Dokta Khalid funika kombe mwanaharamu apite

Calipso

JF-Expert Member
Mar 25, 2009
284
15
DOKTA KHALID FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE

Na mwandishi Wetu

Katika hali isiyo ya kawaida, Wizara ya fedha Zanzibar imegundua wizi wa fedha zaidi ya milioni mia tano (500m) uliofanywa na baadhi ya wahasibu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa utaratibu maalumu. Inadaiwa kwamba mtandao wa siri wa wizi wa wahasibu wa SMZ unahusika na ubadhirifu huo.

WATENDAJI 12 wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali wamesimamishwa kazi kutokana na upotevu mkubwa wa fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa juzi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Salum Mohamed, alisema kati ya watendaji hao wamo wahasibu wakuu wa wizara sita wanaohusika na upotevu huo wa fedha.

“Kwa masikitiko makubwa naomba kutoa taarifa kuwa tumebaini upotevu wa fedha za serikali ambao tumeanza kuuchukulia hatua,” alisema waziri huyo.

Alisema upotevu huo wa fedha unaonekana sio wa bahati mbaya, bali ni jambo la kupangwa na umetekelezwa kwa njama za watendaji wa vitengo vya fedha uliowahusisha wahasibu.

Aidha, alisema hadi sasa kuna hundi zenye thamani ya Sh. milioni 571 zimeshindwa kulipwa kwa sababu ya uhalifu huo na hatua za awali za kutathmini upotevu huo zinaonyesha kuwa kiasi ambacho kinahusika na wizi huo kinaweza kuwa kikubwa zaidi ya hicho.


“Tulipopata taarifa za awali juu ya upotevu huu hatua za haraka zilichukuliwa na kubaini wahusika wakuu” alisema Dk. Khalid.

Alisema taarifa za awali zinaonyesha upotevu huo wa fedha umetokana na njama za baadhi ya watendaji wa kitengo cha malipo katika Wizara ya Fedha na Mipango wakishirikiana na baadhi ya wahasibu wa wizara tofauti za serikali.

Waziri huyo alisema hatua hiyo imezingatia matakwa ya Sheria ya Fedha za Umma namba 12 ya mwaka 2005 na kanuni zake na Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2014 na kanuni zake.



WATENDAJI 12 WAMJIA JUU DOKTA KHALID

Baada ya tangazo la kusimamishwa kazi, Watendaji 12 wa serikali ya Zanzibar wakiongozwa na Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali wameeleza wazi kwamba kama Dokta Khalid amemwaga mboga na wao watamwaga ugali kwa kile wanachodai kwamba wamevishwa ngozi na kuadhibiwa huku walaji halisi wa nyama wameachwa. Chanzo nyeti kutoka wizara ya fedha kimedokeza.


Kwa mujibu wa Sheria na Kanuzi zinazoongoza miamala ya fedha, wahusika wakuu na wasimamizi wa fedha za Serikali ni Makatibu Wakuu wa wizara si wahasibu, na kwamba kwa mujibu wa kanuni na sheria za fedha Wahasibu hufuata maagizo wanayopewa na makatibu wakuu; jambo linaloonesha wazi kuwa wizi wa aina yoyote unaofanywa na wahasibu ni lazima utawahusisha makatibu wakuu na mawaziri.


Dokta Khalid amekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kwa zaidi ya miaka mitano akiongoza ubadhirifu mkubwa wa fedha za ofisi hiyo ambao haujawahi kutokea wala kuripotiwa katika historia ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


“…..Hivi Dokta Khalid unamdanganya nani? Kwa faida ya nani? Kwanini huwaambii ukweli wananchi wa Zanzibar kwamba SMZ inaendeshwa na mtandao wa watu wane kusimamia na kutumia hazina ya nchi? Mtandao huo ukiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee, Khamis Mussa, Omar Hassan King na wewe mwenyewe ambao kwa sasa umekufanyeni kuwa mamilionea kwa ufisadi wa fedha za Serikali” Alisema mmoja wa wahasibu waliosimamishwa kazi.


“…..ubadhirifu wako Dokta Khalid umekufanya wewe hivi sasa kumiliki zaidi nyumba 12 za kifakhari pamoja na mashamba makubwa mbali miradi mbali mbali ya gharama uliofungua, rafiki yako Abdulhamid Yahya Mzee anaongoza kwa kumilki miradi mikubwa na mahoteli lukuki ambayo baadhi inaendeshwa kwa ubiya kwa kushirikiana na bosi wake ambae lazima apate angalau asilimia 10% katika kila wizi mnaofanya…..” aliendelea kudadavua.


“ ….. waeleze wananchi utajiri wa Khamis Mussa anaemiliki zaidi ya ndege tatu na ofisi za ndege mbali mbali, mahoteli na majumba ya kifakhari zaidi ya nane Zanzibar na Dareslam ambayo baadhi amekodisha. Omar Hassan King anamiliki shule za Glorious Academy zilizopo Mpendae na Mombasa, mahoteli na kadhalika…..”


“…. Waeleze waandishi wa habari juu ya ubadhirifu wa fedha wa mamilioni ya Dola za kimarekani za maafa ya MV SPICE? wachambulie watu fedha za mfuko wa wafadhili za uchaguzi wa marejeo zaidi ya Bilioni 7 zilizopelekwa kwa mabegi kwa Makamo wa Pili, zaidi ya Bilioni 3 mkagawana mafungu wewe Dokta Khalid amepewa ngapi? Twambie kuhusu yale mamilioni mliyohonga mahakama kuu ya Zanzibar, Ofisi ya Jaji Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ili kubadilisha matokeo ya kura za wazanzibari...”


Dokta Khalid na timu yako tunakukumbusheni mtu mzima akivuliwa nguo huchutama, na mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba, tuko tayari kueleza uchafu wenu, hatatukubali kudhalilishwa peke yetu.


SENT AS RECEIVED
 

Attachments

  • WhatsApp-Image-20160704.jpeg
    WhatsApp-Image-20160704.jpeg
    19.7 KB · Views: 82
patamu hapo... yaani ni wakati muafaka maana mahakama yao ipo tayari.

hawa ndio wahujumu uchumi na mafisadi.
 
Hivi ile mahakama ya mafisadi inafika mpaka zanzibar mwaka huu wote tutaisoma namba
 
“jino kwa jino,jicho kwa jicho” in sheikh ilunga kapungu's voice.
Hii inatwaga kula sahani moja!
 
Kwa huku zenji sijui nani atabaki maana huku hakunaga wizi wala ubadhirifu bali ni mwendo wa kugawiana mali ya umma kwa mwendo wa nasaba tu nashangaa leo wana ndugu wanataka kugeukana?
Ufusadi wa zenji it is an open secret!
 
Back
Top Bottom