DONGO dhidi ya BUTIKU kwenye gazeti la Majira

Status
Not open for further replies.

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,196
WanaJF,
Jana kwa muda hatuwepo online sijui ni nini kilitokea nadhani ADMIN anaweza kutujulisha, i hope hatukuwa hacked. Lakini vilevile jana nilipokuwa napitia pages za tovuti ya mwananchi nilifurahishwa sana na makala ambayo ilimhusu Butiku. Ingawa mwandishi anaonesha kuwa target yake ni kumbomoa Butiku, lakini alionesha mengine ambayo baadhi ya wanaJF tulikuwa hatufahamu.
Lakini jambo lingine ambalo niliobserve ni lile ambalo Mwafrika wa kike amekuwa akilisema mara kwa mara, Media nyumbani imenunuliwa, imenunuliwa na chief of spin ambaye ananekana kama sasa ni Rais wetu by proxy, kitu ambacho ni tragegy kuliko hata tuhuma za rushwa. Ajabu leo nimeshindwa kuipata hiyo article, kama kuna member akiipata aweke hapa, wenye akili waichanganue. Ilikuwa na heading inayofanana na Kikwete ameachwa peke yake kwenye mapambano dhidi ya Rushwa- Butiku. Sina hakika kama nimekumbuka vizuri.
 
Nimeipata, ingawa mwandishi amejaribu kutimia ujanja sana kuonesha kama amebalance story yake, lakini ukweli ana lengo ovu.

Mapambano ya rushwa: Butiku asema JK katelekezwa

*Asema ni ajabu anapiga kelele peke yake
*Akataa kuzungumzia tuhuma zinazomkabili
*Asema ni vizuri watu waendelee kuzungumza

Na Joseph Kulangwa

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Nyerere Foundation), Bw. Joseph Butiku, amewataka wana CCM na wananchi wote wamsaidie Rais Jakaya Kikwete, kupambana na rushwa bila kutegemea sana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Bw. Butiku alisema hayo jana Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na gazeti hili juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa kuhusiana na hali ya kisiasa nchini na zile ambazo zimekuwa zikitolewa dhidi yake.

Alisema anasikitika kumwona Rais akipiga kelele za kupambana na rushwa mara nyingi na kuonekana kana kwamba ni vita yake peke yake na kusisitiza wananchi wamsaidie kwa sababu wanawajua wala rushwa.

"Nimesikia Mwenyekiti wangu wa CCM, Rais Kikwete, akipiga kelele za rushwa ndani ya chama na kuonya kuwa atakayeonekana akishiriki rushwa, basi PCCB (TAKUKURU) imkamate...kuna kitu amekiona na ndiyo sababu anapiga kelele.

"Hawa watu wanaweza kupatikana kama tukizungumza, tunafahamiana sisi, hata kama hatuna ushahidi, tuzungumze tunawajua, hakuna haja ya PCCB...tuangalie matendo yao na wananchi wawaseme na tuwaambie kwamba wamezidi, basi," alisema Bw. Butiku.

Alisisitiza kuwa TAKUKURU peke yake haiwezi, lakini "sisi wenyewe tunajuana kuliko TAKUKURU, tukipewa nafasi tukazungumza, tutawaumbua tu na tutakuwa tumemsaidia hata Mwenyekiti wetu kupambana na rushwa, hasa katika uchaguzi."

Kuhusu wafanyabiashara kuondoka CCM na kuanzisha chama chao, alisema yeye binafsi hana tatizo na wafanyabiashara au matajiri ndani ya chama, ila isipokuwa wakitumia vibaya nafasi zao hizo, hatakubaliana nao.

"Tajiri lazima afuate kanuni za chama hiki, ambacho ni cha waumini, asitumie utajiri wake kuongoza au kuyumbisha chama, kama watashindwa kufuata Katiba na kanuni za chama watoke wakaanzishe chama cha wafanyabiashara matajiri...hiki si chama cha rushwa.

"Tumefikaje huko mpaka Rais anapiga kelele hivi za kupambana na rushwa, wasimsumbue Rais wetu waondoke wakatafute chama chao huko," alisema Bw. Butiku na kusisaitiza kuwa CCM ni ya wakulima na wafanyakazi, lakini hawazuiwi kuzalisha kihalali na kutajirika, ili mradi wabakie ndani ya chama bila kukiathiri.

