Dr. Ayub Rioba atoa Mwelekeo wa TBC kwa Mwaka 2018. Kufikisha viwango vya juu kiwango cha BBC

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,

Angalia TBC Live, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dr. Ayoub Rioba Chacha, atoa mwelekeo wa TBC for 2018.

Kipindi nimekukitia katikati,
Dr. Rioba amesema amepania kuipaisha TBC kwa kuifanyia maboresho mabalimbali hadi kufikia katika viwango vya kimataifa kama vya BBC.

Dr Rioba amesema kwa hali ilivyo sasa, TBC imejitahidi sana, lakini amekiri TBC kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwa sababu TBC ina operate katika mazingira magumu sana, hivyo amewashukuru sana wafanyakazi wa TBC kwa kufanya kazi kwa kujituma na moyo wa kujitolea licha kufanya kazi katika mazingira magumu ya kazi na huku wakilipwa maslahi duni. Kwa mwaka 2018 atajitahidi sana kuboresha maslahi kwa kuanzia na malipo ya posho ambazo tayari zimeisha kuwa approved na bodi.

Kuhusu kutaka kufanya baadhi ya mambo na kujikuta anakwamishwa na urasimu wa serikali, Dr Rioba, amepigilia misumari kuwa ili TBC ipae na kufikia viwango vya BBC, ziko sheria, taratibu na kanuni za serikali lazima zinadilishwe, ili ziendane na mabadiliko tarajiwa, amekiri urasimu na baadhi ya taratibu za kiserikali zinamuwekea usiku, kuikimbiza TBC kubadilika, hivyo kushindwa kufanya mambo makubwa on time kwa wakati tarajiwa. Ametolea mfano ili kufanya baadhi ya mambo ni lazima uandike barua huku na kule, kuna baadhi ya idara barua inakaa hadi miezi miwili haijajibiwa!, amesema yeye akipokea barua zote huzijibu pale pale!, amesisitiza huu urasimu usio wa lazima katika baadhi ya maeneo serikalini lazima uishe!, ili tupate maendeleo ya kweli, lazima serikali ibadilike the way it does some things.

Dr. Rioba ameulizwa swali kuhusu TBC kufanya upendeleo kwa CCM na serikali

Hapa namuona Dr. Rioba akikumbwa na kigugumizi...
Akitolea mfano matangazo ya mkutano Mkuu wa CCM, amesema TBC inachokifanya ni kutanguliza tuu mbele kitu kinachoitwa Public Interest, hivyo TBC ndio ilikuwa ya mwisho kuamua kuutangaza mkutano wa CCM, hata hivyo amesema CCM imelipa!.

Amesema hata Chadema wakiomba TBC kuwatangazia mkutano wake Mkuu, TBC itawatangaza tuu ili mradi walipe.

Dr. Rioba atoboa siri kuwa TBC imekuwa ikiwaita viongozi wakuu wa vyama vya upinzani, kushiriki kwenye mijadala mbalimbali TBC, lakini wao ndio huwa hawatokei, wanaikimbia!.

Rioba amesema TBC inataka kufanya kazi na watu wote na vyama vyote bila ubaguzi, bila upendeleo.

Kuhusu tuhuma za TBC kuhonga watu ili kumsifia Magufuli, Dr. Rioba amekanusha vikali.
"Mimi ni muumini wa uhuru wa watu kujieleza, lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu, uhuru tunaoutumia kwenye mitandao, tuhuma za TBC kutoa rushwa ili kuandaa Kipindi cha kumsifia Magufuli"

TBC inaamini katika haki, hakuna rushwa kabisa katika TBC

Pia amezungumzia fake news, amekiri TBC kufanya kosa, kuhusu uwepo wa fake news, amesema amezama deep namna bora ya ku deal na fake news ni kuboresha mafunzo, amemshukuru mhe rais kuwasamehe wahusika wa fake news ya TBC, yeye aliishawafukuza jumla.

Amesema alikasirika kwa sababu TBC ndio taasisi yanye pool kubwa kabisa ya waandishi walioelimika kwa viwango vya juu, kabisa, wenye weledi, hivyo kwa mwaka 2017, TBC itaboresha Zaidi contents.

Pia Dr. Rioba amezungumzi TBC TaIfa, TBC FM na TBC international, TBC kuwa TBC itaendeleza dhima ya RTD, ameagiza magari 9, TBC itawafuata wananchi kule vijijini.

TBC pia itafanya kazi ya watchdog to the society, TBC kama chombo cha habari, ikifanya kazi yake ipasavyo, TBC itaisaidia sana serikali kubaini maeneo ya mapungufu kwa kuyaibua, sio kusubiri hadi rais, waziri Mkuu au serikali ndio ikaibue madudu.

Kumbe Dr. Rioba ndie Makamo raia wa Vyombo wa Utangazaji Kusini mwa Africa, SABA, uliochini ya SADC, hivyo amezungumzia umaajumui wa Afrika, kuwa TBC itashiriki.

Amemalizia kwa kusisitiza kuwa TBC inajipanga kujitegemea kwa kuzindua mpango kabambe. TBC kuwa na makao makuu Dodoma, kwa kuanzia itahamishia watumishi 15 Dodoma

Kipindi kimemalizika.

My Take.
  1. Kwanza Dr. Ayoub Rioba huyu aliyeongea leo, ndiye yule Ayoub Rioba tuliomfahamu sisi kama Ayoub Rioba, kabla hawajawa Mkurungenzi wa TBC, sijui ni nini kilimpata hapa katikati, lakini sasa huyu ndiye Ayoub tuliyemfamu ni mwandishi nguli, mbobebezi na mzalendo mwenye kutanguliza mbele maslahi ya Taifa na Watanzania, hivyo sasa Dr. Rioba anakwenda kui transform TBC kutoka kuwa ni TV ya serikali, Government TV Station na kuwa ni Public Broadcasting Station
  2. Kitendo cha kuipania TBC kujitegemea, ni cha kuungwa mkono kwa asilimia 100%, serikali iendelee kuigharimia TBC kama wajibu wake, lakini TBC ibuni vyanzo vingine vya mapato. Hii itaifanya TBC iwe independent, swali ni jee serikali itaikubalia TBC kuwa independent?. Kwa sababu the more TBC inavyojitegemea ndivyo serikali inavyo losse grip kwenye TBC!.
  3. Kwa vile Dr. Rioba amepania kuipaisha TBC kufikia levels za BBC, lazima set up na funding ya TBC iwe ki BBC, Tanzania tuanzishe broadcasting levy, TBC ipatiwe fungu lake linalojitegemea kwa kugharimiwa na umma, nakumbuki nikiwa UK, kila mtu anakatwa Fedha kuigharimia BBC, mimi nakalalamika kuwa nikiwa UK sitaangalia BBC, wala sitasikiliza BBC radio, nikaambiwa usikilize, usisikize as long as umechuma pesa in UK, lazima uligharimie BBC. Kama ilivyo kwa Fedha za SDL.
  4. Ili TBC iweze kuwa kama BBC kwenye programing, lazima sasa TBC ikubali kupokea Vipindi vya nje, kutoka kwa independent produces, hii ni fursa kwa production houses, ku produce good programs zenye maudhui mazuri na good quality kuitumia TBC kurusha diverse opinion.
  5. Kitendo cha Dr. Rioba kupania kuijengea uwezo TBC kuisaidia serikali kwa kuwa a watchdog to society kwa TBC kutosubiri hadi rais Magufuli afanye ziara za kushtukiza ndipo kuibua madudu, sasa TBC itapenya na kuibua madudu, serikali itafuatilia. Hii maana yake TBC sasa itakuwa na Vipindi vya Investigative Journalism, kama ilivyo kwa Jicho Pevu kule Kenya, hakuna TV yoyote Tanzania, inafanya investigative journalism program.
  6. Dr. Rioba amesema TBC haina upendeleo kwa CCM, itatenda haki kwa vyama vyote, kumbe vingozi wa upinzani huwa wanaalikwa TBC lakini wanaingia mitini!, mwaka 2018, tutegemee kuona more political programs zenye balanced representation.
  7. Kwa vile mimi ni mtu wa broadcast journalism, kuna mambo mengine ya TBC ni not for public consumption, hivyo nitamtafuta Dr. Rioba on one on one.
All the Best kwa TBC 2018.

Paskali
Live News Interactive!-TBC-1 Yastahili Pongezi!. ''Hongera TBC-1" Keep it Up!
Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma Ujumbe Gani kwa TV yake ya TBC?!.
Uchaguzi 2010: TBC1 are doing good job!
TBC Yafanya Kweli!, Yashusha OB Van ya Kufa Mtu!, Ina Kamera 12!. Itarusha HDV Signal Kama DSTV.
 
Kipindi nimekikutia katikati.

Amesema amepania kuipaisha TBC katika viwango vya kimataifa kama BBC.

P.
Kujifananisha na bibisii nadhani si sawa kabisa kimaudhui ila kwa ubora wa mitambo yao hapo sawa kujilinganisha. Tunaambiwa, bibisii ni moja ya MSM zenye madhui mengi ya kupotosha hadhira yake. Yaani ni fake wakati mwingine, hili tumelisikia kwa Trump.
====
Kama ni kwa ubora wa upatikanaji wa habiri zake kwenye runinga, simu, mitandaoni na kadhalika namtakia kila la heri Dr. Ryoba.
 
Akitolea mfano matangazo ya mkutano Mkuu wa CCM, amesema TBC inachokifanya ni kutanguliza tuu kitu kinachoitwa Public Interest, hivyo TBC ndio ilikuwa ya mwisho kuamua kuutangaza mkutano wa CCM, CCM imelipa.

Chadema wakiomba TBC itawatangaza.
 
Dr Rioba, amepigilia misumari kuwa ziko sharia, taratibu na kanuni za serikali lazima zinadilishwe, zinamuwekea usiku, kushindwa kufanya mambo kwa wakati. Ametolea mfano urasimu usio wa lazima katika baadhi ya maeneo, lazima serikali ibadilike the way it does things.

P.
Kama kaliona hili yuko sawa kila TBC wanahitaji fikra mpya has a ktk eneo la utayarishaji na uzalishaji,kila wakibaki na safari za Dodoma ,cjui chereko mmh
 
Anaweza kuwa na nia njema sana tu Dr Rioba..

My worry mabadiliko anayoyataka kuyafanya kiukweli pale TBC yanaweza kuwa very POSITIVE kwetu Wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa Taasisi hii ya Habari ya umma lakini yakawa so NEGATIVE kwa Watawala..

Atasalimika??

Hapo ndipo napokumbuka yaliyomkuta Nguli wa Habari Ndg Dunstan Tido Mhando alipokuwa Mkurugenzi hapo TBC.
 
Back
Top Bottom