Dr. Dalaly Kafumu: Kusema ukweli uamuzi wa Rais katika suala la mchanga utaligharimu taifa baadae

HAIHITAJI KUWA NA CHETI CHA UCHUMI AU JIOLOJIA KUELEWA NAMNA TUNAVYOIBIWA MADINI: KWA UFUPI SANA NIKUELEZE KWAMBA SEKTA HIYO YA MADINI INA WATU WENYE MABILIONI YA DOLA NA HAO HUFANYA LOLOTE AU KUTUMIA PESA KWA KIWANGO CHOCHOTE KUFIFISHA JITIHADA ZA SERIKALI KUHAKIKISHA KWAMBA TZ INAFAIDIKA NA RASILIMALI ZAKE NA NDIO MAANA WANAKUJA NA HOJA MBALIMBALI ZA KUTUKATISHA TAMAA KWAMBA HATUWEZI ILI WAENDELEE KUCHUMA - ZAMA HIZI HAITAWEZEKANA CHINI YA JPM WAMEKWAMA. UKITAKA KUNIELEWA - JARIBU KUCHUNGUZA HISTORIA ZA WATU WOTE WANAOWATETEA WANYONYAJI HAO NA UTAGUNDUA JAMBO: WEWE CHUNGUZA TU
Mkuu mim ni michunguza moja wapo ni huyu kafumu
 
RAIS Kafanya vizuri anapaswa kupongezwa ila bado tunarudi kule kule kuwa hii ni shida ya mfumo na sio mtu mmoja mmoja haya mamigodi makubwa wakati yanaanza ilikuwa inapelekwa miswada ya dharula bungeni kubadirisha sheria ndani ya masaa 24 zinapitishwa wapinzani wa enzi zile waliyasema haya yoote yaliyoongelewa na hii tume but walipuuzwa tu kama siku zoote so imewachukua ccm zaidi ya miaka 17 kuja kukubaliana na hoja za wapinzani kuwa tunaibiwa kwenye madinithe same case kama miswada ya dharula ya mafuta na gesi ilivyokuwa inapitishwa last year wakati jk anataka kusepa tutaibiwa kwa miaka 17+ then ndio tuje kujua tunaibiwa wakati akina lissu mnyika,msigwa walishalivalia njuga since day one! Hapa CCM wamejitekenya wenyewe halafu wanacheka wenyewe
ndio maana nilisema makuhadi wa mabwanyenye hawana budi kusoma alama za nyakati kwa maana sio CCM pekeee hata kuna mwanasiasa wa upinzani juzi tu alianza kutupotosha katika suala hili hili la mchanga wa madini wote hawa ni makuhadi ambao wajue muda wao umekwisha sasa
 
Mpaka sasa sina hakika na matokeo ya taarifa ya tume, hivyo hivyo pia pia kwa SGS wanaofanya migodini!
 
Wanaanza kutoka mashimoni sasa.
Mbona hamkutumbia kiasi gani siku zote hizo. Hapa ndo unajua wachache wanaonufaika.
Pope kasema vinu viko 4 tu so chakwetu kitakuwa cha tano maanayake Bado soko lipo.

Kafumu kwanini hakusimamia utekelezaji wa Sera akiwa wizarani.
Hivi huyu ana elimu kubwa kushinda muhongo anayesema kila siku wapo wawili tu Afrika nzima.

Elimu wakati mwngine sio kigezo cha kuwa muwajibikaji.

Kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu.
 
Ni nani aliyemwambia Kafumu Serikali inakurupuka kwenye hili sakata? HV tangu Rais aingie Madarakani anajuaje kama hakuwa anadeal na hii inshu? Je na hizo kamati zenye wataalamu waliobobea zaidi yake iliyofanya kazi kwa zaid ya miez 2 bado nikukurupuka? . Hatutaki siasa muda ndio huu Ikulu ni Taasisi kubwa sio ya one Man show kama anavyodhani
 
Wanaume wanazungumza wewe unakuja na habari za baba wa Taifa , kwani huyo babaako wa Taifa ni mungu?si ndie alieleta ufukara hapa Tz? Swaini kabisa yule, comedian yule chizi kabisa.
Taahira mkubwa wewe!!!!???. Yaani kumtukana baba wa taifa unajiona zinatosha.mwendawazimu mkubwa wewe
 
Mwisho WA siku Mtaelewa tu, kuwa Nani yupo upande WA WAKOLONI MAMBO LEO na nani yupo upande WA TANZANIA na vizazi vyake vijavyo
 
Dr kamfumu nae ni jambazi kama majambazi mengine, aliongwa ili atudanganye, na yeye c alikuwa kwenye hii wizara? Ashughulikiwe nae tena ipasavyo.
huyu kafumu ni culprit. alikua huko wizarani wakati hii mikataba ya kijizi inafanyika. saa hizi ana hofu mtego usije kumfetukia.
 
