Dondoo ya leo

jabirj864

Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
9
Reaction score
13
Ilazimishe nafsi yako kuwa na furaha hata kama moyoni una maumivu. Mambo mengine yanayokusibu jaribu kuyapuuza usiyape nafasi yakakutawala akilini. Moyo ni kiungo kidogo sana ambacho kina kazi kubwa mwilini mwako kazi ambayo hukufanya wewe uwe hai.

Baada ya kupata matatizo kwa mfano kuwa na ugonjwa usiotibika, kupoteza mali, kusalitiwa kimapenzi, kuachwa na unayempenda au kupoteza chochote unachokipenda.

Kwanza kubaliana na tatizo ulilolipata kisha jisahaulishe tatizo hilo na usonge mbele. Amini kuwa sio lazima ukipate kile ambacho unakitaka na hata kama ungekuwa nacho ipo siku hutokua nacho. Na huyo aliyekipata ipo siku hatokuwa nacho na hata hicho ulichokikosa ipo siku hakitokuwepo.

Usijilaumu na kujihukumu wewe mwenyewe subiri vumilia kwa mazito yaliyokutokea. Ukiona njia imefungwa geuza urudi jifananishe na mwili wako kuvitoa vile visivyohitajika mwilini. Usijihukumu subiri uhukumiwe.

Japo moyo na nafsi vinauma lakini hairisha kufanya maamuzi magumu msubiri aliekuumba akuamulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nalo neno.

Hasa pale uliposema kukubaliana na lile linalotusibu. Kutokubaliana na kujishangaa (yaani kuwaza mimi kweli ndiyo naishi hivi. Au kweli ananisaliti mimi). Hiyo ni hali ya kawaida pale mambo yanapoenda tofauti. Lkn tusiruhusu hali hiyo idumu muda mrefu. Inaathiri sana. Inakuwa mzigo mzito sana kwetu.

Kutokukubaliana na hali ni tatizo zito kuliko tatizo lililo tokea. Mfano mtu kapoteza kazi na maisha yamebadilika, kutokukubaliana na hali linaweza kuwa tatizo kubwa kuliko tatizo la kupoteza kazi. Kutokukubaliana kunaathiri afya, mtazamo na hisia. Hata ukiona watu wanacheka unaanza kuhisi pengine wanakucheka. Wengine wanasema usipokuwa na hela hata inzi ukiwafukuza wanatudi tena wanafikiri wanacheza.

Hivyo hisia zinabadilika sana kwa mtu ukiwa na matatizo.
Kama ulivyosema cha msingi ni kumuomba Muumba akupe ujasiri na nguvu ya kuvumilia. Pia kutambua ya kuwa jambo lolote, linaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…