Dr. Ben Carson Kugombea Urais wa Marekani

upupu

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2008
Posts
614
Reaction score
198
Yule Daktari bingwa wa upasuaji, (neurosurgery) na muandishi wa vitabu maarufu ametangaza kuwa atagombea urais wa marekani endapo wananchi wataona anafaa kufanya hivyo,

Earlier today, Dr. Ben Carson announced on his Facebook that he would be launching a 2016 presidential exploratory committee:

"I am pleased to announce that I have established a Presidential Exploratory Committee to examine whether I should become a candidate for President of the United States. If I believe that I have your support and your commitment to help, I will run for President to lead this great country to a brighter future. I will use these next few months to listen to you and prepare to answer that question myself. I look forward to traveling across this mighty nation to listen to your thoughts and ideas."

http://goo.gl/p2uNG8
 
atoke democrat au republican wont make a difference as all are zionists and illuminati puppets.
 
Mwakani anaingia bush mdogo, republicans wakiingia wanarudi vitani rasmi.

"If you're not with us, you're against us" G W Bush
 
​Huyu jamaa anapoteza muda wake bure pia na pesa zake bora hata angeenda kuwekeza NYSE.
 
Anapoteza muda wake...Aendelee na kazi yake ya kutunga vitabu...

Ni ndoto za alinacha kwa Mtu mweusi tena kuwa Rais wa Marekani..
 
hivi hili neno ALINACHA ni kitu gani? huwa najiuliza ever since i was 10 sijawah pata jibu! ni mtu au kitu? msaada kwa anaejua..
 
​Huyu jamaa anapoteza muda wake bure pia na pesa zake bora hata angeenda kuwekeza NYSE.

Urais wa Marekani siyo lazima utumie pesa zako, unagharimikiwa na wananchi kupitia michango inayoratibiwa na taratibu za kisheria. Ndiyo maana hata sasa kuna watu wanachangisha ili kumshawishi agombee. Mpaka sasa hajatangaza rasmi kwamba atagombea ndiyo maana ameunda kamati ya kuangalia kama ana support ya kutosha kufanya hivyo.
 
Angalia hiyo link kwenye bandiko #10, haina maana atatumia 100% pesa zake.

Urais wa Marekani siyo lazima utumie pesa zako, unagharimikiwa na wananchi kupitia michango inayoratibiwa na taratibu za kisheria. Ndiyo maana hata sasa kuna watu wanachangisha ili kumshawishi agombee. Mpaka sasa hajatangaza rasmi kwamba atagombea ndiyo maana ameunda kamati ya kuangalia kama ana support ya kutosha kufanya hivyo.
 
hivi hili neno ALINACHA ni kitu gani? huwa najiuliza ever since i was 10 sijawah pata jibu! ni mtu au kitu? msaada kwa anaejua..

Alinacha ni character kwenye vitabu vya zamani vya hadithi, alikuwa akihangaika na maisha, kuna siku alikuwa amekaa sehem na biashara yake kwenye sinia anauza, akasinzia akawa anaota, ana maisha mazuri, akimiliki magorofa na vito vya thamani, mara akakurupuka usingizini akamwaga biashara yote, na mambo yote yakaishia hapo, hyo ndo ndoto ya alinacha
 
Nikusahihishe kidogo: alikuwa na biashara ya kuuza bilauri alizozitia kwenye pakacha. Aipochoka akaegemea chini ya mti kupumzika. Mbele yake kulikuwa na jumba la ghorofa. Akawaza kuwa siku moja biashara yake hiyo itafaikiwa naye atanuua jumba kama lile. Kisha atanunua vijakazi wamtumikie. Akawaza kuwa siku moja kijakazi atamkasirisha halafu yeye atampiga teke kwenda kuleee. Kumbe akalipiga teke lile pakacha lake na bilauri zile zote zikavunjika. Na huo ndio ukawa mwisho wa ndoto zake za mchana!
 
Haikuwa hadithi moja pekee, bali ni mtiririko wa hadithi za matukio akiyoyafanya menfine yakihusisha ndoto alizoota ambazo mwisho zilikua zikimharibia hata kile kidogo alicho nacho.
Ni kama zile hadithi za Abunuasi zilizokua maarufu kwa Afrika mashariki na zile za Avanti kwa Uchina.
 
Anaacha kuwndelea kutunga vitabu sasa anaanza kutunga urais.
Au wameshageuza weusi kuwa ni mtaji wa wa madaraka huko Amerika!?
 
Back
Top Bottom