Dr. Christopher Cyrilo anaandika juu ya amani nchini

mtanganyika wa kweli

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Posts
2,420
Reaction score
1,724
CDF Mabeyo anashangaa kwa nini watu wana hofu na matukio ya mashambulizi ya risasi ya hivi karibuni kuliko ilivyokuwa wakati wa mauaji ya viongozi wa vijiji vya kibiti.
CDF Mabeyo amegundua kuwa watu wana hofu kwa sababu mitandao na vyombo vya habari vimechafukwa na kauli za kulaani jaribio la kumuua Mh. Tundu Lissu.

Nitatumia haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni kumjibu au kumkumbusha CDF Mabeyo, huku nikiwa na ufahamu kabisa kuwa Haki ni bidhaa adimu katika utawala huu wa Magufuli. Lakini hilo alitufanyi tukae kimya. Tutakaa kimya tukiwa wafu, kama wapendavyo.

Kwanza. Hakuna kipimo sahihi kujua endapo watu wana hofu zaidi kipindi hiki kuliko ilivyokuwa wakati wa mauaji ya Kibiti. Viongozi wa kisiasa walipiga marufuku suala la Kibiti kuzungumzwa. Vyombo vya habari viliwekwa mipaka ya kuripoti mambo ya Kibiti. Spika wa Bunge alizima hoja za wabunge wanne au watano walioibua hoja za Kibiti, kwa utashi wake au kwa maelekezo kutoka juu, hatujui.

Pili. CDF Mabeyo, amejitokeza kuzungumzia masuala ya usalama wa ndani, wakitia yeye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi. Kwa bahati mbaya, nyakati hizi za Magufuli, jina mkuu wa majeshi- halitii hamu kulitamka. Na hata akizungumza, watu hawatilii maanani sana. Na hata yeye mwenyewe ameona hivyo na habari yake haikuwa nzito, hata gazeti la uhuru limeipa uzito mdogo habari yake. Ni tofauti na nyakati zilizopita, mkuu wa majeshi akizungumza, enzi hizo Tanzania inatikisa vichwa! Kukubali au kutafakari. Kwanini! Labda kwasababu Mabeyo sio maarufu, au bado hajawa maarufu kiasi cha kuuza habari. Lakini sababu sahihi yaweza kuwa hofu ya wananchi kuhusu matukio haya ni kubwa na sauti ya generali haina nguvu ya kupunguza hofu hiyo. Ndio maana watu wameendelea kuongelea jaribio la kumuua Tundu Lissu. Na kauli ya Mabeyo kutaka watu watulie imeyeyuka hewani. Ndio kwanza watu wanasoma albadir.
Tatu! Kwanini CDF Mabeyo azungumze wakati huu! Sio kwamba na yeye ana hofu? Naweza kusema CDF Mabeyo ana hofu kuhusu hofu kubwa ya wananchi wakati huu. Hofu yake imemfanya atoke au ashauriwe kutoka hadharani kuzungumzia masuala ya usalama wa ndani wakati yeye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi wa nchi. Hofu imemfanya akope kwa muda, nafasi ya IGP Sirro. Pengine kwa sababu Sirro amezoeleka na hatishi, akasahau na yeye hajazoeleka na wananchi hawamjui, na kwa hiyo ombi lake la kutaka wananchi kuondoa hofu, limekuwa ombi la mtu mgeni asiyejua masaibu yanayowakuta wananchi na kuwasababishia hofu hiyo kubwa. Pengine!!!

Inawezekana katika watu mia moja wanaozungumza habari ya Lissu, wawili au watatu kati yao ndio wamepata taarifa za kauli ya CDF Mabeyo

Maswali kwa Mabeyo.
Sio lengo langu kujibiwa maswali haya, mimi ni nani hata nijibiwe na mkuu wa majeshi?
Lakini si kila swali linahitaji jibu, maswali mengine yanahitaji tafakuri tu! Na najua kuwa maswali haya hayamhusu CDF Mabeyo, lakini yanamuhusu Bw. Mabeyo, kama mwananchi wa Tanzania.
Moja! Badala ya kushangaa, Kwanini asijiulize kuhusu hofu kubwa ya wananchi wakati huu kuliko ilivyokuwa Kibiti, na kisha kupata majibu na kuyafanyia kazi kama mkuu wa majeshi?

2. Je! CDF Mabeyo anaposhangaa kuhusu hofu kubwa ya wananchi katika jaribio la kumuua Tundu Lissu zaidi ya mauaji ja Kibiti, ina maana yeye ana hofu kubwa zaidi kuhusu mauaji ya Kibiti kuliko jaribio la kumuua Lissu? Kwamba kuna matukio yanahitaji hofu kubwa na mengine yanastahili hofu ndogo?

3. Ni nani anayeweza kurusha risasi zaidi ya 30, mchana kweupe, mjini, makao makuu ya nchi, jirani na makazi ya viongozi wakubwa wa nchi, na asikamatwe? CDF Mabeyo, hilo ni la kushangaza zaidi kuliko unaloshangaa! Bila kububuja maneno, mazingira hayo yanatoa taswira mbili. Moja hakuna vyombo vya usalama!
pili, Vyombo vya usalama vinahusika!
Katikati ya hayo mawili ndio kuna mshangao mkubwa zaidi ambao CDF Mabeyo anatakiwa kuwa nawo. Na hapo ndio kuna hiyo hofu kubwa kwa wananchi ambayo CDF Mabeyo anaishangaa!

Mwisho.
CDF Mabeyo, nafasi yako ni nyeti sana na usalama wa nchi upo mikononi mwako. Tunapozungumzia jeshi la wananchi, tunazungumzia binadamu wenzetu walioacha maisha na kuchagua kufa ili kulinda uhai w wengine.

Vyombo (vinavyoitwa) vya usalama vya ndani, (polisi na usalama wa taifa) vimeshatiwa najisi na siasa. Vijana wenye akili wasiotaka kujiunga na jeshi la polisi kisa linatumika kisiasa wanaongezeka, na waliopo humo, tukikutana nao nje ya sare zao, sio wenzetu tena, wanajitenga kwa aibu, au kujichekesha kwa aibu! Na wengine hawapendi kujitambulisha kwa hofu! Wanajua wanachukiwa sana.
Lakini ni tofauti kwa wanajeshi! Tunawaheshimu kweli na hatusiti kulipa bili kwa ajili yao. Ni ndugu zetu, kaka na dada zetu na marafiki wa karibu.
Watawala waliopita wametumia jeshi la wananchi na kulinajisi kwa siasa mara kadhaa! Lakini kwa hulka za utawala awamu hii, jambo hili litakuwa na gharama kubwa. Chonde!
 
Aisee badilisha Heading bana....Heading haiendani na kilichopo ndani ya uzi..
 
Mab y

Mabeyo alinde mipaka yetu. Asubiri kiwake aingie vitani. Masuala ya amani ya ndani awaachie raia wakakamavu (polisi) ambao kwa bahati mbaya kwa sasa si wakakamavu tena! Ukimvua kofia polisi ili kutunza heshima ya nchi, waweza kumpiga kama kuku jike!
 
Ni article mzuri sana, kuna hoja za msingi mno humo
 
Inapofika kipindi watawala wakakataza watu kumwomba Mungu wao NCHI IMEFIKA PABAYA SANA. Kwa nini wanakataza watu wasimwombee mtu fulani wakati wao wenyewe wanajua umuhimu wa maombi na kila mara wanahimiza watu wawaombee?
 
watampoteza utawala wa damu huuu jamaani angalieni
 
Huyo mabeho ndo nani ktk nchi hii ,I think he is not popular in the country at all
 
Musukukuma Joseph,Magufuli John CDF Mabeyo wananikumbusha hadithi maarufu ya Shakespeare "The Three Musketeers"
Kila mmoja anashambulia adui kivyake vyake
 
CDF Mabeyo anashangaa kwa nini watu wana hofu na matukio ya mashambulizi ya risasi ya hivi karibuni kuliko ilivyokuwa wakati wa mauaji ya viongozi wa vijiji vya kibiti.
CDF Mabeyo amegundua kuwa watu wana hofu kwa sababu mitandao na vyombo vya habari vimechafukwa na kauli za kulaani jaribio la kumuua Mh. Tundu Lissu.

