Dowans: Political or technical issue? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans: Political or technical issue?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jan 29, 2011.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nadhani wasioelewa wanaweza kuongea hisia zao na wasiongee ukweli wa mambo, wakijaribu kuunganisha na maswala mengine hasa yale yanayohusu maisha binafsi.

  DOWANS ilikuwa kampuni na ilifanya kazi ya kuzalisha umeme kwa muda wa kuridhisha tu na tuliutumia umeme huo. Mkataba wao ambao tulipaswa kuuhoji mapema, kama ilivyo mikataba mingine huwa ina safeguards za kuepusha kampuni kupata hasara.

  Tatizo swala hili sasa ni la kisiasa na limebadilishwa kabisa kutoka technical issue kuwa political issue, wale wanaolitumia wanajaribu kukusanya wafuasi na wanaelekea kufanikiwa sana. Ninashawishika sana kusema kuna wanasiasa wanataka kuitumia nafasi hii kunufaika kisiasa, si jambo baya na si la ajabu, hatari yake ni upotoshaji wa ukweli wa mambo na kuzungumzia hoja. Hapa mimi hoja ya msingi ninayoiona ni Wingi wa fedha zinazopaswa kulipwa kulinganisha na uchumi duni tulionao, na kama serikali itakusudia kutolipa, wakati ilionyesha ina uwezo, natamani mahakama iamue fedha hizo zitengwe na zipelekwe kwenye huduma muhimu mfano kujenga na kuweka vifaa kwenye shule na zahanati kwenye maeneo yanayohitaji huduma hizo.

  Serikali inaweza kuwa na kiburi cha kutokulipa lakini serikali inayojali utawala wa kisheria ni lazima ifuate taratibu ili kujenga hoja ya kiburi hicho!
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mafisadi na watumishi wao wanajificha nyuma ya technicalities ili waendelee na uhaini wao. Hakuna politics hapa ni prevention of crime and being moral.
   
Loading...