Tuhuma dhidi yake

Bw. Butiku ametuhumiwa kuwa ni muungaji mkono asiyeyumba na mpiga debe mkubwa wa kampeni za kisiasa za Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Dkt. Salim Ahmed Salim, lakini inadaiwa kuwa ndiye aliyeziba nafasi ya Dkt. Salim kuwa Rais wa Tanzania, baada ya kung'atuka kwa Mwalimu Nyerere.

Habari za tuhuma hizo zilidai kuwa Bw. Butiku, wakati huo akiwa Katibu wa Rais Nyerere, alimshauri Mwalimu kuwa Balozi Salim alikuwa hafai kuwa kiongozi wa Tanzania kwa kuwa hakuwa mwanachama wa chama cha ukombozi katika Zanzibar cha Afro-Shiraz (ASP).

Tuhuma zingine ni kwamba ndiye alishauri kusimamishwa kwa vita ya uhujumu uchumi, uamuzi ambao ulimkatisha tamaa aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Bw. Edward Sokoine, ambaye alikuwa anasimamia na kuendesha vita hivyo.

Habari hizo pia zilidai kuwa Bw. Butiku pamoja na kuwashutumu viongozi wa utawala uliopita wa Rais Benjamin Mkapa na wa sasa, kwa kushindwa kupambana na rushwa, amekuwa anaishi katika nyumba ya Serikali, kwa miaka 21 iliyopita, kinyume cha taratibu na bila kulipa kodi, pamoja na kwamba amekuwa si mtumishi wa Serikali katika kipindi hicho chote.

Imedaiwa vile vile, kuwa alikuwa ni Butiku huyo huyo ambaye katika miaka ya mwanzoni ya 1980 alianzisha mfumo wa utoaji vibali wakati wa uhaba wa kutisha wa bidhaa nchini, mfumo ambao ulichochea kwa kiasi kikubwa kukua na kuongezeka kwa rushwa nchini, ambayo kabla ya hapo, rushwa yake ilikuwa ndogo na ya chini zaidi kulinganisha na nchi nyingine za Afrika.

Kuhusu hatua ya kumzibia nafasi Dkt. Salim, habari zilidai kuwa wakati Mwalimu Nyerere anajiandaa kung'atuka kutoka uongozi wa nchi mwaka 1985, alifikia uamuzi kuwa Dkt. Salim, ambaye wakati huo alikuwa Waziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi aliyefaa na aliyekuwa na sifa za kumrithi katika urais wa Tanzania.

Tuhuma zingine ni kuwa alimshawishi Dkt. Salim kukubali kuwa Mwenyekiti wa Nyerere Foundation baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere, baada ya nafasi hiyo kushikiliwa kwa muda na mwanasiasa mwingine mkongwe nchini, Bw. Alnoor Kassum, ambaye alipata kushikilia nafasi nyingi za juu za uongozi, ukiwamo uwaziri katika wizara mbali mbali nchini.

Kwamba pia Butiku alikuwa miongoni mwa wanasiasa ambao walikuwa mstari wa mbele katika kumfanyia kampeni Dkt. Salim katika kinyang'anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM wa urais katika uchaguzi mkuu mwaka juzi.

"Hii ndiyo ajabu ya kweli kweli. Pengine tuseme ni unafiki kwa kiwango cha juu kabisa. Joseph Butiku alibadilika lini kutoka katika upinzani mkubwa wa Salim Ahmed Salim na ghafla kuwa shabiki wa mwanadiplomasia huyo mkongwe wa Tanzania, ama ni baada ya kuwa amekubali kuongoza Nyerere Foundation?," kilikaririwa chanzo cha habari hizo kikihoji.

Kuhusu vita dhidi ya uchumi, habari zilidai kuwa alimshauri Mwalimu kusitisha ghafla vita hivyo, kwa madai kuwa Waziri Mkuu Sokoine, alikuwa akiviendesha kwa uonevu.

Habari zilisema Butiku alitoa ushauri huo baada ya mfanyabiashara (jina tunalo) wa mjini Musoma ambaye ni rafiki yake mkubwa, kukamatwa katika vita hivyo.