Nitatumia haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni kumjibu au kumkumbusha CDF Mabeyo, huku nikiwa na ufahamu kabisa kuwa Haki ni bidhaa adimu katika utawala huu wa Magufuli. Lakini hilo alitufanyi tukae kimya. Tutakaa kimya tukiwa wafu, kama wapendavyo.

Kwanza. Hakuna kipimo sahihi kujua endapo watu wana hofu zaidi kipindi hiki kuliko ilivyokuwa wakati wa mauaji ya Kibiti. Viongozi wa kisiasa walipiga marufuku suala la Kibiti kuzungumzwa. Vyombo vya habari viliwekwa mipaka ya kuripoti mambo ya Kibiti. Spika wa Bunge alizima hoja za wabunge wanne au watano walioibua hoja za Kibiti, kwa utashi wake au kwa maelekezo kutoka juu, hatujui.

Pili. CDF Mabeyo, amejitokeza kuzungumzia masuala ya usalama wa ndani, wakitia yeye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi. Kwa bahati mbaya, nyakati hizi za Magufuli, jina mkuu wa majeshi- halitii hamu kulitamka. Na hata akizungumza, watu hawatilii maanani sana. Na hata yeye mwenyewe ameona hivyo na habari yake haikuwa nzito, hata gazeti la uhuru limeipa uzito mdogo habari yake. Ni tofauti na nyakati zilizopita, mkuu wa majeshi akizungumza, enzi hizo Tanzania inatikisa vichwa! Kukubali au kutafakari. Kwanini! Labda kwasababu Mabeyo sio maarufu, au bado hajawa maarufu kiasi cha kuuza habari. Lakini sababu sahihi yaweza kuwa hofu ya wananchi kuhusu matukio haya ni kubwa na sauti ya generali haina nguvu ya kupunguza hofu hiyo. Ndio maana watu wameendelea kuongelea jaribio la kumuua Tundu Lissu. Na kauli ya Mabeyo kutaka watu watulie imeyeyuka hewani. Ndio kwanza watu wanasoma albadir.
Tatu! Kwanini CDF Mabeyo azungumze wakati huu! Sio kwamba na yeye ana hofu? Naweza kusema CDF Mabeyo ana hofu kuhusu hofu kubwa ya wananchi wakati huu. Hofu yake imemfanya atoke au ashauriwe kutoka hadharani kuzungumzia masuala ya usalama wa ndani wakati yeye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi wa nchi. Hofu imemfanya akope kwa muda, nafasi ya IGP Sirro. Pengine kwa sababu Sirro amezoeleka na hatishi, akasahau na yeye hajazoeleka na wananchi hawamjui, na kwa hiyo ombi lake la kutaka wananchi kuondoa hofu, limekuwa ombi la mtu mgeni asiyejua masaibu yanayowakuta wananchi na kuwasababishia hofu hiyo kubwa. Pengine!!!

Inawezekana katika watu mia moja wanaozungumza habari ya Lissu, wawili au watatu kati yao ndio wamepata taarifa za kauli ya CDF Mabeyo

Maswali kwa Mabeyo.
Sio lengo langu kujibiwa maswali haya, mimi ni nani hata nijibiwe na mkuu wa majeshi?
Lakini si kila swali linahitaji jibu, maswali mengine yanahitaji tafakuri tu! Na najua kuwa maswali haya hayamhusu CDF Mabeyo, lakini yanamuhusu Bw. Mabeyo, kama mwananchi wa Tanzania.
Moja! Badala ya kushangaa, Kwanini asijiulize kuhusu hofu kubwa ya wananchi wakati huu kuliko ilivyokuwa Kibiti, na kisha kupata majibu na kuyafanyia kazi kama mkuu wa majeshi?

2. Je! CDF Mabeyo anaposhangaa kuhusu hofu kubwa ya wananchi katika jaribio la kumuua Tundu Lissu zaidi ya mauaji ja Kibiti, ina maana yeye ana hofu kubwa zaidi kuhusu mauaji ya Kibiti kuliko jaribio la kumuua Lissu? Kwamba kuna matukio yanahitaji hofu kubwa na mengine yanastahili hofu ndogo?

3. Ni nani anayeweza kurusha risasi zaidi ya 30, mchana kweupe, mjini, makao makuu ya nchi, jirani na makazi ya viongozi wakubwa wa nchi, na asikamatwe? CDF Mabeyo, hilo ni la kushangaza zaidi kuliko unaloshangaa! Bila kububuja maneno, mazingira hayo yanatoa taswira mbili. Moja hakuna vyombo vya usalama!
pili, Vyombo vya usalama vinahusika!
Katikati ya hayo mawili ndio kuna mshangao mkubwa zaidi ambao CDF Mabeyo anatakiwa kuwa nawo. Na hapo ndio kuna hiyo hofu kubwa kwa wananchi ambayo CDF Mabeyo anaishangaa!

Mwisho.
CDF Mabeyo, nafasi yako ni nyeti sana na usalama wa nchi upo mikononi mwako. Tunapozungumzia jeshi la wananchi, tunazungumzia binadamu wenzetu walioacha maisha na kuchagua kufa ili kulinda uhai w wengine.

Vyombo (vinavyoitwa) vya usalama vya ndani, (polisi na usalama wa taifa) vimeshatiwa najisi na siasa. Vijana wenye akili wasiotaka kujiunga na jeshi la polisi kisa linatumika kisiasa wanaongezeka, na waliopo humo, tukikutana nao nje ya sare zao, sio wenzetu tena, wanajitenga kwa aibu, au kujichekesha kwa aibu! Na wengine hawapendi kujitambulisha kwa hofu! Wanajua wanachukiwa sana.
Lakini ni tofauti kwa wanajeshi! Tunawaheshimu kweli na hatusiti kulipa bili kwa ajili yao. Ni ndugu zetu, kaka na dada zetu na marafiki wa karibu.
Watawala waliopita wametumia jeshi la wananchi na kulinajisi kwa siasa mara kadhaa! Lakini kwa hulka za utawala awamu hii, jambo hili litakuwa na gharama kubwa. Chonde!
Du.. nondo muafaka!
 
Knachofanyka sasaivi n kujalbu kizma hil sakata la lsu, na wakae wakjua hl swala haliish hivi hvi na yamkn ndo tukageuka syria waspokua makni na hl, hatuwez ona watawala wanatufanyia unyama kanakwamba hii inch n yao na family zao, haiwezekan tunataka haki itendeke sio kuleta ubabe wa kjeshi apa
 
Hakika Dr Christopher kwenye thread yako article namba 03, imebeba theme nzima! iko very brief hakika maswali haya yameulizwa na Daktari wa,falsafa,PhD! eko!!
 
Mwambieni baba Mchungani amwandikie Mbowe ili amruhusu yule Dereva wa Lissu arudi Tanzania kusaidia uchunguzi.
 
3. Ni nani anayeweza kurusha risasi zaidi ya 30, mchana kweupe, mjini, makao makuu ya nchi, jirani na makazi ya viongozi wakubwa wa nchi, na asikamatwe? CDF Mabeyo, hilo ni la kushangaza zaidi kuliko unaloshangaa! Bila kububuja maneno, mazingira hayo yanatoa taswira mbili. Moja hakuna vyombo vya usalama!
pili, Vyombo vya usalama vinahusika!
Katikati ya hayo mawili ndio kuna mshangao mkubwa zaidi ambao CDF Mabeyo anatakiwa kuwa nawo. Na hapo ndio kuna hiyo hofu kubwa kwa wananchi ambayo CDF Mabeyo anaishangaa!

Chonde!
Aisee, hii paragraph nahisi ndo imebeba ukweli wote.
 
Back
Top Bottom