Donald Trump sacks FBI Director Comey!

Donald Trump sacks FBI Director Comey!

Duu huyo acting FBI Director anatema madini huko si mchezo, Trump is in trouble aisee!
Inaonekana Trump anazidi kuumbuka na WH inazidi kuchanganyikiwa swali kubwa likiwa ni sababu zilizopelekea Comey kutimuliwa huku kila msemaji akinena ya kwake. Sijui kama kuna siku na hapa kwetu kamati za Bunge tutaziona live zikiwaweka kikaangoni wakuu wetu wa usalama na ulinzi kama tunavyoshuhudia kwa wenzetu...nadhani hilo hata ndotoni haliwezi kutokea...ha ha haa!
 
Trump kakalia kuti kavu manake naibu wa James Comey ameahidi kuendelea na uchunguzi dhidi ya uhusiano wa Trump na Russia
 
402B1EAF00000578-4492690-image-a-18_1494434389318.jpg


Trump cozy with the Russians in the Oval Office...only Russian press was allowed!​
 
WOW!

US President Donald Trump warns fired former FBI chief James Comey against leaking to media.

SOURCE: BBC
 
Ivi ilo kuti kavu huwa halivunjiki tu kila siku amekalia na atamaliza 4yrs mnaimba the same song


Na hili wingu la Russia halionekani kuondoka leo wala kesho. Hata akiwekwa huyo Independent prosecutor.
 
Haha, True. Trump has placed in a position where you can not plan on him. Period!
Let's wait and see, the moment I thought he couldn't make it he surprised me with great comeback, from thee I've no doubt this will also pass!
 
Let's wait and see, the moment I thought he couldn't make it he surprised me with great comeback, from thee I've no doubt this will also pass!


He is indeed, been that come back kid. We'll see.
 
Ivi ilo kuti kavu huwa halivunjiki tu kila siku amekalia na atamaliza 4yrs mnaimba the same song
marcus rojo, hatusemi ivi ilo kuti kavu, hicho si Kiswahuli, tunasema hivi hilo kuti kavu. Hilo ni moja, lakini la pili ni kwamba kwenye demokrasia zilizokomaa kama Marekani, watu hawakurupuki kama unavyodhani. Mambo huenda taratibu na hatua zinapokuja kuchukuliwa ni baada ya kujiridhisha Kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu hata kama inachukua zaidi ya mwaka moja. Hata mtu anayekamatwa red handed akifanya uhalifu, upelelezi lazima ufuate mkondo wa sheria na baadaye mtuhumiwa kufikishwa mahakamani na hukumu kutolewa.

Kwa swala la Trump kuna ugumu zaidi hata kama ana makosa ila kaa ukijua kama itathibitika kakiuka sheria na utaratibu, hakutakuwa na namna, sheria itachukua mkondo wake. Kinachofanyika sasa hivi ni kukusanya ushahidi usio na shaka kuhusu kuhusika kwake katika tuhuma zinazomkabili na mambo yatakapoiva, utawaona hata hao wanamtetea wakijiondoa taratibu. Yuko Gavana alituhumiwa kwa makosa ya kiutendaji na ilichukua zaidi ya miaka mitatu kutiwa hatiani na sasa yuko jela akitumikia kifungo baada ya makosa yake kuthibitishwa mahakamani.

Ni kweli Donald Trump kakalia kuti kavu na pamoja na nguvu zote alizo nazo Kikatiba kama Rais hawezi kuzuia upelelezi na mahojiano yanayoendelea katika Kamati za House na Senate. Katika muda huu ambao angetakiwa kukaa kimya, yeye anazidi tu kujiharabia kwa kutoa kauli za ajabu ajabu bila kujua madhara yake. Uzuri wa Marekani ni kwamba kila kauli (na tweet zake) zinawekwa kwenye kumbukumbu na kujadiliwa hadharani na watu wote...wanaomuamini dhidi ya wasiomuamini na bahati mbaya kwake asilimia zaidi ya 60% hawana imani naye tena.
 
Back
Top Bottom