Double Standards katika vita ya Ufisadi

Unakuwa na haraka kama haja la tumbo kuuma? Unataka Lowassa akamatwe leo? Mchezo huu hauhitaji hasira.
 
Lazima umdharau sababu kagusa chanzo cha wewe kwenda chooni.
 
Maoni yako ni mazuri lakini nadhani itakuwa ikisimamiwa na watu wanaojua mambo mengi kwa undani zaidi kuliko mimi na wewe ambao vyanzo vyetu vya habari ni vile vinavyotupa habari za juu juu tu. Yapo mengi watakayoanza nayo, wape muda wafanya ya kwao.
 
Nikiwa mwanajamiiforum mwenzako nimeona nikukumbushe juu ya kuweka akiba ya maneno. Usipende kumdharau sana mtu ambaye ana cheo cha amiri jeshi mkuu haswa kwa nchi kama yetu ambayo anakuwa na mamlaka makubwa. Hujui kesho ataamua kufanya nini.

Usisahau pia kuna maeneo hata amiri jeshi mkuu wa nchi kama yetu hana ubavu wa kutua. Kwa kuanzia, jiulize ilikuwaje JK akanywea kwa wauza ngada na majangili. Kama huyu akituthibitishia hakuna untouchables mbele yake basi tutakiri kuwa CCM si ileile. Bado sana kuona dalili hizo. Na kibaya zaidi tumeona dalili za mipasho kama ya JK zikianza. Hopefully, atapewa ushauri mzuri abakie kwenye kazi tu.
 
Huyu ni mchapakazi, na vita ya kupambana na watu waliozoea neema za bure bure sio ndogo, popote pale duniani. Wanaharakati walifikiri wanashughulika na JK, wakajua kuwa wakiongea watachukuliwa kidiplomasia halafu mambo yatakuwa yameisha, kumbe hali haipo hivyo, huyu JPM kaja kivingine.
Tumpe muda july 2016 sio mbali kutoka leo.
 
Double Stanndard ni kusema Magufuli alikuwa kwenye system inayofanya ufisadi miaka yote akiwa waziri halafu ushindwe kuwasema Mawaziri wakuu waliokuwa wakimuongoza kufanya ufisadi.Useme CCM kina damu ya kifisadi halafu ushindwe kuitambua damu hiyo na ukatae kumwita fisadi mtu aliye kiasisi chama na kuwa brain ya 'chama' kwa zaidi ya miaka sitini.Hakuna asiyejua kuwa CCM ni chama cha kifisadi na hakuna asiyejua vinara walioshiriki kujenga na kuimarisha ufisadi wa ccm ni akina nani. Muda huu ni wa kuwasaka mmoja baada ya mwingine popote walipo kutumia utaratibu wa kisheria kuwatia nguvuni wapate stahili yao. Acha kupaparika unapoona 'mwenye unaye mahaba nae' anazidi kusogelewa. Kwani muda gani toka Magufuli aingie madarakani mpaka useme double standards? Kazi ndio kwanza imeanza, subiri ukiambiwa imeisha ndo ulalamike.
 
Unakuwa na haraka kama haja la tumbo kuuma? Unataka Lowassa akamatwe leo? Mchezo huu hauhitaji hasira.
Hadi muda huu walio kwisha kamatwa ni 100% wote ni makada wa kutegemewa wa ccm
 
Maoni yako ni mazuri lakini nadhani itakuwa ikisimamiwa na watu wanaojua mambo mengi kwa undani zaidi kuliko mimi na wewe ambao vyanzo vyetu vya habari ni vile vinavyotupa habari za juu juu tu. Yapo mengi watakayoanza nayo, wape muda wafanya ya kwao.
Unajuwaje wewe?
 
Naiona ccm ikibakia jina kwenye vitabu,hasa kwenye majengo ya uhuru media maana ukiwagusa mafisadi wa nchi hii ndio hao hao wafadhili wakuu wa ccm hivyo ccm watakosa mfadhili na kufa kifo cha kawaida kabisa
 

Ndugu yangu ni kweli tumeona dalili za JPM kuwa mchapa kazi na ametupa matumaini kiasi chake. Lakini alivyowajibu HRLC haikuwa katika kiwango cha u-rais kabisa (not presidential at all). Ningependa asikilize na kusoma tena walichosema HRLC. Hawakupinga utumbuaji wa majipu. Walichoshauri ni utaratibu mzuri kufuatwa - unaolinda hata heshima ya rais.

Rais mwenyewe keshasema anachofanya kwa watendaji wa umma, ni kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi. Wakithibitika hawana tatizo watarudi kazini. Wakiwa na tatizo ndio bye bye. Sasa kuna heshima gani kwa rais kutangaza hadharani kuwa anamtumbua jipu mtu wa aina hiyo tena kimipasho: "wananchi nimtumbue nisimtumbue ...?"

Mimi ninayejali niliipatwa soni sana kwa vibwagizo vilivyotolewa darajani. Nikasikitika zaidi niliposikia kauli ya rais ya kuwatumbua "wanaompinga" - eti nao ni majipu! Halafu kibaya zaidi, zikasikika sauti kadhaa zikichochewa na media kuwalaani "wanaompinga rais kutumbua majipu!" Hata ITV ninayoiangalia sana niliipuuza kwa kujiunga na ujinga huo.

Rais anaweza kumuita Mama Bisimba na kumhoji alichomaanisha kutoa kauli alizotoa kwa niaba ya HRLC badala ya kuanzisha ligi ya majibizano mitaani. Who is Bisimba, by the way? Rais anaweza kumuita wakati wowote wakamaliza mambo inavyostahili. Tuache uswahili; tuanze kuwa watu wa maana na kumrejeshea rais wetu hadhi yake. Tumesoma shule kwa ajili hiyo.
 
Wawili kati ya uliowapongeza tayari, wawili watafuatia na wawili ndio watasalimika.
Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…