Down town DSM

Safi sana kila Mtu mwenye kuweza kufungu Mgundi na Afungue tu.
 
Lipi hilo mkuu
Hao wafanyabiashara walitakiwa wawe na sehemu rasmi zakufanyia biashara zao na sio kuweka sehemu yoyote tu barabarani.

Kwanza inakuwa rahisi kwa serikali kukusanya kodi yake kwakuwa sehemu rasmi ya biashara inafahamika. Pili utunzaji wa mazingira kwa kuepusha kutupa taka hovyo. Tatu kama jiji ni fedheha kuona yanayoendelea maana mpaka mji ufikie kuwa jiji kuna mambo yanatakiwa kuachwa kufanyika.

Ubaya wakurugenzi wa majiji walijitahidi sana kupambana na hii hali lakini ikatoka kauli moja juu kuwa "waache wauzie wanapotaka". Ndio viongozi wetu hawa hawa wanatunga sheria na kuzivunja wewenye. This is Africa.
 
Tatizo kuu hapo ni viongozi, hawana ushirikiano na msimamo wa pamoja na hii yote ni mambo ya siasa. Wananchi wanajitafutia mkate ni jukumu la viongozi kuwashika mkono kwa kuwatengea sehemu maalum ambapo kunafikika kirahisi na wateja na sio tu just sehemu na kuwatelekeza huko.

Swala la usafi hapo ni tatzo, na kweli mji umechafuka na msongamano umeongezeka. Viongozi husika wawajibike kiufasaha.
 
Basi usijali kesho asubuhi ntampigia aliyeruhusu kufanya hivyo asitishe mara moja hilo zoezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…