Dongfeng-41: Kombora jipya la Jamhuri ya Watu wa China ni ujumbe tosha kwa Marekani na Urusi?

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,450
7,891
Salamu!

Ikiwa ni maadhimisho ya miaka 70 ya Kikomunisti ya Jamhuri ya Watu wa China (P.R.C.), moja ya matukio katika siku hii ni maonesho ya zana za kijeshi ama kivita likiwemo gwaride kubwa la kijeshi na uzinduzi wa silaha mpya.

Moja ya silaha hizo ni hili kombora jipya la masafa ya mbali ama kwa kitaalamu Intercontinental Ballistic Missile lijulikanalo kama Dongfeng-41 ama DF-41 ambalo kwa mujibu wa Jamhuri ya Watu wa China, ni kombora lenye uwezo wa kuifikia Marekani ndani ya dakika 30 na kinadharia, ni kombora lenye uwezo wa kusafiri kwa umbali wa kati ya kilometa 12,000 hadi kilometa 15,000, kiwango kinachotajwa kuwa ni kikubwa zaidi kuliko kombora lolote lile la masafa ya mbali duniani.

Mbali na hapo kombora hilo linatajwa kuwa na uwezo wa kubeba 'Payload' yenye silaha (Warheads) takribani 10 kwa wakati mmoja ama kwa kitaalamu MIRV yaani Multiple Independently Targetable Reentry Vehicle ambapo hulenga shabaha zaidi ya moja. Mfano, likifyatuliwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kabla tu ya kumaliza kiwango chake cha masafa (Range), hugawanyika na kila 'Warhead' huelekea kwenye shabaha yake kwa maana hiyo huongeza ufanisi kwa kushambulia eneo kubwa zaidi bila ya uhitaji wa kufyatua kombora jingine.

Kasi ya uendeshaji ni jambo la muhimu sana katika kombora lolote la masafa ya mbali duniani na kwa hili kombora la Dongfeng-41 lina kasi ya uendeshaji ya mpaka mara 25 zaidi ya kasi ya sauti hivyo kulifanya kuwa imara na kuweka ugumu zaidi wa kulizuia ama kulifanyia 'Interception' kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa makombora ya masafa ya mbali, mifumo ijulikanayo kama Anti-Ballistic Missile Systems.

Marekani na Urusi pia ni mataifa mengine yenye uwezo mkubwa sana kijeshi na pamoja na China, yote matatu yamekuwa katika ushindani mkubwa sana wa kijeshi na uundaji wa zana za kisasa zaidi za kivita.

Kwa upande wa Marekani, pia inamiliki aina kama hizi ya silaha hususani kombora hatari la masafa ya mbali linalofyatuliwa kutokea ardhini (Land-Based ICBM) maarufu kama Minuteman ambapo kwa sasa likijulikana kama LGM-30G Minuteman III lenye uwezo wa kupiga umbali wa hadi kilometa 13,000 kutokea mahali lilipofyatuliwa. LGM-30G Minuteman III ni toleo la 3 la kizazi cha Minuteman.

Licha ya uwepo wa Minuteman III, upo mpango wa kulistaafisha kombora hili na kuleta mabadiliko mapya ya makombora yaliyoboreshwa zaidi katika mpango ujulikanao kama Ground Based Strategic Deterrent Next Generation Nuclear ICBM, mpango utakaogharimu Dola za Kimarekani takribani Bilioni 86. Tayari kampuni kubwa za Kimarekani kama vile Boeing, Lockheed Martin, pamoja na Northrop Grumman zinashindania mkataba huo.

Kwa upande wa Urusi, inamiliki kombora hatari la masafa ya mbali lijulikanalo kama R-36M ama R-36M (SS-18 Satan) lenye uwezo mkubwa wa kusafiri kwa umbali wa kati ya kilometa 10,000 hadi kilometa 16,000 pia linatajwa kuwa kombora zito zaidi duniani. Kombora hili lipo katika matoleo 6 mbalimbali kuanzia Mod 1 hadi Mod 6 yenye sifa tofauti tofauti.

LGM-30G Minuteman III pamoja na R-36M (SS-18 Satan) ni vigogo wawili hatari katika anga za kiulinzi wa kinyuklia kwa muda mrefu tu lakini kwa ujio wa Dongfeng-41 pengine tunaweza kugeuza shingo zetu na macho yetu na kulitazama kombora hili kwa jicho la tatu kama moja ya kombora hatari sana ambalo laweza kuwa tishio kubwa kwa miamba miwili ya kijeshi, yaani Marekani na Urusi.

Je, Kombora jipya la Jamhuri ya Watu wa China 'Dongfeng-41' ni ujumbe tosha kwa Marekani na Urusi? Karibu kwa maoni yako!


PICHA:
1569917967676.png

1569922090332.png

Makombora ya Dongfeng-41 yakiwa katika magari maalumu. PICHA: The Sun.
 
Marekani ina kadiriwa kuwa na nuclear war heads 5500 ambazo ziko enriched mara 1000 ya zile za hiroshima na nagasaki izo ICBM zipo kwao miaka na miaka alafu unashindana. Hakuna mtu ana taka vita saivi kwenye dunia ya wastaarabu, labda umchokoze.
 
Hayo mambo ya gamboot ya kutishi na magwaride yalisha pitwa na wakati.
Kwanini mkuu unasema hivyo?

Maana kila taifa lina mifumo yake ya kiutawala na katika maswala ya kiulinzi, kiusalama (Modern Warfare) na kujihami, maonesho kama haya yanaweza kuwa ni njia mojawapo ya Deterrence ambao ndiyo msingi mkuu wa kuwa na Nuclear Weapons kwa sasa.
 
Back
Top Bottom