DPP afanyiwa ukachero - INASHANGAZA SANA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DPP afanyiwa ukachero - INASHANGAZA SANA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mstahiki, Apr 23, 2009.

 1. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  2009-04-23 14:56:16
  Na Muhibu Said  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Elieza Feleshi, ambaye ofisi yake inashughulikia majalada ya kesi kubwa zinazohusu ufisadi, ukiwamo ule wa uchotaji wa mabilioni ya fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kompyuta yake imeibwa.

  Tukio la wizi huo linaonekana kama la kikachero, limefanywa na watu wasiojulikana kwa kuiba kompyuta yake ndogo anayoitumia kwa shughuli zake mbalimbali katika mazingira, ambayo hadi sasa bado ni kitendawili.

  Wizi huo unaonekana kama mikakati ya kusaka taarifa nyeti.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Suleiman Kova, alilithibitishia Nipashe jana kuibwa kwa kompyuta ya DPP Feleshi.

  Hata hivyo, alisema tukio hilo ni la muda mrefu bila kutaja muda huo na kuongeza kuwa hawezi kulizungumzia kwa vile hatua hiyo inaweza kuharibu upelelezi wa kuwanasa watuhumiwa.

  ``Hilo la kuibwa kompyuta ya DPP mbona ni la siku nyingi sana?

  Waandishi wengi leo (jana) wameniulizia, nikawaambia hivyo,`` alisema Kamanda Kova.

  Wakati Kamanda Kova akisema hayo, habari za kiuchunguzi, ambazo Nipashe imezipata zinaeleza hadi tunakwenda mitamboni jana, polisi walikuwa wameshawakamata watuhumiwa wawili wanaoshukiwa kuhusika na wizi wa kompyuta hiyo.

  Kati ya watuhumiwa hao, mmoja ametajwa kuwa ni mwanamke, ambaye alikamatwa baada ya askari polisi kuvamia nyumba moja iliyoko katika eneo la Sinza, jijini Dar es Salaam juzi asubuhi.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya mwenzake kumtaja.
  Alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo jana, Kamanda Kova kwanza alisema:

  ``Polisi huwa hawavamii, bali tunachokifanya hivi sasa ni kuendelea kuwatambua watuhumiwa wa wizi wa kompyuta hiyo ya DPP.``

  Hata hivyo, baadaye Kamanda Kova alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa licha ya kutakiwa na waandishi wa habari wengi afanye hivyo kwa vile hatua hiyo inaweza kuharibu upelelezi.

  Alisema amefikia uamuzi huo ili kuleta ufanisi katika operesheni ya kuwasaka na kuwanasa watuhumiwa wa wizi huo, ambao hadi sasa haijulikani sababu ya kufanya kitendo hicho.

  Feleshi alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo, hakupatikana na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokewa.

  Hadi sasa watu 22 wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika na uchotaji wa fedha za EPA, baada ya ofisi ya DPP kuridhika kwamba, wanastahili kushtakiwa mahakamani.

  Kesi hizo zinahusu makampuni 22 yaliyothibitika kujichotea fedha za EPA zaidi ya Sh bilioni 133 kifisadi.

  Kati ya makampuni hayo, Kagoda Agriculture Limited, ndiyo kinara wa wizi huo ikiwa imechota kiasi cha Dola za Marekani milioni 40.

  Hadi sasa suala la Kagoda limekuwa chungu kwa maofisa wote wa serikali kueleza kama wamiliki wake watafikishwa kortini au walau hatua ya upelelezi iliyofikiwa.

  Moja ya majalada ambayo DPP Feleshi anadaiwa kuyashughulikia ni pamoja na Kagoda, kampuni ambayo umma unasubiri kwa hamu kubwa kujua hatima yake katika ufisadi wa EPA.

  Mbali na Kagoda, majalada mengine ya kesi kubwa yaliyoshughulikiwa na ofisi ya DPP kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ni pamoja na la Kampuni ya Alex Sterwart, Kiwira na Richmond.

  DPP alikabidhiwa majalada yote ya makampuni yaliyotajwa kwenye ripoti ya uchunguzi wa EPA, na ni jukumu lake kufikishwa watuhumiwa wote mahakamani kulingana na ushahidi wa kesi zilizo mbele yake.

  Baadhi ya wadadisi wa mambo waliozungumza na Nipashe jana baada ya kusikia kwamba kompyuta ya DPP imeibwa, walieleza wasiwasi wao kwamba huenda kazi hiyo ni mkakati wa kifisadi wa kutafuta taarifa muhimu za kesi zinazowakabili.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahah, next you will see a govt building mysteriously burn down...etc etc.....this is like watching a really cheezy movie...
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa tutaambiwa kuwa DPP alikuwa anamalizia issue ya Kagoda lakini deal limiharibika so hana ushahidi tena na itakuwa tumeliwaaaa
   
 4. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahaaaaaaaa,

  haiwezekani.

  atafanyaje kazi bila kuwa na backup?
   
Loading...