Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,071
UKAWA wameanza kampeni za urais rasmi huku Mawaziri wakuu wawili wa zamani walihama CCM na kujiunga na UKAWA, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wakipiga kampeni kwa pamoja katika jiji la Dar siku ya jana na kuendelea hivyo hivyo katika mkoa wa Iringa kwa siku ya Leo.
Mtindo huo wa kampeni uliopewa jina la "Double Impact" umepelekea kuvuruga kabisa kampeni za CCM na kujikuta wakiacha kunadi sera zao na kubakia kukachifu na kumwaga matusi ya nguoni.
Kwa mfano, siku ya leo katika kampeni za mgombea urais wa CCM huko mkoani Njombe, ilibidi apandishwe jukwaani Amon Mpanjo (Kada wa CCM, mwenye ulemavu wa macho) ili kutumika katika kujibu hoja za Sumaye na Lowassa walizozitoa jana Jangwani. Baadhi ya viongozi wa CCM wa mkoa wamekosoa tabia ya baadhi ya makada wa CCM kudandia majukwaa na kuropoka kwani inaharibu mwelekeo mzima wa hotuba ya mgombea wao wa urais, wabunge na madiwani kwa kuwa unafanya wasahau kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka huu.
Inadaiwa kuwa CCM wako mbioni kufanya kikao cha dharula ili kufanya mabadiliko katika timu ya kampeni ya Magufuli ikiwemo kuongeza baadhi ya makada wenye ushawishi zaidi. Kuna taarifa zinasema Benjamini Mkapa na Pinda wameombwa kuongozana na Magufuli katika baadhi ya mikoa ili kuongeza nguvu.