Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Kama kuna vita ambayo nimekuwa nikiomba na kusugua magoti ianze, basi ni hii!
Amani haiji, ila kwa ncha ya upanga!
Punda haendi, ila kwa mjeledi!
Wakenya walishapita huku kitambo, hawacheki na fisadi, na wala hawangoji wapate Evidence kama mazuzu sisi tunavyodanganywa kwa peremende na lawalawa!
Yeyote anayeingia ktk vita hii, ana baraka zangu nyingi!
ndioMmmhh!!!
'Wewe ndie fisadi mkubwa sana kwa kutaka machafuko. Unatangaza vita? Unajuwa athari zake?
Serikali yenyewe ya CCM ni sera yake kupunguza msaada wa bajeti. Kwa hiyo hii petition itakuwa ni nzuri sana kusaidia kufika huko kwenye kujitegemea kwa bajeti yetu haraka iwezekanavyo. Hii itakuwa ni nzuri sana na itatufikisha pazuri sana kwa haraka sana. Mimi wa kwanza kuisaini hii.
Siku zote si vizuri kuwa omba omba. Na tumeona JMK alivyozishusha asilimia za utegemezi wa bajeti kutoka zilipokuwa kabla yake na mpaka sasa zipo chini na kila mwaka ataendelea kuzishusha mpaka tuwe tuna bajeti yetu mia kwa mia. Rejea hotuba ya kuzinduwa Bunge la 10.
kuna wadau wameanza kampeni "PETITION" ya kuzitaka nchi wafadhili kukata misaada kwa Tanzania kwa sabau za kifisadi za serikali ya kikwete. Mnaomba kusaini hiyo petition ili hawa mafisadi washike adabu.... wanaiona nchi kama yao, linki hiyo hapo
DONORS CUTTING FUNDING FOR TANZANIA