Donald Trump aikosoa NATO, ataka ifumuliwe

Donald Trump aikosoa NATO, ataka ifumuliwe

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,584
Reaction score
28,739
Mmoja wa wagombea wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amesema muungano wa kijeshi wa NATO umepitwa na wakati na amependekeza ufanyiwe mageuzi.

Trump pia amesema jumuiya ya NATO yenye nchi 28 wanachama iliundwa wakati wa enzi tofauti wakati kitisho kikubwa kwa nchi za magharibi kilikuwa ni muungano wa zamani wa Sovieti. "NATO haina uwezo wa kupambana na ugaidi na inaigharimu Marekani fedha nyingi mno," akaongeza kusema mgombea huyo.

Kauli hiyo ameitoa siku chache kabla kufanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa dunia mjini Washington kuhusu usalama wa silaha za nyuklia. Rais wa Marakani Barack Obama atauandaa mkutano huo siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii utakaowaleta pamoja wajumbe 56. Huku mkutano huo ukitarajiwa kujikita katika kutafuta njia za kuepusha mashambulizi ya kigaidi dhidi ya vituo vya nykulia, mapendekezo ya Trump huenda yakajadiliwa pia, hususan pembezoni mwa mkutano. Urusi haitahudhuria mkutano wa mjini Washington, lakini rais wa China, Xi Jinping atahudhuria.

Machi 21 mwaka huu Trump alisema Marekani inatakiwa ipunguze ufadhili wake kifedha kwa NATO, iliyoundwa mwaka 1949 baada ya vita vikuu vya pili vya dunia na kuwa ukuta wa ulinzi dhidi ya utanuzi wa muungano wa Sovieti.

Mgombea hasimu wa Trump kwa uteuzi wa chama cha Republican seneta wa jimbo la Texas, Ted Cruz, aliyaeleza maoni ya Trump kuhusu NATO kuwa ya kipuuzi. Cruz alisema kuliacha bara la Ulaya, kujiondoa kutoka kwa muungano uliofanikiwa zaidi katika nyakati za sasa, hakuna maana yoyote, akiongeza kuwa kufanya hivyo kutampa ushindi mkubwa rais wa Urusi, Vladimir Putin, na kundi la Dola la Kiislamu IS.

Katika hatua nyingine inayoondokana kabisa na sera ya kihistoria ya Marekani, Trump alisema katika mahojiano yaliyochapishwa jana na gazeti la New York Times kwamba atazingatia kuiachia Japan na Korea Kusini zitengeneze silaha zao za nyuklia, badala ya kuitegemea Marekani izilinde kutokana na kitisho cha Korea Kaskazini na China.

Trump kuziruhusu Japan na Korea Kusini kwa na nyuklia

Katika mahojiano hayo Trump alisema atakuwa tayari kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Japan na Korea Kusini mpaka nchi hizo mbili zilipe fedha zaidi kuwahudumia na kuwalisha. Marekani ina wanajeshi 50,000 nchini Japan na wengine 28,500 nchini Korea Kusini.

Waziri kiongozi wa Japan, Yoshihide Suga, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari leo mjini Tokyo kwamba hakujafanyika mageuzi ya sera ya Japan ya kutojenga, kumiliki au kuanzisha silaha za nyuklia na akasisitiza bila kujali nani atakayekuwa rais wa Marekani, uhusiano kati ya Marekani na Japan utaendelea kubakia kuwa msingi imara wa diplomasia ya Japan na muhimu kwa uthabiti wa kanda hiyo na dunia kwa ujumla.

Trump, mfanyabiashara bilionea kutoka New York anayetaka ateuliwe na chama chake cha Republican kugombea urais wa Marekani katika uchaguzi wa Novemba 8 pia alisema huenda akasitisha ununuzi wa mafuta kutoka kwa Saudi Arabia na mataifa mengine ya kiarabu yaliyo washirika wake hadi pale yatakapotoa wanajeshi wa ardhini kupambana na kundi la dola la kiislamu au yailipe Marekani kwa kufanya hivyo.