Mhe.Dr.Dalaly Kafumu (Mbunge wa Igunga na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Viwanda na Biashara) ametoa maelezo yafuatayo kuhusu agizo la kuzuia kusafirisha mchanga nje ya nchi;
______________________________________________

Suala la kuhakikisha Tanzania inachenjua madini yote hapa nchini; Mhe Rais yuko sawa kwani ni la kisera; Sera ya Madini ya mwaka 2009 (niliyosimamia utengenezaji wake); kifungu 5.11; policy statement no. 3 inasema hivi: (iii) The Government will collaborate with the private sector, regional and international organisations to strategically invest in smelting and refining.

Kwahiyo mchakato wa kuchenjua mchanga hapa nchini ni matakwa ya kisera lakini shida inakuja tu pale ambapo shughuli hii inaanzishwa kwa haraka na dharura kubwa. Hali hiyo inaweza kuleta uhusiano usio sawa na makampuni ya kimataofa na hata nchi makampuni yanakotoka.

Pia maamuzi haya ya haraka yatatupotezea mapato kama wengine walivyosema. Nia njema na nzuri ya Mhe.Rais ni lazima iendelezwe kwa kumshauri tena Mhe.Rais aangalie namna bora zaidi ya kufikia malengo haya mazuri ya Sera ya Madini ya mwaka 2009.

Washauri wa Mhe Rais - wizara yenye dhamana, tafadhali ni wajibu wenu; na jukumu lenu kumsaidia Mhe Rais juu ya hili jambo jema lenye manufa kwa Taifa letu.

Dr.Dalaly Kafumu
____________________

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Dr.Kafumu ni mtaalamu aliyebobea wa madini. Kwa wale wasiomfahamu vizuri ana shahada ya madini na elimu miamba (B.Sc in Geology) kutoka chuo kikuu UDSM. Ana Stashahada ya juu ya elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Chuo Kikuu UDSM.

Pia ana Stashahada ya Juu ya Uchakataji Madidi (Postgraduate Diploma in Mineral Exploration) kutoka Institute of Aerospace Science, Uholanzi. Ana Shahada ya Uzamili ya madini na elimu miamba (M.Sc in Geology) kutoka Chuo kikuu cha Brussels, Ubeligiji. Na Shahada ya Uzamivu ya madini na elimu miamba (PhD in Geology) kutoka Chuo kikuu cha Brussels, Ubeligiji.

Nimeamua kueleza historia fupi ya elimu ya Dr.Kafupi ili tujue kwamba ni MTAALAMU ALIYEBOBEA kwenye masuala ya madini. Ushauri wake ni ushauri wa kitaalamu na si wa kupuuzwa. Kama JPM anataka kuisidia nchi yetu afanyie kazi ushauri wa Dr.Kafumu.

Kwa lugha rahisi Dr.Kafumu anasema suala la kuchakata mchanga wa madini nchini ni la kisera. Sera ya madini ya mwaka 2009 inaelekeza mchanga unaobaki uchakatwe nchini badala ya kusafirishwa nje. Lakini Dr.Kafumu anashauri kuwa ni vema kuwe na utaratibu mzuri wa kufaniksha jambo hili badala ya "kukurupuka".

"Kukurupuka" kunaweza kuliingiza taifa kwenye hasara. Kwa mfano taarifa ya mgodi wa Geita inaeleza kuwa wanapata hasara ya dola milioni 1 kila siku (zaidi ya Bilioni 2 za kitanzania) kutokana na mchanga huo kuzuiwa kwenda nje. Pia Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe amesema hadi sasa nchi imeingia hasara ya Trilioni 1.3 kutokana na maamuzi ya kuzuia mchanga huo kusafirishwa.

Sasa unaweza kujiuliza kama kwa siku mbili tumepata hasara ya trilioni 1, mchanga huo ukiendelea kukaa bandarini kwa muda mrefu zaidi ni hasara kiasi gani. Kadri mchanga unavyoendelea kukaa ndivyo hasara inaongezeka zaidi. Je nani atalipa hasara hii?

On other hand, migodi kadhaa imetangaza kusimamisha ajira kwa wazawa baada ya mchanga huo kuzuiwa bandarini. Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya kazi za kuchimba mchanga huo, kupembua, hadi kusafirisha zinafanywa na wafanyakazi wazawa. Tayari mgodi mmoja umewafuta kazi wafanyakazi zaidi ya 80 jana kufuatia kadhia hiyo.

Lakini swali la msingi sana tunalopaswa kujiuliza ni je tuna uwezo wa kuchakata mchanga huo ili kupata madini? Inaelezwa kwamba 20% ya vipande vya madini hubaki kwenye mchanga huo. Lakini je tuna uwezo wa kuchakata udongo ili kupata madini hayo?

Mfanyabiashara Zacharia Hans Pope anasema dunia nzima kuna vinu vinne tu vya kuchakata udongo ili kuexcute madini yaliyopo. Hans Popa anasema gharama za kutengeneza kinu kimoja ni karibu bajeti yetu ya mwaka mzima. Yani mwaka mzima tusile, tusivae, tusinywe, tusilipe mishahara, tusiuze, tsinunue, tusizalishe chochote.

Uchumi wa nchi usimame ndipo tuweze kutengeneza angalau kinu kimoja cha kuchenjua udongo utakana na madini. Hans Pope anasema hata tukiweza kujenga kinu hicho, bado hatuwezi kukiendesha. Tunahitaji umeme mkubwa sana ili kuendesha kinu hicho. Tunahjtai angalau nusu ya umeme wote tunaotumia kwa sasa ili kuendesha kinu kimoja.

Kama taarifa hiyo ya Hans Pope ni kweli, maana yake ni kwamba hata tukizuia udongo huo kwenda nje, bado hatuwezi kuchakata udongo huo hapa nchini. Sasa kwanini tunazuia udongo kusafirishwa nje wakati hatuna uwezo wa kuuchakata?

Yani huu wivu wa kuzuia kitu ambacho hatuwezi kukutumia kwa manufaa umetoka wapi? Mbona ni wivu wa ajabu sana? Kuna kisa cha "choyo cha mbwa kwa majani ya ng'ombe." Yani mbwa anapomfukuza ng'ombe asile majani wakati yeye hawezi kuyala. Nadhani kuna haja ya kutafakati upya suala hili.

Vinginevyo tutabaki na mchanga ambao hatuwezi kuufanyia chochote, huku tukiingiza taifa hasara. Mwisho wa siku mchanga utazuia nafasi bandarini na kuzuia mizigo inayoingia kukosa nafasi na kuipelekea bandari kavu ambako ni gharama zaidi. Yani hasara mara dufu.

Hata hivyo naungana na ndugu Exaud Mshana kwamba badala ya kukimbizana na huo mchanga (concentrate) wenye 20% gold tungejikita kwenye 80% extracted gold ili value addition yake ifanyike hapa kwetu. Haya ya kuzuia vifusi vya mchanga wakati hatuna uwezo wa kuextract ni kujilisha upepo. Tuache ubabe usio na manufaa.!

Malisa GJ
Unasema ripoti ya Mgodi wa Geita inaeleza kwamba wanapata hasara ya dola za kimarekani milioni 1 kwa siku kwa kuzuiwa kusafirisha Copper Concentrate nje ya nchi, ni lini Mgodi wa Geita umezalisha Copper Concentrate? Je hiyo ripoti ya Geita unaweza kuiweka hapa tuione? Copper Concentrate inazalishwa na migodi miliwi tu Tanzania yaani Bulyanhulu na Buzwagi na si vinginevyo. Hii ndo shida ya kuambiwa tu na kuchukua jambo kama lilivyo bila kufanya utafiti...!!!
 
Kwa nini leo aje hapa kuongea yeye kama Kamishina wa madini na waliomfuata wote ni lazima wanahusika kwa namna ye yote na kwa nini hawakujitokeza mwanzoni? Na ndiyo maana akavaa viatu vya aliekuwa mbunge wa jimbo kwa namna moja ama nyingine ndie master mind hadi leo forbes ianamtambua na siku ya kuondoka akatupa salaam .
 
Malisa ungemsikiliza mh raisi alivyosema leo kuhusu huyu Dr/Prof Kafumu,yeye ndie mnufaika wa huo mchanga ,yeye ndie alikuwa kamishna mkuu wa madini wakati uwizi huu ulipoanza na hakufanya chochote kwa kuwa alikuwa mnufaika na genge lake,sasa kaaumbuliwa ndio analeta porojo zake na wewe Malisa kwa kuwa ni kijana wa Ufipa umerukia na kumuona yeye Kafumu ndio wa maana,na je kwenye tume hao wasomi wote wamekuwa wajinga kiasi cha sisi tusiwaamini bali tumwamini huyo Kafumu,na anabahati kwa kuzaliwa Tanzania ,angekuwa kazaliwa China saa hii angeshakuwa historia.
Malisa acha ujinga na acha siasa kwenye mambo ya manufaa ya umma kumbuka anachokipigia kelele mheshimiwa raisi ndicho kinachokuweka mjini wewe pamoja na familia yako,hizo hela ndio zinalipa ruzuku ya mwajiri wako Chadema,hiyo ruzuku ndio mshahara wako kwa hiyo acha upuuzi ,muda si mrefu tutamsikia mwenda wazimu mwingine Kimambi akija na ujinga wake hapa .
safi mfianchi kazi yao ufipa kula ruzuku kwa kesi huku jpm anahangaika kudhibiti ujambazi dhidi ya taifa.
 
Back
Top Bottom