Donald Trump tangu utotoni na vituko vyake

Donald Trump tangu utotoni na vituko vyake

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,355
Reaction score
16,402
Tangu utotoni, Trump alikuwa mtundu na wazazi wake walimpeleka shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi mjini New York.

Baadaye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, kitivo cha elimu ya biashara mwaka wa 1968.
Alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha kadiri, viungani mwa new york.

Hata hivyo Donald Trump alikuwa na ndoto ya kufanya biashara nje ya makaazi ya Queens na Brooklyn.

Aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyowekwa na utawala wa Reagan miaka wa 1980.

Kuna tofauti kuhusu utajiri hasa wa Trump. Aliwahi kuambia tume ya uchaguzi kwamba anao utajiri wa kima cha dola bilioni 10. Hata hivyo jarida la Forbes limenadi kwamba utajiri wa Trump haufikii juu ya bola bilioni 4.5.
Lakini unapotembea barabara kuu za Manhattan, kampuni ya Trump imeweka mabawa yake kwa majumba ya kifahari yaliyofuatana.
Yapo mahoteli, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai nembo yake ikiwa ni Trump.

Ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking'aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, "The Apprentice," katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico.

Matusi


Licha ya kufanikiwa katika biashara, Trump pia amefeli kwenye hizo biashara na maisha. Kwa mara nne kati ya mwaka 1991 na 2009, miradi yake ya hoteli na majumba ya kamari ilitangazwa kufilisika.

Ndoa zake tatu zimevunjika, pia alikejeliwa kwenye vyombo vya habari kwa kudai kwamba cheti cha kuzaliwa cha Rais Barack Obama hakikua cha Marekani.

Wengi walimcheka alipotangaza nia yake kuwania urais wa Marekani.

Mambo muhimu kuhusu utawala wa Trump

Haijalishi matusi anayotoa, wafuasi wake wameendelea kusimama naye na kumpenda zaidi.
Aliwaita wahamiaji kutoka Mexico kama wabakaji, na kusema mtangazaji wa runinga ya Fox alimuuliza maswali magumu kwa sababu alikuwa anapata hedhi.

Alivutia habari kubwa za kimataifa baada ya kusema ataweka marufuku kwa Waislamu wote kuingia Marekani kwa muda.

Saa kadhaa kabla ya kushinda mchujo wa jimbo la Indiana, na kumshinda Cruz, alitoa madai kwamba babake Cruz alihusishwa na mtu aliyemuua Rais John F. Kennedy.

Licha ya haya yote, watu wengi wameendelea kuvutiwa na mwanasiasa huyu ambaye amesema ataweka ujuzi na mafanikio yake binafsi kuboresha hadhi ya nchi.
Aliwahi kuwa mwanachama wa Democratic, na pia akajiunga na upande wa kujitegemea.
Trump sasa amebadilisha msimamo wake wa kadri kuhusu umiliki wa silaha, utoaji wa mimba na kutetea msimamo mkali huku akiwapuuza wanachama wa Republican walio na msimamo wa kawaida kuhusu umiliki wa silaha, utoaji mimba Huku akiwakashifu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja

Huyu ndiye Donald Trump
FB_IMG_15288813807556847.jpg
 
Ukisoma Historia kwa undani ya Trump , basi jamaa mpaka hapo alipofika anahitaji pongezi Sana.

Bongo mtu akianguka kwa mtaji wa samaki basi hainuki tena ila jamaa alianguka akainuka akaja akaanguka tena akainuka.

Kwenye Kitabu chake cha "The Art of the Deal" anasema "Mwenye nia njema huwa hakati tamaa"
 
Ukisoma Historia kwa undani ya Trump , basi jamaa mpaka hapo alipofika anahitaji pongezi Sana.

Bongo mtu akianguka kwa mtaji wa samaki basi hainuki tena ila jamaa alianguka akainuka akaja akaanguka tena akainuka.

Kwenye Kitabu chake cha "The Art of the Deal" anasema "Mwenye nia njema huwa hakati tamaa"
Nimeitaja Hapo mkuu
 
Back
Top Bottom