Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Sio kila kinachotokea kwa binadamu hujulikana makusudio yake kwa haraka.Mwenyezi Mungu ana majeshi ya aina nyingi kuanzia vidudu visivyoonekana kwa macho kam vile virusi aina mbali mbali, Wako wadudu wadogo wadogo wasioshindikana kwa mabomu wala dawa kama vile nzi na mbu. Silaha za Mwenyezi Mungu zinaweza kuwa hata mtu mmoja tu kuwa na nguvu na balaa za kuangamiza wenzake wengi.
Nchi ya Marekani kwa kipindi kirefu imekuwa ikiitesa dunia vibaya sana kiasi kwamba nchi takriban zote wamekuwa wakiigopa na yenyewe imekuwa na kiburi sana kiasi kwamba kila jambo linalonong'onwa kwenye nchi nyengine lazima wajipenyeze kutaka kutoa hukumu,hii si sifa anayotakiwa kuwa nayo binadamu. Kwa upande mwengine watu wengi wanyonge wameumizwa na wengi kuuliwa na nchi hiyo haitaki kuchukua jukumu lolote la yale maovu yanayojifanyia.
Katika moja ya ahadi anazosisitiza Mungu kuwa hachoki kuzitekeleza wala kuzipuuza ni dua za mwenye kudhulumiwa.Raisi Donald Trump tangu aingie madarakani na ahadi yake ya kuiinua tena Marekani aliyoona yeye haijafanya zaidi ya pale ilipofanya badala yake amekuwa akiiporomoa nchi hiyo hatua kwa hatua mpaka baada ya miaka yake 4 inaonekana iko chini sana ya mataifa ambayo zamani yalikuwa dhaifu sana.
Katika kuzidi kuiporomoa nchi hiyo Trump yuko mbioni kuua mfumo wa kidemokrasia ya nchi hiyo na bado anaendelea kufanya madudu ya kuivunjia hadhi Marekani utadhani ikulu ya nchi hiyo imevamiwa na jeshi lisiloonekana linaloshambulia ndani kwa ndani.
Leo tunaweza kumzingatia Trump pekee lakini pia wapo marasi wa nchi nyengine tatu wanakuwa ni bakora ya kuzipiga nchi zao kwa kuzusha majanga yasiyokuwa ya lazima na kuingia kwenye mizozo ya kuzivunja nguvu nchi hizo.