Dowans- missing link | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans- missing link

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Mar 8, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu kimoja naona kinakosekana katika huu mjadala wa DOWANS. Kamati ya Mwakyembe ilishasema kuwa mkataba na DOWANS ni feki. Sasa hii kamati ya nishati inavyokutana kujadili jinsi ya kuirudisha na kuipa mkataba mpya DOWANS mbona haiongelei kabisa matokeo ya kamati ya Mwakyembe? Nafikiri kama kuna uamuzi wa kuipa mkataba mpya inabidi bunge na CCM wakubaliane kwamba utafiti uliofanywa na kina Mwakyembe haukutoa matokeo yenye ukweli. La sivyo, kujadiliana na DOWANS ni sawa na kujadiliana na mwizi aliyekuibia ili umpe mali zako akuchungie.

  Kwa kifupi naona kama bunge, CCM na kamati ya nishati wanajichanganya na mwisho wa siku wananchi tutakosa imani na kamati zinazoundwa na bunge kwa sababu matokeo yake yatakuwa hayana umuhimu na ni upotevu wa hela bure. Kama wanataka kuiwasha hiyo mitambo labda wachukue wazo la Mnyika la kuitaifisha, na watuhakikishie wananchi kwamba hakuna hela itakayolipwa kwa DOWANS kutokana na kuwashwa kwa mitambo hiyo. Otherwise watueleze wazi kuwa uchambuzi/utafiti uliofanywa na kamati ya Mwakyembe haukuwa makini.

  Naona kuna umuhimu wa kamati ya Mwakyembe kuhusishwa katika kila mjadala au hatua inayochukuliwa kuhusiana na DOWANS.

  Ni mtazamo tu.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mkataba ndio ulikuwa fake lakini Kampuni siyo fake
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kujadiliana na Dowans ni sawa na kufanya mazungumzo na majini ya Sheikh Yahya.. Dowans iliyosaini mkataba na Tanesco ni ya UAE, Dowans iliyoishitaki Tanesco kwa kuvunja mkataba ni ya Costa Rica, sasa kwa nini serikali yetu ijiingize kwenye biashara za kishetani namna hii?

  Je kuna ugumu gani kwa Tanesco kununua mitambo yao wenyewe badala ya hii ya kukodisha? Je serikali haiwezi kupata fedha za kuwapa Tanesco wanunue mitambo mpaka tulazimishwe kuingia mikataba na majini???
   
 4. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Na iweje akina mwakyembe wanyamaze au kukaa kimya na kutokuzungumza chochote kuhusu maoni ya kamati ya makamba jr?
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Usitudanganye, hakuna mahali kwenye kamati ya Mwakyembe ilisema mkataba wa Dowans ni feki, kama papo tuonyeshe.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Umekosea yote. Dowans iliyosaini mkataba ni Dowans Tanzania.
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unauhakika????
   
 8. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani mitambo ya DOWANS kununua ni bilioni ngapi?......mi nimelipwa leo nataka kumaliza hili tatizo kabisa, niinunue hiyo mitambo ya DOWANS halafu niwacharge wabongo TSHS 500 tu kutumia umeme.....tena nitakuwa naujaza kwenye kikombe....ukimwagia kwenye nyumba yako mara moja tu umeme haukatiki tenaaaaa!
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Kabisa tena
   
Loading...