"Sasa huyu ni mtu ambaye anaweza kujidai hadharani kuwa anapinga na kupigana vita ya rushwa? Mtu huyo alisimamisha vita ya kweli kweli ya kuokoa uchumi wa nchi hii. Dhahiri hiyo si tabia ya mpingaji wa kweli wa rushwa," kilikaririwa chanzo cha habari kilichokuwa serikalini miaka hiyo.

Juu ya vibali, habari zilidai kuwa katika nafasi yake ya Katibu wa Rais alianzisha mfumo wa utoaji vibali vya upatikanaji wa bidhaa adimu nchini, mfumo ambao ulikithirisha rushwa na kuikuza nchini katika hali ya dhiki kubwa kwa wananchi.

Kuhusu nyumba anamoishi Dar es Salaam, habari zilidai kuwa amekataa kutoka katika nyumba alimokuwa akiishi katika nafasi ya Katibu wa Rais, pamoja na kwamba aliondoka katika nafasi hiyo tangu mwaka 1986, miaka 21 iliyopita na hivyo kutoka katika utumishi wa Serikali.

Katika siku za karibuni, Bw. Butiku alijitokeza hadharani kuushutumu utawala uliopita wa Rais Mkapa kwa kushindwa kupambana na rushwa nchini na pia kudai kuwa kwa sababu hiyo, Rais Mkapa aliingiza madarakani Serikali ya sasa kwa njia za rushwa.

Pamoja na kwamba amekuwa akizungumza kama mwanasiasa katika siku za karibuni, ukweli ni kwamba Butiku hajapata kuwa kiongozi wa siasa na badala yake amekuwa mtumishi wa Serikali.

Majibu ya tuhuma

Kwa tuhuma hizo, Bw. Butiku hakutaka kuzizungumzia moja baada ya nyingine, ila akasema anafurahi kuwa Watanzania sasa wanazungumza na kuwa suala si kujibu tuhuma au kuzungumza watu bali ni kujadili hoja.

"Nashukuru na nafurahi sana kuwa Watanzania sasa tunazungumza, na vivyo hivyo nashukuru na kufurahi hata kwa yanayosemwa juu yangu, tuendelee kuzungumza, ni imani yangu kuwa mazungumzo haya yatatusaidia kuelewana katika mambo mbalimbali ya msingi hasa kuhusu Taifa letu," alisema.

Alisema katika mazungumzo hayo, Watanzania wataweza kufahamiana kwani watakuwapo wenye nia mbaya na wenye nia njema ambao si hasa wanaotakiwa katika jamii.

"Mazungumzo haya tuendelee nayo tu yatatusaidia kutambua wenye nia mbaya, ya makusudi, waongo, wanafiki, wafitini, wachonganishi...lakini ni muhimu yatusaidie kutambua kuwa miongoni mwetu watakuwamo hao.

"Yatatusaidia kuelewana na kutambua wale wasemao kweli na wajinga, niseme wapumbavu...lakini jambo kubwa ni kuvumiliana, mimi nitavumilia na nitapokea kila linalosemwa na kama si leo, kesho nitayatumia kusema jema zaidi kuliko ninalosema leo," alisema Bw. Butiku.

Alipoulizwa kama yuko tayari kujieleza mbele ya CCM kuhusiana na tuhuma alizokuwa akitoa kuhusu chama hicho kukosa mwelekeo, Bw. Butiku alisema yuko tayari kwa kuwa ni mwanachama na anazungumza yaliyo katika Katiba, kanuni za CCM, kanuni za uteuzi wa wagombea katika vyombo vya Dola, na ahadi za CCM katika Ilani yake.

"Mimi naamini katika vyote hivyo na ni mtiifu katika vyote hivyo na najua kuna uhakika wa ulinzi wa unachokisema na uhuru wa kujadili na wenzako unachokisema kuhusu mambo ya Taifa letu," alisema.

Akifafanua kuhusu rushwa, alisema maadam yeye ni Mtanzania na bado anaishi nchini hataacha kuzungumzia hali hiyo, na kusisitiza kuwa riushwa imekuwapo miaka nenda rudi jhata wakati wa Ukoloni.

Na kwamba imekuwapo hata katika awamu zote za uongozi nchini na hivyo ni vizuri Mtanzania halisi akaizungumzia nakuipoigia kelele ili iondoke.

"Sasa kama ilikuwapo enzi hizo mimi ni Katibu, na sasa inaendelea ninyamaze tu iendelee kutuumiza!," alishangaa Bw. Butiku.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom