ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
ACT WAZALENDO YAPINGA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UCHAGUZI MKUU
Chama cha ACT Wazalendo kinapenda kuwajulisha wananchi wote wa Tanzania kuwa katika muktadha wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26, tumechambua kwa kina matumizi yaliyotengwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, na tunatoa msimamo wetu rasmi kwa umma.
Serikali imetenga takribani shilingi trilioni 1 kwa ajili ya uchaguzi mkuu, ambapo tayari shilingi bilioni 741.5 zimetumika, na kiasi cha bilioni 378.2 kimeelezwa kitatumika katika mwaka huu wa uchaguzi.
ACT Wazalendo tunasisitiza kuwa fedha hizi ni mali ya wananchi wa Tanzania – si mali ya CCM wala chama chochote cha siasa. Ni fedha za umma ambazo zinapaswa kutumika kuimarisha haki na demokrasia, si kuharibu mchakato wa uchaguzi kwa upendeleo au udhalimu wa kisiasa.
Tunakumbusha kuwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, zaidi ya shilingi bilioni 254.82 zilitumika na badala ya kuleta haki, zilishuhudiwa kuwezesha uporaji wa demokrasia. Hali hiyo ya kuvunjwa kwa misingi ya haki bado inaendelea hadi sasa.
Kwa mara nyingine tena, tunaingia kwenye uchaguzi bila matumaini ya kuona haki ikitendeka. Hata hivyo, ACT Wazalendo tumeamua kushiriki uchaguzi huu kwa ari ya mapambano ya kulinda kura na kudai haki ya kila Mtanzania.
Tunasisitiza kuwa hatutaki fedha zetu zitumike kuumiza wananchi wala kupora maamuzi yao. Tunataka uchaguzi huru, wa haki, na wenye uwanja sawa kwa vyama vyote vya siasa bila bughudha, vitisho wala udanganyifu.
Katika muktadha huu, ACT Wazalendo tunatamka bayana madai yetu sita ya msingi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025:
1. Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani kupitia mchakato wa usaili wa wazi, kama inavyotamkwa na sheria.
2. Wakurugenzi wa Halmashauri waondolewe kuwa wasimamizi wa uchaguzi, badala yake Tume iajiri wasimamizi huru wa uchaguzi na wasaidizi wao.
3. Mawakala wa vyama wapewe uhuru wa kufanya kazi bila bughudha, vizuizi wala vitisho.
4. Wagombea wote wa vyama vyote wapewe nafasi sawa bila kuenguliwa, ili wananchi wawe na fursa ya mwisho ya kufanya maamuzi.
5. Kura feki zipigwe marufuku, na fedha za umma zisihusishwe kabisa na uchapishaji wa kura batili.
6. Vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie mchakato wa uchaguzi, bali visaidie kulinda amani na haki kwa wote.
ACT Wazalendo tunatoa angalizo na onyo kali kwa Serikali: Isithubutu kutumia fedha za wananchi kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi si mali ya CCM, na matumizi ya bajeti hayapaswi kumpendelea yeyote bali kuhakikisha haki inatendeka kwa kila Mtanzania.
Tunawahimiza wananchi wote wa Tanzania kutumia hasira na manung’uniko yao dhidi ya mwenendo wa Serikali ya CCM kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura, na zaidi ya yote, kulinda kura zao kwa nguvu zote.
ACT Wazalendo tumejidhatiti kuongoza mapambano ya kidemokrasia, na tutaendelea kusimama imara dhidi ya kila aina ya ufisadi, udhalimu na unyanyasaji wa kisiasa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Tuungane kuikataa hila! Tuungane kupiga na kulinda kura!
Imetolewa na:
Abdallah Khamis
Afisa habari ACT Wazalendo
Dar es Salaam, Juni 21, 2025