Dr. Bashiru: Nikiwa na hoja na mipango thabiti nitaenda majukwaan kuongea na wananchi!

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
3,450
Wadau hayo maneno aliyasema wakati akihojiwa na Tido Mhando katika kipindi cha funguka!Bahati mbaya JF haikuwa hewani!

Swali no je,yeye ni mbunge wa jimbo gani?Maana mwenyekiti wake amezuia watu wengine tofauti na wabunge kufanya mikutano ya hadhara,na zaidi hao wabunge wafanye kwenye maeneo yao ya jumbo na ni marufuku kuleta mzungumzaji kutoka nje!

Nawaza tu kwa sauti!!!!!!!
 
Ccm ruksa tena na ulinzi juu kwani hukumuona mwenyekiti wa uvccm afanye vile wa bavicha uone polisi wanakavyowang'ang'ania
 
Kipindi cha Funguka : Azam TV,
Katibu Mkuu mpya wa CCM Dr. Bashiru Ally afunguka maisha yake ya kisiasa ndani ya CCM na ndoto yake ya kukifanya chama chao kiwe tofauti na hapo nyuma, yaani ' kuleta upya' kupitia falsafa ya CCM MPYA !

Source: Azam TV
 
TIDO, zile simulizi za maisha yako hasa ya kikazi pale RTD Pugu road ulikuwa unaandika kwenye gazeti la Mwananchi, lini utachapisha kitabu, nilikuwa nafuatilia ila kuna baadhi nilizikosa....

Mwongozo wako tafadhali.....
 
Back
Top Bottom