya ni Zitto Kabwe!
 
Nakubali kwamba Kigwangalla ( mwenye jina halisi ambaye yupo kijijini akisukuma toroli) si fisadi. Ila huyu Andrew aliyeko bungeni ni mtafuta umaarufu tu
 
Huwezi kumlinganisha January na Kigwangalla. January zaizi ya ni Zitto Kabwe!

January na Zitto wote ni MAMLUKI; wanaweza kununliwa kiurahisi kwa pesa, si mmeona ushahidi wa pesa dada yake alizohongwa kumletea January ili amshinde Shellukindo; Zitto nae na mahela ya Dowans mpaka kununua Hammer mtoto wa kijiweni umaskini wa familia yake unajulikana , hao ndio mnaotaka kuwaachia nchi; you better leave the country to the dogs!!
 
Birds of the same feathers.
Hamna kitu tofaut hao Jamaa wanacho ambacho Serukamba hana au hata chizi wetu Ndugai
 
Nadhan Hawana Jipya!! Huwezi Kukata Tawi Huku Umelikalia!! Just Naiona kwa Hawa Jamaa!! Shame on them!! Wote mavuvuzela tu Wanatetea matumbo Yao - Period!!
 
Hawana lolote, H. Kigwangala kafika hapo alipo kwa kuiba jina la mtu, na Januari kama unavyomuona ni mtu mwenye kuwa na ndoto ya either kuw waziri wa mambo ya nchi za nje au Waziri wa Madini na Nishati (aliombewa pesa za kampeni na dadake sehemu fulani).
Yote haya wanayofanya ni ZUGA waonekane ni wazalendo, hawana lolote.
Kigwangala alipewa stimulus package kwa kusaidiwa na mama Mwanaasha, muulize hizo pesa alizifanyia nini zaidi ya kuhonga achaguliwe.
 
Makamba Jr anahaha sana kutafuta attention ya watu na kujipambanua kwamba naye ni mtu tofauti sana kwa kuwa eti alisoma USA. Hana msimamo wowote ule

Jf si Gulio la kutafuta Umaarufu LE GRAND ,Zulqrnayne,Dr kigwangalla wote hawa ni Mtu mmoja nae ni Kigwangalla acha kuleta ***** wako hapa kutafuta Umaarufu
MODs hizi post zinatupotezea muda na kujaza space humidity ndani kigwa acha utoto huu

Tazameni uandishi Wa post zote za majina niliyotaja mtaelewa
 
Makamba Jr anahaha sana kutafuta attention ya watu na kujipambanua kwamba naye ni mtu tofauti sana kwa kuwa eti alisoma USA. Hana msimamo wowote ule

Jf si Gulio la kutafuta Umaarufu LE GRAND ,Zulqrnayne,Dr kigwangalla wote hawa ni Mtu mmoja nae ni Kigwangalla acha kuleta ***** wako hapa kutafuta Umaarufu
MODs hizi post zinatupotezea muda na kujaza space humidity ndani kigwa acha utoto huu

Tazameni uandishi Wa post zote za majina niliyotaja mtaelewa naamaanisha nini
 
Back
Top Bottom