Domo zege disease tukutane hapa

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,580
48,729
Kuna wanaume kweli hawajui kutongoza

Kuna jamaa alikuwa ananionesha kabisa ananitaka ila ile kusema abc naona kama anakuwa muoga

Zikapita siku nyingi siku moja akaniambia wikend tutoke kuna jambo anataka kuniambia.Tukaenda mahali nikapiga msosi wa maana kama elf 70 hivi, ile bufee haikuwa ya nchi hii nilishinda pale masaa matatu nakula tu.

Baada ya kushiba nikamuuliaza ulikuwa unasemaje mkuu eti akaniambia alitaka kuniuliza nywele zangu nimesuka wapi na huo mtindo unaitwaje? hadi leo huwa namcheka sana. Nataka nimtongoze ndo namalizia kufanya upelelezi wangu wa mwisho kama anafaa kwa matumizi ya binadamu.

Wanaume mnachoogopa ni nini? Ningekuwa mwanaume mimi pasingetosha
 
kwahiyo mpaka sasa hajasema anakupenda basi atakuwa domo zege huyo .
 
Kama kweli na wewe ulimpenda na unajua ni domo zege (anakupenda Ila anashindwa kukwambia) kwanini usingemharakishie kazi? Kinyume na hapo kama ulikuwa humpendi hakukuwa na haja ya yeye kuundoa udomo zege wake kama unajua fika angekwambia ombi lake ungemkatalia.
 
hata mleta thred ni domo zege

kwa nini baada ya miaka mingi anakununulia msosi na wewe unazubaazubaa unasubirisubiri umchunguzechunguze?
 
Kuna wanaume kweli hawajui kutongoza

Kuna jamaa alikuwa ananionesha kabisa ananitaka ila ile kusema abc naona kama anakuwa muoga

Zikapita siku nyingi siku moja akaniambia wikend tutoke kuna jambo anataka kuniambia.Tukaenda mahali nikapiga msosi wa maana kama elf 70 hivi, ile bufee haikuwa ya nchi hii nilishinda pale masaa matatu nakula tu.

Baada ya kushiba nikamuuliaza ulikuwa unasemaje mkuu eti akaniambia alitaka kuniuliza nywele zangu nimesuka wapi na huo mtindo unaitwaje? hadi leo huwa namcheka sana. Nataka nimtongoze ndo namalizia kufanya upelelezi wangu wa mwisho kama anafaa kwa matumizi ya binadamu.

Wanaume mnachoogopa ni nini? Ningekuwa mwanaume mimi pasingetosha
unasema tu....kutongiza kazi sana
 
Kwanza kutongoza ni sanaa...

Wanaume tupo tofauti tofauti sana kwenye mambo haya....

Wanawake wenyewe wanasema kwamba kuna wanaume wengine sauti yao tu tayari analegea,wengine wanasema unapoonana naye tu au kutoka naye out,ile namna yao ya kumsikiliza mwanamke na kumjali wakati wa out mwanamke anajikuta tu mwenyewe anajipeleka machinjioni...

Wanawake wanasema kwamba kuna wanaume wanajua sana kupangilia maneno ya kumueleza mwanamke na anajikuta tu anashindwa kukataa maana yale maneno yanakuja huku yanadondosha asali na anajikuta anayabugia mazima mazima na akija kustuka keshamalizwa....

Kwa maana hiyo usimcheke huyo huenda ameshajifunza kutokana na makosa na akaona hiyo ndiyo njia bora ya kukutongoza maana tayari ushamuelewa na kwa namna nyingine keshakutongoza tayari....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom