Donald Trump aionya tena Korea Kaskazini

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Rais wa Marekani Donald Trump ameaonya kwa mara nyengine kwamba mzozo mkubwa utaibuka na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa kinyuklia na ule wa kutengeza makombora.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Reuters amesema kuwa angependelea mzozo huo kukabiliwa kidiplomasia lakini amesema hiyo itakuwa vigumu kuafikia.

Bwana Trump alimpongeza mwenzake wa China Xi Jinping akisema amekuwa akijaribu kwa kila njia kuishinikiza Korea Kaskazini.

Awali waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alisema China imeionya Pyongyang kutarajia vikwazo iwapo itafanya majaribio mengine ya kinyuklia.

Wakati huohuo Korea Kaskazini imetoa kanda ya video ya propaganda ikionyesha itakavyoishambulia Marekani.

Kanda hiyo inashirikisha ikulu ya Whitehouse na ndege ya kubeba ndege za kijeshi inayokabiliwa na inakamilika na ikulu hiyo ikilipuka.
 
Mchina si mtu wa kumuamini... always mchina anaangalia maslahi yako wapi maana yeye ni mfanya biashara.
Soon NK atajikuta yuko mwenyewe huku wanaodaiwa kuwa washirika wake wakimwacha mwenyewe
 
f41821f52d76c263fcf9b6e574b75cd9.jpg
 
Mchina si mtu wa kumuamini... always mchina anaangalia maslahi yako wapi maana yeye ni mfanya biashara.
Soon NK atajikuta yuko mwenyewe huku wanaodaiwa kuwa washirika wake wakimwacha mwenyewe
China inapinga marekani kuweka military base yake Korea Kusini na inachukulia mgogoro wa Korea kama mbinu ya kuidhoofisha. Marekani imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha majimbo ya Tibet na Taiwan yajitenge kutoka China na kuchochea mgogoro wa kugombea kisiwa cha Senkaku katika ya China na Japan.
 
Dunia naona inategeneza balance of power tuanze kurudi kwenye NAM tena
 
rais wa twilla ( twitter), majigambo kibao, marekani anajua hasara na maafa yatakayojitokeza iwapo vita zitaanza
 
Nilikuwa najuwa Trump ni mtu wa maamuzi magumu kumbe na yeye muimba taarabu
Trump ni mtu wa Mungu sana yule baba Hawezi kuangamiza wananchi wasio na hatia ,apo Nadhani analia timing kiduku akiweza amalize mwenyewe ila km unasubiri trump amuuru kombora kurushwa na kuua jamii kubwa isiyo na hatia utasubiri sana Mzeee hilo Hawezi hata kdg .
 
Mwambieni huyo Trump avue hilo wigi limefunika akili zake mbona amekalia mipasho tu hachukui maamuzi sahihi alishaambiwa N korea siyo Waarabu akae akijua hilo
 
China inapinga marekani kuweka military base yake Korea Kusini na inachukulia mgogoro wa Korea kama mbinu ya kuidhoofisha. Marekani imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha majimbo ya Tibet na Taiwan yajitenge kutoka China na kuchochea mgogoro wa kugombea kisiwa cha Senkaku katika ya China na Japan.
Juzi china na america marais wao wamekutana. Walichoongea uko wanajua wenyewe ... mchina hatetei north korea. Anakaa neutral.. si barid si moto. Si mtu wa kumuamini
 
kuna watu humu nawaona huwa wanatokwa povu wakitetea NK na marekani lkn hayo yote ni maneno tu ila muda ndio utaongea,kama ni kupigana wapigane mapigano ndo yataamua nani mbabe
 
Mbona kiduku anatoa mipasho ya kufa mtu lakin ahafanyi kitu?
Ni lini kiduku alitishia atamvamia USA kijeshi.USA ndio kiherehere Mara aweke vikwazo Mara nitawashambulia

Kiduku yupo wazi mimi natengeneza silaha kujilinda sababu nazungukwa na maadui ,nikiguswa nitajitetea

Hajasema atamvamia mtu bila ya sababu yeyote..lkn huyo kimbelembele chenu Trump Mara apeleke nyambizi,meli,Navy seals

Sasa kati ya Trump na kiduku nani ana mipasho hapo

Kiduku ni kama mwanaume ambaye anajifañyia zake mazoezi hataki Shari na mtu ,Trump ni kama mwanaume ambaye Mara avue t shirt ,Mara avue viatu mikwara kibao ila vitendo 0 lakini kiduku yupo calm eneo lake tu
 
Siyo kirahisi hivyo Nk anaongeza usalama wachina
NK anawalinda wachina.... kaka umedanganya... sana.
China wana nuclear weapon, wana airforce kubwa... wana technology bila kusahau maendeleo.
baadhi ya ndege anazotumia NK chengdu J-7 na J-6 hizi zimekuwa modified na mchina.

Nk hana uchumi... mkubwa kama wa china.
Nk hana technology aliyonayo mchina..

Kwa kauli yako ni sawa sawa na kisiwa cha mafya kilinde Tanzania bara...? Ndoto za mchana
 
Juzi china na america marais wao wamekutana. Walichoongea uko wanajua wenyewe ... mchina hatetei north korea. Anakaa neutral.. si barid si moto. Si mtu wa kumuamini
Hiyo ndio diplomasia mkuu, hata Bongo unaweza kudhani ni rafiki wa kila nchi ndani ya Afrika Mashariki kumbe ni diplomasia tu ndo inakufanya uone hivyo lakini mambo mengine kama ya usalama hayana cha urafiki.
 
NK anawalinda wachina.... kaka umedanganya... sana.
China wana nuclear weapon, wana airforce kubwa... wana technology bila kusahau maendeleo.
baadhi ya ndege anazotumia NK chengdu J-7 na J-6 hizi zimekuwa modified na mchina.

Nk hana uchumi... mkubwa kama wa china.
Nk hana technology aliyonayo mchina..

Kwa kauli yako ni sawa sawa na kisiwa cha mafya kilinde Tanzania bara...? Ndoto za mchana
Mkuu ndenda taratibu utagundua Nk yupo anaishi kwa ajili ya china anafanya kazi ya china ni mtoto wa mchina anaisumbua marekani na mataifa mengine kwa nguvu ya china siyo kila jambo unaweza elezwa ukaelewa mkuu pengine ninaifahamu china kiasi kikubwa kuliko wewe !!!
Baada ya miaka 3 ijayo Technology ya north ambayo ni ya china itakushangaza wewe na mataifa yote ulimwenguni !!! Mkuu kuna mambo mengi sana hujuwi uomb mungu atupe umri mrefu utajuwa mengi marekani hana lolote bila wizi ata sisi tungekuwa tuna wapa kazi sema walituwahi wakatumaliza hatuwezi fufuka tena ila kwa Asia haswa (china) wamechelewa meli imesha ngoa nanga mungu ni mwema!
 
Back
Top Bottom