Source: DW
 
Trump akili mingi sana,huyo Cruz anafaa kuwa mjumbe wa sherehe labda,dunia imebadilika inahitaji Sera mpya,Sera za ubabe zimepitwa na wakati,wenye IQ chini ya kumi percent hatuwezi elewa hili
 
Trump akili mingi sana,huyo Cruz anafaa kuwa mjumbe wa sherehe labda,dunia imebadilika inahitaji Sera mpya,Sera za ubabe zimepitwa na wakati,wenye IQ chini ya kumi percent hatuwezi elewa hili

Kaka wala hujakosea; jamaa ni kichwa balaa. Mavitegauchumi yake yanaonesha ni kichwa cha aina gani: http://www.trump.com/. Wengine watakashifu ni urithi; kiukweli aliikuta kampuni ya mzee wake inasuasua lakini leo ni kampuni la kimataifa baada ya kuwekeza brain yake pale. Wengine wangepewa kianzio sana sana wangeishia kwenda ku.t.mb.e.a. na biashara ingeishia hapo.
 
Huyu jamaa alikosea tu pale alipotamka yale maneno kuhusu waislamu na waafrika..hapo ndipo hakutumia uungwana.....lkn mambo mengine yupo right
 
Trump is a business man, he does everything in a 'business mindset'
  • Mexico will pay for the wall he wants to build
  • Ataingilia mahusiano ya biashara btn America and the rising China, and of course, to benefit America more. (smart idea)
  • New one...middle east countries walipe Marekani for American forces to be there...wow!
Pengine third world countries will have to 'BUY' misaada if he's elected POTUS.

Question is, will this work for him or for American foreign policy in general?!
 
Atakatwa na republican au watamuacha agombee? Tusubiri tuone.
 
Kaka wala hujakosea; jamaa ni kichwa balaa. Mavitegauchumi yake yanaonesha ni kichwa cha aina gani: http://www.trump.com/. Wengine watakashifu ni urithi; kiukweli aliikuta kampuni ya mzee wake inasuasua lakini leo ni kampuni la kimataifa baada ya kuwekeza brain yake pale. Wengine wangepewa kianzio sana sana wangeishia kwenda ku.t.mb.e.a. na biashara ingeishia hapo.
Ni vema ukaangalia pia habari zake kutoka kwenye tovuti nyingine. Kwa sababu hapo kwenye website yake, hawezi kusema lolote la matatizo yake ya bankruptcy, scandals zake, na matusi anayomwaga pande zote. Usimshabikie tu kwa sababu ya habari moja tu. Fuatilia habari kwa makini ujue utapeli wa bilionea huyo. Hebu msikilize huyu bwana John Oliver. John Oliver finally destroys "serial liar" Donald Trump and it's brutally fantastic
 
Trump is the only right choice for current America and the world!. He sees what others can not see, he looks beyond where no one has ever tried to imagine. Hawa kina Clinton na wengine wanaogelea mle mle ambamo pamefanya dunia iwayewaye kama machela na bado hawana hata chembe ya suluhu zaidi ya mazoea. Hawana jipya lolote zaidi ya kuendeleza mzungoko wa itiakdi na filosofia zile zile zinazopambana ili kuendelea kupumua. Hawana jipya. Trump atapingwa na watu wenye affiliations na upumbavu unaoharibu dunia, wanufaika wa udhaifu wa mifumo ya sasa ama wajinga wanaoishi kwa kukariri wasiokubali kwenda nje ya sanduku.

Trump for the World of Visionaries !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jiwekee akiba ya kutaka kujua kabla hujamwaga matusi yasiyo na sababu. Did it ever occur to you kwamba watu wanaomkataa wanaweza kuwa wanamjua zaidi kuliko wewe uliyemjua juzi tu kwa kusikia habari za vijiweni? Angalia polls za Marekani uone wanamwangaliaje. Kuwa makini unapopata habari na uziangalie critically. Ni kitu gani ambacho Trump amekisema au kukifanya kinachokuonesha kwamba yeye ndiyo uchaguzi mzuri kwa dunia? The man is so ignorant of the world, hata sijui kama anajua hata kwamba kuna nchi inaitwa Tanzania.
Nakiri kwamba akina Clinton wata-recycle mambo yale yale. Lakini kwa uelewa wa mambo na uwezo wa kuendesha nchi, Clinton anamtupa Trump kwa mbali sana. Angalia historia ya failure zake.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom