Dr Dalaly Peter Kafumu ashinda ujumbe wa NEC Igunga

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
603
340
Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi CCM wilaya ya Igunga wamemchagua Dr Dalaly Peter Kafumu kuwa mjumbe wa Nec kupitia wilaya ya Igunga. Uchaguzi ambao umefanyika jana katika ukumbi wa Nkinga mission hospital. Dr Kafumu alikuwa akichuana na Mwenyekiti wa halmashauri ya Igunga na Diwani wa kata ya Ndembezi bwana Abubakar pamoja na mama Ngesi.
 
umenishtua nilidhani ni rufaa ya kuvuliwa ubunge wake, ile hali nasikia hana mpango wa kukata rufaa.
 
CCM bwana! naona wameamua kumpa kifuta jasho, baada ya kumpotezea muda katika ubunge!
 
Huyu naye...!!!??
Si aliwahi kusema hatojihusisha tena na siasa, yamekuwa hayo tena.!!!
 
siasa bwana, jamaa aliaga zamani lkn naona bado anataka madaraka kweli ni matamu sana.
 
yaani kafumu naona laana ulioachiwa inakutafuna sana sijui unataka nini au uliambiwa huwezi kfanikiwa kwenye maisha bila siasa?
 
Huko hakuna shida njoo kwenye ulingo wa kweli....!! safari hii hatoki mtu na matusi yaliyokuwepo this time naona hakuna....!!
 
Alisema hana mpango wa kukata rufaa, ila nape na CCM wanamlazimisha kukata rufaa.
 
si alisema siasa sio fani yake hivyo anaenda kwe madini,inamaana ameghairi.?
 
alisema hana mpango wa kukata rufaa, ila nape na ccm wanamlazimisha kukata rufaa.

Nape anaona aibu kwa kuwa itaonekana ni dhahiri wanaiogopa CHADEMA, ingawa anajua fika kuwa uchaguzi ukirudiwa tutawamwaga mapema.
 
Back
Top Bottom