"Dk. Slaa hana dhamira ya dhati ya kutaka CCM iondoke madarakani, kama yeye anaona kurudishwa NEC kwa akina Lowassa na Chenge ndiyo kifo cha CCM hakupaswa kusema hayo.
"Alipaswa kunyamaza ili waweze kuishughulikia CCM na mwisho wa siku Chadema ishinde uchaguzi iingie Ikulu, lakini kwa maneno hayo ni sawa na kuifungua macho CCM, hivi wakisimamisha mtu strong (anayekubalika) Chadema itapitia mlango gani kuingia Ikulu?.
Nilitarajia Dk Slaa angefurahia CCM kuanguka ili Chadema iingie Ikulu, lakini yeye anasikitika CCM inakufa.