Dr. Chami akanusha kuhusu ujumbe unaosambaa unaoiponda Serikali ya awamu ya tano

Gilbert A Massawe

JF-Expert Member
May 14, 2015
4,912
3,987
c4c241b6176657fc318a625ccc812f3a.jpg


Habari za muda huu wanjf
Aliyekuwa mbunge wa moshi vijijini 2005-2015
Dr Cyril Chami anakanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii amabazo zinamchonganisha yeye na Rais Magufuli pamoja na serekali ya Chama cha mapinduzi (CCM) ikumbukwe Chami ni mjumbe wa halmashauri kuu kutoka Wilaya ya Moshi Vijijini
"Mimi sina ubaya wowote na mtu ila kuna watu wameamua kunichafua kwa mategemeo yao ya kisiasa"-Dr Chami
Pia Dr Chami hana account yeyote ya mitandao ya kijamii iwe Facebook,Twitter,hata Instagram

Ni wenu mzalendo
Gilbert Massawe
 
Hii tabia ya kuwazushia watu mambo ambayo hata hawajayasema kwenye social media naona inazidi kupata kasi, huu sio uungwana kabisa.
 
Waacheni wafu waendelee kuzika wafu wao ....."what goes around, comes around"
 
Mbona maneno hayo, ambayo ni ukweli mtupu, yanatamkwa waziwazi au kichinichini au pia kimoyo moyo na watanzanzania walio wengi ndani na nje ya CCM ? Nani asiyejua kuwa hali ya Tanzania kiuchumi, kisiasa, kiutendaji na hasa kijamii mambo siyo mazuri ? Nani asiyejua kuwa wananchi wengi wanaishi kwa woga ? vijana hawana ajira? Mikopo kwa vijana wengi wa vyuo vyetu vya juu hawapati tena mikopo ? Kwamba hata Katiba inavunjwa waziwazi ? nk. nk. nk. nk.
 
Back
Top Bottom